Mkuu ili suala ni kubwa mi nshamuachaga Mungu maana unajaza mafuta lakini unatembea kwa hofu
EWURA hawawezi kamata huo uwizi kwasababu anaeibiwa ni mteja na mwizi ni muuza mafuta na sio sheli. Wenye magari huibiwa kilaini sana kwasababu hashuki kwenye gari kuangalia kilichoandikwa kwenye pamp. Mfano km umeomba mafuta sh50000, bas muuzaji anakusoma kwanza je ulivyo akiona haushuki kusoma pamp ataandika 30000 shap na kuweka mafuta alafu anafuta tarakimu ili usione. Na atakuambia sogeza gari mbele. Na kwa vile kuna jam utalipa fasta 50000 yake na kuondoka.Nipo mjini Morogoro, siku kadhaa zilizopita nilikwenda kununua petroli kwenye kituo cha mafuta kilichopo opp na stand ya Dodoma, ambapo bei zao kwa lita ni shilingi 2348 kwa lita, mafuta hayo yalikwisha baada ya mizunguko yangu ya kilomita kadhaa na nikapata hofu, jana nikahamia kituo kingine kilichopo na eneo hilohilo, mafuta niliyopata yalinifikisha umbali uleule wa juzi na yakabaki, nikapata wasiwasi kwamba kituo kimoja kinafanya ujanja.
Leo nimekutana na mdau vijana wawili wanaouza mafuta ya kupima kwenye chupa, vijana hao hununua mafuta kwenye vituo hivyo viwili tofauti, leo walipokutana wakawa wanapeana uzoefu kuwa wakinunua mafuta ya shilingi 56000 kwenye kituo kinachouza mafuta kea bei ya juu wanapata lita 22.29 lakini kwenye kituo kinachouza mafuta kwa bei ya chini wanapata mafuta pungufu zaidi, kitu kinachoashiria kuwa kuna wizi unafanyika.
Kwa scenario hizo mbili, mkasa wa kwangu na wale vijana wawili ninajifunza kuwa EWURA mnatakiwa kufanya ukaguzi wa kushitukiza kubaini ujanja unaofanywa na vituo vya mafuta, nimejifunza pia kuwa wengi wa wahanga wa wizi huu ni wanunuzi wanaoweka mafuta kwenye matanki ya magari moja kwa moja, wenzetu wanaonunua kwenye madumu wanaweza kubaini mchezo huo mchafu kwa urahisi zaidi.
EWURA hawawezi kamata huo uwizi kwasababu anaeibiwa ni mteja na mwizi ni muuza mafuta na sio sheli. Wenye magari huibiwa kilaini sana kwasababu hashuki kwenye gari kuangalia kilichoandikwa kwenye pamp. Mfano km umeomba mafuta sh50000, bas muuzaji anakusoma kwanza je ulivyo akiona haushuki kusoma pamp ataandika 30000 shap na kuweka mafuta alafu anafuta tarakimu ili usione. Na atakuambia sogeza gari mbele. Na kwa vile kuna jam utalipa fasta 50000 yake na kuondoka.
Binafsi nilidhani EWURA, kwakuwa sijawahi kusikia kitu inaitwa wakala wa vipimo maana hasikiki kabisa na wala hajitangazi ili afikishiwe malalamiko kama haya
Hivi hapo ni Ewura au wakala wa vipimo?
Hapa ni wote wanahusika Mkùu...
Pole sana mkuu.
Hayo yapo sana. Mi huwa nahisi wauza nafuta wanazichezea pump kiasi kwamba hata wakaguzi wa vipimo huwa hawang'amui ama wanakula nao maana utakuta ukaguzi wameufanya jana na kuweka stika zao/ wakala wa vipimo lakini bado hakuna mabadiliko.
Ina kera sana hii hali.
Zipo baadhi ya vituo vya njia kuu kama korogwe ni shida. Kila leo nalazimika kuhama kituo.
Mbinu mojawapo ni pale unapouziwa mafuta kwa kuynganisha. Utaratibu ni lazima arudishe mkono wa pump mahali pake mpaka receipt ya mteja aliyetangulia itoke. Vinginevyo anakuunganisha na bili iliyopita.
Wakala Wa vipimo ndo mhusika Mkuu wa hizo pumpHapa ni wote wanahusika Mkùu...