EWURA haina msaada kwa Watanzania, bora ifutwe tu

EWURA haina msaada kwa Watanzania, bora ifutwe tu

Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizopo EWURA walifuata taratibu zote za muhimu katika kuridhia kupandisha bei ya umeme, ambapo hapo awali TANESCO walitaka ongezeko la 18% lakini hatimaye baada ya mchakato EWURA walikubali ongezeko la umeme kwa 8.5%.

Kwa Mtendaji Mkuu wa EWURA tangazo la ongezeko hilo lilikuwa ni la kawaida kama ambavyo huko nyuma wamekuwa wakiongeza ama mara nyingine kupunguza bei za umeme, maji, gas, mafuta n.k

"Wakati huo" huko nyuma walifanya kazi kwa mujibu wa taratibu na bila kufikiri athari za nini kitatokea kwa maamuzi wanayo yafanya lakini baada ya tamko lao la jana la kupandisha bei ya umeme na matukio yaliyofuata baada ya tangazo hilo ni wazi kuwa kwa sasa taasisi hii imebaki kwenye "dilema" hawajui kama walikose ama walikuwa sahihi.

Nina mashaka kama kuna umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa taasisi hii kwani kwa sasa hawawezi tena kuwa huru wala hawawezi kufanya kazi kitaalamu na ufanisi bila ku"consult" wanasiasa na wale waliowateua.

Ni maombi yangu kwa Mh. Raisi aangalie upya kama kuna umuhimu tena wa kuwa na taasisi kama EWURA maana kama maamuzi yanayofanywa na EWURA yanawezwa kutenguliwa tu kwa tamko la Waziri ni bora kazi za EWURA zikawa zinafanywa na kitengo tu cha wizara ili kuokoa kodi nyingi tunazotozwa bila sababu za msingi.

Nawatakia heri ya mwaka mpya 2017.

Kinyungu
Hapo umenena ndg,kwa watu waelewa watakuwa wamekuelewa vzr.
 
Ndo maana hatuwezi kuendelea kw hali hii ya vyombo husika kunyimwa uhuru wa kuamua na pia pale ambapo wanaonekana wanaamua vibaya ni vyema kushauriana na sio kutumbuana kw masifa
 
Hapa kuna double standard zinatumika. Nchi inaendeshwa kikanda,kikabila na kidini.

Matamko karubia asilimia kubwa yanatolewa makanisani, je nyumba za zimekuwa majukwaa ya kisiasa kwa utawala huu?

Tanzania haitaendelea kwa utawala huu wa milipuko.
 
unakosea kusema EURA haina faida kwa watanzania SEMA HIVI eura haina manufaa kwa wanaUKAWA maana nyie ni wapinga maendeleo ya nchi hii......Naikubali EURA,huwezi shusha mafuta bcoz ww umenunua passo 1989. lazima ihakikishe inapandisha makusanyo ya nchi.
Hi
Hivi wana UKAWA ni foreigners??
 
Huyo Jamaa anayetetea ewura ni
Yule wa futuhi anavaaga mashati marefu wa kukurupuka
 
unakosea kusema EURA haina faida kwa watanzania SEMA HIVI eura haina manufaa kwa wanaUKAWA maana nyie ni wapinga maendeleo ya nchi hii......Naikubali EURA,huwezi shusha mafuta bcoz ww umenunua passo 1989. lazima ihakikishe inapandisha makusanyo ya nchi.
Chadema tena..?
 
Back
Top Bottom