Ewura wameshindwa kazi ivunjwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ewura wameshindwa kazi ivunjwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rimbocho, Jul 5, 2011.

 1. r

  rimbocho Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana jf. Ni wiki chache zimepita toka waziri wa fedha atangaze bajeti ya nchi iliyo kuwa na mambo kadhaa moja wapo ni la kuongeza kodi katika mafuta ya taa na kupunguza kodi kwa petroli na diseli lengo likiwa ni kufuta kabisa tatizo la uchakachuaji. Nionavyo mimi na ndivyoilivyotakiwa kuwa kwamba kabla ya maamuzi haya lazima wizara ilikutana na wataalamu wa ewura na kujadiliana ndio wakafikia maamuzi haya. Chakushangaza mpaka sasa baada ya bei ya ewura kutangazwa vituo vyote vimetupilia mbali mapendekezo ya kushusha bei na kupandisha bei kama ewura na wizara ya fedha ilivyotaka. Kwa sasa bado mafuta ya taa yanauzwa kwa bei ya chini kuliko diseli na petroli, je huu si ushahidi tosha kwamba hawa ewura hawaijui sekta hii ya nishati wanayotakiwa kuiongoza? Je ni kweli kuondoa hii kodi iliyopendekezwa na wizara na ewura kutapunguza bei ya mafuta? Au kunamchezo humo ndani wa kuwanufaisha wafanyabiashara na kuikosesha serikali mapato hatimaye mlala hoi akose dawa hospitali?

  Kwa maoni yangu
  1. Ewura na wizara walitakiwa kukutana na wadau wa nishati na kujadili suala la uchakachuaji na kupata suluhisho
  2. Kabla ya kuongeza kodi katika mafuta ya taa ilitakiwa watoe mbadala wa mafuta ya taa ambayo hutumiwa na 97% ya watanzania.
  3. Kodi iliyoongezwa katika mafuta ya taa ingetolewa katika gesi.
  4. Serikali ingetoa elimu ya matumizi ya biogesi bure vijijini kwa wale wenye mifugo.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa ni kushuka kwa thamani ya Tshs against USD ambayo ndio inatumika kununulia hayo mafuta...last week 1500 na leo ni zaidi ya 1600
   
 3. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hivi hamjui kama kupanda kwa bei ya mafuta, maji na umeme kunainufaisha EWURA? Kwa mfano EWURA inapata 1% kwa kila kiasi kinacholipwa na mteja wa TANESCO, bei ya umeme au mafuta ikipanda na wao mapato yanapanda kama wafanyabiashara. Hivyo naona hawa wanafanya mazingaombwe tu. Hizi hela zinawafanya watanue bila kufanya kazi yo yote ya maana kwa mwananchi wa kawaida. nashauri wapatiwe fedha za kuendeshea shughuli zao moja kwa moja toka kwenye bajeti ya serikali ndipo watakapoweza kudhibiti bei ya huduma hizo kikamilifu, vinginevyo bei za nishati zitaendelea kupanda kila siku na inawezekana wanashirikiana na waingizaji wa mafuta.
   
 4. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  EWURA!
  Wanataka kutengeneza faida tu hao. Hawapo kwa ajili ya wananchi bali 'wenyenchi'. Kwanini watulinde sisi wakati maumivu yetu ni nafuu kwao?
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  EWURA!
  Wanataka kutengeneza faida tu hao. Hawapo kwa ajili ya wananchi bali 'wenyenchi'.
  Kwanini watulinde sisi wakati maumivu yetu ni nafuu kwao!?
   
Loading...