EWURA yasitisha bei ya maji kupanda Kahama

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
EWURA yasitisha bei ya maji kupanda Kahama

Na Patrick Mabula, Kahama

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imesimamisha kusudio la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka ya Wilaya ya Kahama (KUWASA) juu ya ombi lake la kutaka kuongeza gharama ya akra ya maji kwa wateja wake.Katika kikao
cha wadau wa maji kilichoitishwa na EWURA wiki hii, mamlaka hiyo ilikataa sababu zilizotolewa na kuainishwa na KUWASA kuhusu kuwaongezea gharama za maji wateja wa Kahama.

EWURA ilisema hatua hiyo imekuja baada ya KUWASA kuonekana na dosari za kiutendaji, ikiwemo mahesabu yake kutokaguliwa tangu kuanzishwa kwake.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Mutaekulwa Mutegeki alisema kabla ya kikao walishapitia sababu zilizotolewa na KUWASA juu ya kusudio na maombi yao juu ya kuongeza bei na kuona zina mapungufu mengi.

Katika kikao hicho wananchi na wateja wanaopatiwa huduma hiyo walipinga kuongezewa gharama za malipo ya maji, zikiwemo za kuingiza huduma hiyo majumbani mwao.Walisema tangu mradi huo uzinduliwe miaka miwili iliyopita hata gharama wanazotozwa katika akra zao ni kubwa, na hivyo kuiomba EWURA iwapunguzie kwa kuwa maji hayo hawayatumii kibiashara.

Awali katika taarifa yake, Meneja wa KUWASA wa Wilaya ya Kaham, Bw. Joel Rugemarila alisema mamlaka yake inakabiliwa na changamoto nyingi za uendeshaji ndiyo maana wanataka gharama ziongezwe.

Katika kikao hicho wananchi na wateja wanaopatiwa huduma hiyo walipinga kuongezewa gharama za malipo ya maji, zikiwemo za kuingiza huduma hiyo majumbani mwao.Walisema tangu mradi huo uzinduliwe miaka miwili iliyopita hata gharama wanazotozwa katika akra zao ni kubwa, na hivyo kuiomba EWURA iwapunguzie kwa kuwa maji hayo hawayatumii kibiashara.

Huu ni mradi wa Lowassa alipokuwa Waziri wa maji................ulikuwa ni mradi wa ulaji sasa hauwezi kujiendesha mwisho wake itabidi hazina itoe ruzuku tu iuendesha au ufungwe.....................It is a white elephant................lengo lilikuwa ni kujipatia kipato cha bwerere........sasa uendeshaji haiwezekani............EWURA hata wakigoma kupandisha lakini itafika mahali aidha wapandishe au madi ufungwe................gharama za uendeshaji zinazidi mapato.......suala la mahesabu halitoshi kufunika huu ukweli......................
 
Back
Top Bottom