Ewe mwanadada wa humu JF soma hii na uelewe

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,909
Binti yangu nisikilize mimi...

1. Mwanaume atakaekutambulisha kwa wazazi wake na si kwa rafiki zake pekee huyo ndiye mwenye mwelekeo wa kufanya maisha na wewe.

2. Usitizame gari wala pesa nyingi ukadhani ndio kipimo cha utajiri wa mwanaume, ndoto na maono yake yenye tija ndio muelekeo mzuri wa utajiri wa mwanaume.

3. Binti yangu, ni wazi kwamba mwanaume anaweza akakupa talaka au kukufukuza kwake, ila elimu, ujuzi na kipaji hakiwezi kukupa talaka. Hivyo basi focus katika kupata elimu na ujuzi kabla hujampata mwanaume wako.

4. Binti yangu mpendwa, usikubali ngono ikufanye kuwa mama kabla ya ndoa kukufanya kuwa mke. Tangulia kwanza kuwa mke ndipo uwe mama.

5. Wanaume bora sio vigumu kuwapata, ila ni vigumu kuwavutia. Hivyo basi kama unataka mwanaume bora jiandae kumvutia. Si kumvutia kimapenzi! La hasha binti yangu..namaanisha kuwa na tabia na siha njema anayokufunza mama yako.

6. Matokeo ya kuwadharau wanaume walio bora na kujichanganya na wanaume matapeli ni kwamba utakuja kuchanganyikiwa, hasira na visasi pale utakapoona wale wanaume bora uliowadharau wanaoa wanawake ambao nao uliwaona kama sio wazuri kama wewe.

7. Binti yangu, kama utamuuliza Mungu ni nini kanuni ya uchumba ni rahisi tu; Kama huyo Mwanaume hana Mungu, basi hastahili kuwa na wewe.

8. Bibi yako enzi za ujana wake alikuwa mzuri kweli, sasa nakupa agizo hili, kila utembeapo tembea na picha ya bibi yako katika pochi yako. Ili kila utakapoifungua pochi picha itakukumbusha kwamba uzuri ni wa muda tu, ila tabia, hekima na busara zinadumu milele.

9. Jipende na ujitunze, wewe ni hekalu la mwenyezi Mungu, Mungu hatapenda kuona hekalu lake likichafuliwa.

10. Hakuna mpumbavu mkubwa kama mwanamke ambae anamdharau mwanaume kwa sababu ya hali yake ya kiuchumi aliyonayo kwa wakati huo.

Si mtumishi wa Mungu mwenye busara Nabii Zekaria aliyehoji kwamba, "Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo?" Tupilia mbali dhambi ya dharau. Ishi na watu vizuri na Mwenyezi Mungu wa baraka atakubariki
 
Hoja yako ya tano ni njema sana! Maana wanaume hawapendi majigambo na hawana kihelehele cha kujifanya wanauwezo na kitu Fulani! Na wanapenda wanawake wapole
 
10. Hakuna mpumbavu mkubwa kama mwanamke ambae anamdharau mwanaume kwa sababu ya hali yake ya kiuchumi aliyonayo kwa wakati huo.

hapo wanaume watakuunga mkono hatar JAMAN WATU WAFANYE KAZ HATA KUIBA PESA IPATIKANE TU
 
Kati ya vyote hapo namba 2 ndio kigezo pekee wanachotumia kina dada siku hizi kukubali mwanaume. Wakiona magari na outing kila weekend wanajua huyo ndio mwanaume kutokujua wengine kubadili magari ni sababu mafundi magari, watu wa car wash ama madalali. Akija kutahamaki keshapoteza muda na magari yameyayuka anabaki kuhangaika na waganga wa kienyeji.
 
Well said mkuu.
Ila walio wengi yataingia na kupitiliza. Lisibaki hata moja kichwani mwao.
 
Namba 8. Kama watatambua kuwa uzuri ni kitu cha muda tu na kinapita ungekuta wala hawalalamiki kuhusu kuolewa.
Namba sita(6) ndipo mabinti wengi wanapopotea kwa tamaa za muda mfupi.
 
ujumbe mzuri wakiufuata singo maza watapungua
Mkuu hii ni kwa wote waliomo na wale wanaoleta Maombi ya kutafuta wenza Humu. Kama kweli hayupo tayari kusamehe na Kusahau Ningewaomba wasahau kabisa kuingia kwenye Mahusiano. Mahusiano ni Taasisi inayojitegemea kabisa
 
Kweli, ila pia wasisahau ukiwa mvivu jiandae kuwa na wivu. Uvivu wako sasa ndio utakaokufanya uje kuwachukia wenzako wakati wanaendelea. Soma, Soma Soma haya mambo yapo itafika muda utafanya mpk utakimbia kitandn. Mm ni mwanamke sasa sio bint tena nakwambia coz nilishapitia yote unayopitia Sasa. Try to build your future now!!
 
Wanaume, mana mko bize kushauri wanawake tu kila uchao.,
Mkuu Taasisi zote Duniani zinazotoa misaada Kwenye Nchi zenye Majanga ni Kwa sababu ya Jinsi ya Ke, hivyo tunayaona Mtaani ni viashiria vikubwa kuwa Jinsi ya Ke inahitaji kusaidiwa kushauriwa kuangaliwa Muda wote bila kuchoka. Unaweza ukawa huoni kama linakuhusu wewe kama Wewe ila linaweza kumgusa zaidi ya Kumi katika Kaya zinazokuzunguka. Hivyo tusichoke kupaza sauti hata kama tukisemacho hatuonii kikipokelewa ipasavyo.

Mimi ni mmoja wa watu ambao najiuliza mpaka kesho kutwa kuwa "Kwa nini Mwanamke anajiuza Kingono""'...
 
Back
Top Bottom