ex-girlfriend anataka nizae nae | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ex-girlfriend anataka nizae nae

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kifyoga b, Mar 17, 2011.

 1. k

  kifyoga b Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ni baba wa familia(nimeoa) kabla ya kuoa nilikuwa na rafiki yangu wa kike ambae nilidumu nae kwa miaka mitatu hivi. nilipokuwa tayari kuoa nilimtaarifu mwenzangu kuwa nataka kujitokeza kwao aliniambia kuwa kwa wakati huo hayupo tayari kuolewa kwa sababu bado hajajiandaa na wazazi wake hawawezi kukubali na pia alikuwa na plan ya kuendelea kusoma. kwa sababu nilikuwa nimeweka malengo yangu kuwa ikifika age fulani nioe nilichukua uamuzi wa kutafuta mtu mwingine aliyetayari kuolewa na mungu si athumani nikampata. baada ya kumpata nilitumia busara yangu kumjulisha kuwa nimeamua kutafuta mwingine aliye tayari kuolewa na nimeshampata so no need kuendelea kuwa na mahusiano nae, alikubali ingawaje kwa shingo upande na kwa kulia sana baada ya hapo tuliendelea kuwasiliana kama marafiki wa kawaida kwa sababu hatukugombana. sasa ni miaka mitatu imeshapita ametokea kuwa karibu tofauti na ilivyo kawaida na pia amekuwa akilalamika kila siku kuwa boyfriend wake hamkidhi mahitaji yake(sex) nimekuwa nikimshauri awe mvumilivu na ampeleke kwa washauri wa mahusiano lakini kali ni last week alipoanza kuniambia live kuwa hatokuwa na maana yoyote kama hatozaa nami maana ni mwanaume pekee ambaye nimebaki na nafasi katika moyo wake so anachoomba yeye si kurudiana bali niweze kuzaa naye ili iweze kuwa kumbu kumbu yake for rest of her life, kwangu imekuwa ni mtihani sana kwa sababu ya urafiki wetu hata baada ya mimi kuoa. ushauri wenu wanajf
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  We unaonaje hadi hapo uko tayari kuzaa nje ya ndoa au?
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Umeoa na una familia, lazima ujue cha kufanya wewe ni mtu mzima hivyo mwambie haiwezekani kama una kifua...fikiria mbele zaidi ya hatua ya mguu wako mana utajitakia matatizo..
  Mtu unaejali familia na kuipa kipaumbele sidhani jambo kama hili litakusumbua kuamua labda kama na wewe unataka kuzaa nae.
   
 4. P

  Pomole JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hilo ni jambo binafsi zaidi,ushauri wa kuzaa nae au hapana unao mwenyewe na imani yako ktk ndoa yako!!!Kama ndoa yako ni takatifu basi ilinde ndoa yako na kutochakachua nje!!!Ukiweza mshirikishe mkeo kama atakuruhusu ila kama hawezi siku akija gundua umezaa na mtu wakati ushamuoa ugomvi ni mkubwa na yeye ataweza kukuzalia na bwana mwingine!!!mwambie asake wa kwake ila sikukatazi kuzaa kimtindo
   
 5. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  dah, kutembea na mwanamke mwingine tu nje ya ndoa,
  ni sumu kali sembuse kuzaa kiongozi?
  hebu peperusha mbali hizo fikra!!!!!!!!!
   
 6. W

  Wakuchakachua JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmh:hatari:
   
 7. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tuna masuala mengi muhimu ya kushauri hili lipo ndani ya uwezo wako. Kwa ufupi mpe msimamo wako kuwa kwa sasa hana nafasi na huna mpango wa kuzaa nje ya ndoa.
   
 8. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  upo wewe mdada,
  hebu ingia kule kwenye chat room,
  kuna ujumbe wako mzito!!!
   
 9. Mamuu55

  Mamuu55 Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeoa kaka tulia na wako usihangaike utadhurika bure
   
 10. Mamuu55

  Mamuu55 Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ungemtumia PM ingekuwa bora
   
 11. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Jamani hizi shule zinawacost wasichana wengi sana sasa kwani ungemuoa ungemkataza kusoma? ona sasa anavyotaka kuharibu maisha yake kuliko hata angeolewa kipindi hicho nyuma, sasa hapo embu angalia hili la kuzaa na kama angeolewa kipindi kile kipindi kile kipi wazazi watakasirika zaidi? mwanzo alikuharibia plan za maisha ukakubaliana mkaachana sasa unamkaribisha tena jitayarishe na mparagano wa ndoa yako
   
 12. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Wewe umesahaamua kuoa na kuacha zinaa sasa mbona unataka kurudi ulikotoka ?:juggle:
   
 13. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  tunajuanana huyu, wa ubani wangu!!!!!!!
   
 14. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mkuu,
  Heshimu ndoa yako! Na kama ni mkristo inabidi ujitahidi umsahau huyo dada, na ningekushauri upunguze ukaribu naye kwa kadiri inavyowezekana.
  Kwa maelezo yako inaonesha bado mpo karibu kimawasiliano. Ningependa nikushauri umwache huru ajiamulie mambo yake mwenyewe. Akutafute kama ana shida za kibinadamu za kawaida, tena akushirikishe mbele ya mkeo.

  Inawezekana kweli ulimpenda, ni kweli, lakini mwangalie pia mkeo. maana akifahamu utamweka katika mazingira magumu na kuhatarisha ndoa yako nzuri.
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mwambie haiwezekani!!Kama ambavyo yeye hakutaka kuharibiwa maisha yake huko nyuma ndivyo atakavyokuharibia ya kwako sasa hivi au mbeleni!!Kua mwanaume!!!:embarassed2:
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Angalia upande wa pili wa shilingi.
  Mkeo angekufanyia haya, ungejiskiaje?

  kwamba, wewe humridhishi, na hajiskii raha ya maisha bila
  kumzalia mtoto huyo ex-boyfriend.
   
 17. The Inquisitive

  The Inquisitive Senior Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mpendwa, kugonga thanks mara mbili hairuhusiwi hivyo naomba nikupe thanks nyingine. Umemaliza kila kitu!

  Kifyoga b, hizo hila za shetani kaa nazo mbali kabisa!
   
 18. F

  FUSO JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  kuzaa?, ina maana utapiga kavu wakati una wife nyumbani? ..... kazi ipo.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ndo mwanzo wa kujitafutia matatizo na nyumba kubwa

  Mpotezee tu kama vp kazae na nyumba kubwa
   
 20. n

  ngoko JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuendelea na ukaribu inaonyesha bado mnahitajiana , kama hutaki kuleta balaa nyumbani ebu weka gap kubwa la mawasiliano. Otherwise fanya kadri roho yako inavyotaka
   
Loading...