Ewe mwanaume, kwanini umdhalikishe mke wako?

Ewe mwanaume, kwanini umdhalikishe mke wako?

Bernard bakari

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2016
Posts
407
Reaction score
781
Zipo Tabia hufanywa na baadhi ya wanaume zenye lengo na dhamira ya kumdhalilishe mke au mpenzi wake. Huwa najiuliza mwanaume anawezaje kuwa na roho ya kumdhalilisha mke wake au mpenzi wake mbele za watu.

Kitendo cha mwanaume kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine tena katika eneo ambalo wanajua fika una mke wako ni njia mojawapo ya kumdhalilisha mkeo. Watu humtazama mkeo kama si chochote si lolote ndiyo maana unahangaika. Mkeo hakuridhishi anaonekana kituko mbele za watu.

Pili kitendo cha kutoa madhaifu ya mke wako au mpenzi wako mbele za watu yawezekana marafiki au watu wa karibu ni kumdhakilisha pia. Mwanaume bora hukabiliana na changamoto hutatua matatizo yake mwenyewe, huficha madhaifu ma kasoro za mke wake machoni pa watu.

Hatua ya kuinua mikono yako na kumpiga mkeo tena kwenye nyumba za kupanga mtaa mzima wanajua ni udhalilishaji tosha. Humfanya mwanamke kuwa mnyonge na kukosa Amani hujisikia aibu kwa watu na kukosa ari na moyo wa kufanya mambo yake machoni pa watu. Humpunguzia kujiamini mbele za watu.

Wanaume tunao wajibu wa kuhakikisha wanawake wetu na wengine pia wanatengenezewa mazingira salama ya katika maisha yao. WANAWAKE BILA KUDHALILISHWA HUWAFANYA KUWA BORA NA WENYE KUJIAMINI SIKU ZOTE ZA MAISHA YAO
 
Hivi mpk leo kuna wanaume wa namna hiyo??? Labda wanywa mataputapu
 
Heri umpige kama amekukosea saana kwa kiwango kikubwa kuliko Kutoa madhaifu yake, tena kwa mchepuko!!!

Huo ni ushamba kabisa wa kiwango cha hekta 4000.

Kubali au kataa, mwanaume imara hawezi kusema madhaifu ya mke mbele ya watu au mbele ya mchepuko.
 
Back
Top Bottom