Mwenda pole hajikwai
JF-Expert Member
- Oct 24, 2018
- 290
- 212
Acha kumfundisha roho Mbaya mwenzioAchana nae. Utapita Kipindi kigumu cha kumkumbuka ila itafika hatua. Hata kumuona utakuwa hutaki

Muhumu kuweza kumove on aiseeeHabari zenu?
Kwanza napenda kuwashukuru wale wote wanaojitahidi kutoa ushauri kwa watu wenye matatizo mbalimbali. Kuna muda mtu unahitaji kuongea tu ili upate ushauri ila unapokosa mtu wa kukusikiliza ndipo hupelekea hata kujiua na kufanya mambo ambayo hukuwahi kufikiria kuyafanya.
BACK TO TOPIC
Mimi ni mwanamke mtu mzima mwenye miaka 28. Katika safari yangu ya mahusiano nimewahi kudate na wanaume wawili. Huyo wa kwanza sikuwahi kumpenda na yeye hakuwahi kunipenda. Tatizo lipo kwa huyu mtu wa pili.
yeye tumefahamiana naye miaka kumi sasa ingawa safari ya mapenzi ilidumu kwa miaka mitatu tu mapak 2017. Kutokana na mimi kufahamika kwao na yeye kufahamika kwetu, kuna undugu ambao ulianza kujitokeza hata kabla ya sisi kuunganishwa na Mungu. Kushirikiana kwenye mambo ya kijamii, kusaidia na kwenye magonjwa, kushirikiana kwenye sherehe nk. Vitu hivi vilitufanya tuwe karibu sana na ex wangu.
Tulikaa chini tukayaongea na yeye akaweka wazi kuwa katika watu asiowafikiria kua nao tena ni mimi hivyo tunaweza kuwa best friend kama kawaida. Na kweli tuilishirikiana sana sana sana kwa muda wa miezi kama mitatu au minne. Yeye akinishirikisha vitu vyake vya ndani hata vinavyomuhusu girlfriend wake nami nikimuhusisha katika baadhi ya mambo.
Ugumu ulianza pale ambapo kila jamaa anapolewa, ananiambia ananipenda anaitaka nk. Na msema kweli mpenzi wa Mungu, mimi nampenda sana huyu kaka ila naenjoy hata kuwa rafiki nae inatosha.
Mara mbili tatu tulifanikiwa kuvunja amri ya sita pasipo kupanga. Yalipotokea hayo, ex akaniomba kuwa inabidi tuanze kudate lakini tutakua pamoja na yule girlfriend wake yaani tuwe wawili ingawa huyo girlfriend wake hajui uwepo wangu ila ananifahamu kwa kunisikia kua nilikua na huyo jamaa kwa muda tena in serious relationship.
Mara ya kwanza aliponiambia swala la kuwa nae, nilimuomba aniache kwanza nifikirie. Baada ya siku ya pili nilimuambia wazi kuwa mapenzi ya nmana hiyo yasiyo na dira mimi siyawezi. Kama ananitaka kweli achague moja, either tubaki kwenye serious relationship au tuendelee kuwa marafiki tena tunaoheshimiana.
Cha ajabu mwenzangu amekasirika na nikimtumia ujumbe hajibu wala kupokea simu yangu.
Asubuhi ya leo amenipigia na kuniambia hawezi kuwa rafiki nami kwa kua kila anapokua nami anapata hisia za kimapenzi hivyo kujiepusha ni bora tukatengana.
Guys i feel bad kumpoteza mtu ambaye tumesaidiana naye kwenye kila hali na bado anaendelea kunisaidia hata baada ya kuniambia hivyo.
Naombeni mnishauri kwa vyovyote vile jamani.
Akishaachana nae pesa za kulia bata utampa wewe? Watu wazima tushaelewa hapo jamaa yuko vizuri kifedha na ukizingatia hali ya hivi vyuma hapo ye akomae nae tu mpaka kieleweke akimuacha tu wadangaji wanampitiaAchana nae. Utapita Kipindi kigumu cha kumkumbuka ila itafika hatua. Hata kumuona utakuwa hutaki
Huamn kama n mm enhe?Eti umesema!!
Huamn kama n mm enhe?
Ha ha ha ha ha twende nkupeleke mbinguni basiKweli hata shetani akizeeka anakuwa malaika.
huyu ni killazza fullMiaka 28 hujitambui wewe vipi kuwa na akili hata kidogo watu wanaolewa mpaka 40 yrs sasa 28 unakuwa wa hivyo, miaka 20 mwanamke unajitambua acha hizo
Meridah Tough
inasikitisha sana kuwa una umri mkubwa lakini akili ni ya kitoto sana.
Amekuweka wazi kuwa hamuwezi kuwa pamoja yaani kuoana, na ana mpenzi wake na bado unamng'ang'ania!
Unapoteza muda kumpenda asiyekupenda.
Fungua moyo wako kwa mpenzi mtarajiwa ili aingie, achana na asiyekupenda
Alikuwa anataka uendelee kumpa kitumbua chako . Kama unaweza endelea kumpa kitumbua jamaa atakuwa na njaa Kali .Habari zenu?