Ewe mwanachuo jipange

Ewe mwanachuo jipange

GoPPiii.

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
1,792
Reaction score
3,079
Wazungu walituletea msemo 'if you fail to plan, you plan to fail' mwenzenu nilishindwa kuplan, japo ninajipa tumaini kuwa it is never too late, nina tumaini nitarekebisha kwa namna moja au nyingine.

Mimi ni mwanachuo na mambo yakienda vema basi mwakani nitakuwa nahitimisha, japo nina hofu na nitapambana vipi na hali ya huko niendako sababu ni kama nimechelewa kujipanga.

Mambo yamebadilika, upepo hausomeki huko baada ya chuo, ajira hamna kama zamani, pesa hazikamatiki. Ila nina amini kabisa una uwezo wa kujipanga kabisa kukabiliana na ugumu uliopo mbele kama tu utajipanga mapema.

Wanafunzi wengi wa chuo, 'BOOM HALIKAMATI BOOM' Hili ni kosa kubwa ambalo nimelifanya, boom la miezi miwili nilitumia kwa muda wa mwezi mmoja au mmoja na nusu. Serikali inatoa 8500 kwa siku, inamaanisha kuna siku nilitumia zaidi ya 8500. Japo kuna wengine waliitumia hii pesa kuongezea kwenye ada nawapa hongera kwa hilo.

1. Kama hauna ma kando kando 8500 ni pesa nyingi sana kwa siku kwa mtu mmoja. Tumia kidogo kadri uwezavyo, inayobaki itunze. Weka hata 2000 kwa siku kwenye kibubu chako, hii pesa utaitumia kama mtaji wa kuwekeza uwapo chuoni au baada ya chuo. Ajira hazieleweki.

2. Epuka kuiga uwapo chuoni. Sometime niliiga, nile kama fulani, nivae kama fulani ninywe kama fulani. Hii imenifanya nitumie pesa hovyo ndugu zangu. Nakushauri kuwa kama mjinga, kuwa kawaida tu, kuwa wewe, ni sumu kuiga.

3. Sikuwa mtu wa mademu, ila niliona wenzangu, mademu 3 mpaka 5 ni kawaida. Huyu kamtoa out kule, huyu kampeleka huku, huyu kamlisha kile n.k yote kudhihirisha yeye ni kidume. Hii ilikuwa sana pale boom linapotoka. Epuka hii, kuwa mwangalifu kwenye matumizi uwapo kwenye mahusiano. Pesa nyingi washikaji waliitumia hapa.

4. Hakuna mtu kwenye historia aliwahi kuikamata fashion. Kila siku kuna fashion mpya iwe mavazi, technologia n.k Nilipenda kuwa na smartphone kali, ikitoka iphone 6 nilitaka kuwa nayo, sijui nguo gani nilipenda kuwa nayo. Achana na hii mambo, kila kitu kina muda wake. Nilitumia pesa kwa ajili ya kujiweka wa kiwakati zaidi.

5. Jaribu kufikiria ni kitu gani unaweza fanya, ukawa comfortable kufanya ukiachana na profession unayoisomea, hii itakusaidia na itakupa urahisi wa kuwekeza pale unaposubiria ajira au zisipotoka kabisa. Hata mimi mpaka sasa nipo nachanganua nitafanya nini nimalizapo chuo maana waliopo huko bila ajira ni wengi, nawaza mimi itakuwaje.?

6. Kuwa mwepesi wa kuchagua marafiki, chagua wale wanaoendana na ndoto zako, watakaokusindikiza katika kuitafuta kesho yako.

Utakayo save uwapo chuoni mpaka unamaliza chuo inaweza isiwe kubwa sana lakini tukumbuke hata milioni ilianza na shilingi moja. Kidogo hicho hicho kinaweza kuwa msaada huko uendako. Hata biashara kubwa zilianza kwa kuwa ndogo hapo mwanzo.

Nimejaribu kushare experience yangu chuoni, I hope nitarejea kwenye mstari maana naelekea kumaliza na sikujipanga toka mwanzo.

Shukrani.
 
Wazungu walituletea msemo 'if you fail to plan,you plan to fail' mwenzenu nilishindwa kuplan, japo ninajipa tumaini kuwa it is never too late,nina tumaini nitarekebisha kwa namna moja au nyingine.

Mimi ni mwanachuo,na mambo yakienda vema basi mwakani nitakuwa nahitimisha,japo nina hofu na nitapambana vipi na hali ya huko niendako sababu ni kama nimechelewa kujipanga.

Mambo yamebadilika,upepo hausomeki huko baada ya chuo,ajira hamna kama zamani,pesa hazikamatiki.Ila nina amini kabisa una uwezo wa kujipanga kabsa kukabiliana na ugumu uliopo mbele kama tu utajipanga mapema.

Wanafunzi wengi wa chuo, 'BOOM HALIKAMATI BOOM' Hili ni kosa kubwa ambalo nimelifanya,boom la miezi miwili nilitumia kwa mda wa mwezi mmoja au mmoja na nusu. Serikali inatoa 8500 kwa siku,inamaanisha kuna siku nilitumia zaidi ya 8500. Japo kuna wengine waliitumia hii pesa kuongezea kwenye ada nawapa hongera kwa hilo.

1. Kama hauna ma kando kando 8500 ni pesa nyingi sana kwa siku kwa mtu mmoja.Tumia kidogo kadri uwezavyo,inayobaki itunze. Weka hata 2000 kwa siku kwenye kibubu chako,hii pesa utaitumia kama mtaji wa kuwekeza uwapo chuoni au baada ya chuo. Ajira hazieleweki.

2. Epuka kuiga uwapo chuoni. Sometime niliiga,nile kama fulani,nivae kama fulani ninywe kama fulani. Hii imenifanya nitumie pesa hovyo ndugu zangu. Nakushauri kuwa kama mjinga,kuwa kawaida tu,kuwa wewe,ni sumu kuiga.

3. Sikuwa mtu wa mademu,ila niliona wenzangu,mademu 3 mpaka 5 ni kawaida. Huyu kamtoa out kule,huyu kampeleka huku,huyu kamlisha kile n.k yote kudhihirisha yeye ni kidume. Hii ilikuwa sana pale boom linapotoka. Epuka hii,kuwa mwangalifu kwenye matumizi uwapo kwenye mahusiano. Pesa nyingi washikaji waliitumia hapa.

4. Hakuna mtu kwenye historia aliwahi kuikamata fashion. Kila siku kuna fashion mpya iwe mavazi,technologia n.k Nilipenda kuwa na smartphone kali,ikitoka iphone 6 nilitaka kuwa nayo,sijui nguo gan nilipenda kuwa nayo. Achana na hii mambo,kila kitu kina mda wake. Nilitumia pesa kwa ajili ya kujiweka wa kiwakati zaidi.

5. Jaribu kufikiria ni kitu gani unaweza fanya,ukawa comfortable kufanya ukiachana na profession unayoisomea,hii itakusaidia na itakupa urahisi wa kuwekeza pale unaposubiria ajira au zisipotoka kabisa. Hata mimi mpaka sasa nipo nachanganua nitafanya nini nimalizapo chuo maana waliopo huko bila ajira ni wengi, nawaza mimi itakuwaje.?

6. Kuwa mwepesi wa kuchagua marafiki,chagua wale wanaoendana na ndoto zako,watakaokusindikiza katika kuitafuta kesho yako.

Utakayo save uwapo chuoni mpaka unamaliza chuo inaweza isiwe kubwa sana lakini tukumbuke hata milioni ilianza na shilingi moja. Kidogo hicho hicho kinaweza kuwa msaada huko uendako. Hata biashara kubwa zilianza kwa kuwa ndogo hapo mwanzo.

Nimejaribu kushare experience yangu chuoni,i hope nitarejea kwenye mstari maana naelekea kumaliza na sikujipanga toka mwanzo.

Shukrani.
Safi sana huu ushauri
 
Vizur kwa kuwakumbusha wadogo zako... Vijana wawapo chuo wanatakiwa kuutumia uhuru wao vizuri,
maana utajikuta unamaamuzi ya kila jambo na hakuna wakukusimamia wala kukukataza, na hapo ndo vijana wanapoanza kupotea inabidi watambue kuwa kuna maisha baada chuo
 
Waambie mkuu maisha huku sivyo kama wazaniavyo usipokua makini utamaliza chuo na pc tu ambayo itabidi uiuze pindi ukimliza chuo ili upate hela ya kuzungukia maofisi mbalimbali kutafuta ajira
 
Asante san'a mkuu najipanga ili walau mwaka wa kwanza mwishoni niwe tayar nina kitu nmewekeza ata kidg kiasi gani
Jipange mdogo mdogo mwisho wa siku utajikuta una kitu cha kuanzia.
 
Vizur kwa kuwakumbusha wadogo zako... Vijana wawapo chuo wanatakiwa kuutumia uhuru wao vizuri,
maana utajikuta unamaamuzi ya kila jambo na hakuna wakukusimamia wala kukukataza, na hapo ndo vijana wanapoanza kupotea inabidi watambue kuwa kuna maisha baada chuo
Kweli kabisa.
 
Waambie mkuu maisha huku sivyo kama wazaniavyo usipokua makini utamaliza chuo na pc tu ambayo itabidi uiuze pindi ukimliza chuo ili upate hela ya kuzungukia maofisi mbalimbali kutafuta ajira
Ni kweli mkuu usipokuwa makini hata pc unaweza uza kabla ya kumaliza chuo
 
Back
Top Bottom