Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Wakati Mkurugenzi aliepita wa TANESCO Felchesmi Mramba akianza mwaka kwa kukosa kazi, TANESCO inaendelea na mchakato wa kuangalia ni vipi itoze gharama za umeme nchini.
Lakini tukirudi nyuma mwezi Mei mwaka jana, kampuni ya uzalishaji umeme ya Symbion ilieleza kusudio lake la kuishtaki TANESCO mahakama ya kimataifa nchini Ufaransa kwa kusitisha mazumguzo ya kurekebisha mkataba wa miaka 15 wa uzalishaji umeme kutoka Symbion.
Mkataba huo ulo ndani ya mpango uitwao PPA unahusu kampuni binafsi za kufua umeme ambazo zitaiuzia umeme Tanesco kwa kuingiza kiasi cha umeme huo katika gridi ya taifa.
Kwa mujibu wa mkataba huo ambao ulisainiwa tarehe 10 December mwaka 2015 umeme wa kiasi cha MW112 ungeuzwa kwa TANESCO hadi mwaka 2030.
Kampuni ya Symbion ilipata leseni ya kufanya shughuli za ufuaji umeme mnamo tarehe 7 ya mwezi huohuo wa December, leseni ambayo iliridhiwa na EWURA, pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali wa serikali.
Wizara ya Madini na Nishati haikuwa imepata waziri kwa kuwa raisi JPM alikuwa akiandaa baraza lake la mawaziri baada ya kuapishwa hivyo kuwepo na uwezo kwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa wakti ule kuidhinisha leseni hiyo kwa niaba ya serikali.
Mwanasheria wa TANESCO bwana Godson Makia ambae kwa wakati ule alikuwa akikaimu nafasi hiyo alisaini mkataba huo kwa niaba ya TANESCO na kwa upande wa Symbion ulisainiwa na mkurugenzi mtandaji Dr Wagesverom Subramaniam, na mhasibu wao bwana Gosbert Mutagaywa.
Lakini mwezi April mwaka 2016 bwana Mramba (labda kwa maelekezo ya Ikulu baada ya kuitwa kwenye kikao) akawaandikia barua Symbion ya kuwataarifu kwamba mazungumzo ya kuhusu PPA "power purchasing agreement" yamesitishwa mpaka hapo maagizo mengine yatakapotolewa na serikali.
Baadhi ya maneno ya Mramba katika barua hiyo yanasema kwa kiingereza kwamba, "We wish to inform you that TANESCO has formally withdrawn from being party to the intended PPA [power purchasing agreement],” aliandika na kuendelea
“You will recall that TANESCO and Symbion were negotiating a long-term power purchase agreement which would have been executed subsequent to issuance of necessary approvals from the government and other relevant authorities.
TANESCO is in receipt of categorical directives from the government to suspend the execution of the intended PPA on any party thereof as from the date of this letter,” ilieleza barua hiyo.
Baada ya barua hiyo tarehe 10 mwezi Mei Symbion wakaandika barua kwenda kwa waziri Profesa Muhongo, mwanasheria mkuu wa serikali na Ikulu kulalamika kwamba labda wameuziwa mbuzi kwenye gunia.
Symbion wakaendelea kudai kwamba TANESCO walikuwa wa deni kwa Symbion kwa kisingizo kwamba suala la PPA bado lipo mezani (hapa tuchukulie ni Wizarani na Ikulu).
Ikumbukwe kwamba mwezi huo wa Mei waziri Muhongo, alikuwa tayari amekwisharudi wizarani hapo, George Masaju alikuwa amechukua nafasi ya mwanasheria mkuu wa serikali.
Pia itakumbukwa kuwa mwezi June katika kikao cha bunge la bajeti Waziri Muhongo alikijibu suali bungeni kuhusu deni la TANESCO Profesa Muhongo alikiri kwamba deni la TANESCO ni kubwa na limesababishwa na uongozi dhaifu, rushwa, wizi na mikataba mibovu ambayo TANESCO imeingia. Alisisitiza kwamba hakuna mkataba unaolinufaisha Taifa.
Sasa kuna masuali kadhaa ya kujiuliza.
1. Je, ni kwanini EWURA na mwanasheria mkuu wa serikali wa serikali ya awamu ya nne waliridhia leseni ya Symbion harakaharaka ndani ya mwezi mmoja?
2. Je ni kwanini bwana Felchesmi Mramba alimwachia bwana Godson kwenda kusaini mkataba mkubwa kama huu (bado haijathibitika kama Mramba alikuwepo kwenye utiaji saini) siku ya tarehe 10 December.
3. Je, inawezekana bwana Mramba alikuwa akisukumwa na nguvu ya gizani kiasi cha kutoelewa anafanya nini kwa maslahi ya taifa hili?