EWURA, Symbion na TANESCO

kongomboli

Senior Member
Apr 11, 2011
155
34
Yakaribia wiki moja sasa tangu ewura watoe tangazo la pingamizi kwa mtu yeyote dhidi ya symbion power kwani wanataka kupewa leseni ili waiuzie TANESCO umeme.Wakati huohuo Symbion wamesema mitambo imekamilika na wapo tayari kuunganisha umeme wao kwenye grid ya taifa mara tu watakapopewa leseni na ewura.

Jambo la kushangaza ni kwamba tayari Tanesco wametangaza mgawo mkali wa masaa kumi mfululizo Tanzania nzima.

Swali:Je,huku sio kuhujumu watz tushindwe kuweka pingamizi dhidi ya symbion??!!

Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa kuna mchezo tunachezewa hapa! Nani sasa ataweka pingamizi ktk mazingira kama hayo yaliyotokea ndani ya wiki moja tu?!!

Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI!!!
 
Symbion, Dowans na Richmond wote Wamoja, Tusiongopeane!

Namshangaa sana Makamba(mtoto) kwa kuitetea kampuni hii! Lakin Naamin UKweli utajulikana!
 
Nakumbuka haohao walisema Richmond shwari, BOT (epa) shwari! Wakaja kuumbuka baada ya Mwanaume wa Shoka MWAKYEMBE Kufanya kazi nzito, Mmoja baada ya mwingine wakaanza kujiuzulu, Waangalie akina Makamba na Ngeleja Isije SYMBION Ikawaumbua nao
 
Dah inawezekana hii ni hujuma ya kutunyamazisha. Wapewe tu hiyo leseni. Huu mgao ni mkali hsijaeshi yoke. Saa 12 jioni hadi kesho yake saa 4 asubuhi.
 
Back
Top Bottom