Kilichomponza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hiki hapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi.

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Ngamlagosi amesimamishwa kazi kuanzia Juni 11, 2017.

Kilichomponza ni hiki. Mwishoni mwa wiki iliyomalizika Mamlaka hiyo ilitoa tangazo katika vyombo vya habari kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imepokea maombi ya kuongeza muda wa leseni ya kuzalisha umeme kutoka kwa kampuni ya uzalishaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) "Mwombaji".

Hivyo basi, EWURA ina uarifu umma na wadau mbalimbali kwa ujumla kuwasilisha maoni au pingamizi ili kufanikisha uchambuzi mzuri wa maombi haya.

Taarifa ilitolewa chini ya kifungu cha 19 cha sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, sura ya 414 ya sheria za Tanzania na kifungu cha 8 cha sheria ya umeme, sura ya 131 ya sheria za Tanzania.

Tayari wadadisi wa mambo wanahusisha kusimamishwa kazi huko kunatokana na tangazo hilo la kutafuta maoni ya wananchi ya kutaka kumuongezea mkataba IPTL.

Itakumbukwa kuwa Januari Mosi mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, katika hali inayoonesha kuwa Rais amekerwa na jaribio la (TANESCO) bei ya umeme.

Baada ya Mramba kutenguliwa nafasi yake alipewa Dk. Tito Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO) akimtoa chuo kikuu cha Dar es salaam alikokuwa akifundisha.

Rais Magufuli, alichukua hatua hiyo siku mbili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuiidhinisha ongezeko la asilimia 8.5 ya bei ya huduma za umeme kwa kilichoelezwa kuwa lengo ni kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.
 
Sawa kabisa hata mtoto mdogo anajua makosa makubwa waliyofanya IPTL, haikuhitaji maoni ya wananchi kuwapa au kuwanyima mkataba mpya, ilikuwa ni suala la kuwapiga chini na kutangaza tenda upya kwa mujibu wa sheria
 
Sheria ni sheria kama sheria inatamka kuwa atangaze angefanyaje?
Angewanyima leseni bila kutangaza public hearing angewapa loophole ya kukata rufaaa
Tuache siasa...ilikua fomalities kutangaza hata kama tunajua watakosa
 
Dah watanzania wengi tunachangia mambo tusiyoyajua. Mimi nilimsikia huyu mkurugenzi wa EWURA akihojiwa na Henry Magumo wa ITV . Alisema wao hawaongezi mkataba wa IPTL na kwamba IPTL mkataba wao unaisha mwaka 2020 au 2022 ( kama sijakosea) ila kilichoisha muda wake ni LESENI YAO YA BIASHARA. kwahiyo hata kama watapewa leseni mkataba wao utabaki palepale na hata kama hawatapewa mkataba uko palepale. Sasa tujiulize inawezekana mkataba ukawepo bila leseni? Je, kama hawa watu hawataongezewa muda wa leseni wataweza kuendelea na shughuli zao bila shida kisheria? Je kama serikali haitawaongezea muda wa leseni mpaka mwisho wa mkataba wao takuwaje?
 
wao wana mkataba mpaka 2022, lazma kwenye mkataba kuna kipengele cha kuvunja huo mkataba , asa inategemea kama hicho kipengele kilikuwa kwa ajili ya kuisaidia Tanzania au hao IPTL.

vinginevyo mamlaka haikuwa na namna zaidi ya kufwata procedures kama kutangaza, hayo ya kutumbuliwa ni matokeo tu. na tuone baada ya kutumbuliwa je hawataongezewa.?
 
Dah watanzania wengi tunachangia mambo tusiyoyajua. Mimi nilimsikia huyu mkurugenzi wa EWURA akihojiwa na Henry Magumo wa ITV . Alisema wao hawaongezi mkataba wa IPTL na kwamba IPTL mkataba wao unaisha mwaka 2020 au 2022 ( kama sijakosea) ila kilichoisha muda wake ni LESENI YAO YA BIASHARA. kwahiyo hata kama watapewa leseni mkataba wao utabaki palepale na hata kama hawatapewa mkataba uko palepale. Sasa tujiulize inawezekana mkataba ukawepo bila leseni? Je, kama hawa watu hawataongezewa muda wa leseni wataweza kuendelea na shughuli zao bila shida kisheria? Je kama serikali haitawaongezea muda wa leseni mpaka mwisho wa mkataba wao takuwaje?
bora umefafanua vizuri.
 
Sheria ni sheria kama sheria inatamka kuwa atangaze angefanyaje?
Angewanyima leseni bila kutangaza public hearing angewapa loophole ya kukata rufaaa
Tuache siasa...ilikua fomalities kutangaza hata kama tunajua watakosa
Tatizo la mamlaka za kuteua na kutengua huwa hawatuelezi makosa ya wanaosimamishwa kazi. Nivyema tukapewa makosa au tuhuma zao ili tupunguze hisia za kuonewa kwa wahusika
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi.

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Ngamlagosi amesimamishwa kazi kuanzia Juni 11, 2017.

Kilichomponza ni hiki. Mwishoni mwa wiki iliyomalizika Mamlaka hiyo ilitoa tangazo katika vyombo vya habari kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imepokea maombi ya kuongeza muda wa leseni ya kuzalisha umeme kutoka kwa kampuni ya uzalishaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) "Mwombaji".

Hivyo basi, EWURA ina uarifu umma na wadau mbalimbali kwa ujumla kuwasilisha maoni au pingamizi ili kufanikisha uchambuzi mzuri wa maombi haya.

Taarifa ilitolewa chini ya kifungu cha 19 cha sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, sura ya 414 ya sheria za Tanzania na kifungu cha 8 cha sheria ya umeme, sura ya 131 ya sheria za Tanzania.

Tayari wadadisi wa mambo wanahusisha kusimamishwa kazi huko kunatokana na tangazo hilo la kutafuta maoni ya wananchi ya kutaka kumuongezea mkataba IPTL.

Itakumbukwa kuwa Januari Mosi mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, katika hali inayoonesha kuwa Rais amekerwa na jaribio la (TANESCO) bei ya umeme.

Baada ya Mramba kutenguliwa nafasi yake alipewa Dk. Tito Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO) akimtoa chuo kikuu cha Dar es salaam alikokuwa akifundisha.

Rais Magufuli, alichukua hatua hiyo siku mbili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuiidhinisha ongezeko la asilimia 8.5 ya bei ya huduma za umeme kwa kilichoelezwa kuwa lengo ni kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.

Inawezekana maana sasa hivi naona wamesitisha kupokea maoni.

Ila wanaposimamisha watu kazi wawe wanasema na sababu basi.
 
Back
Top Bottom