EWE BINTI TAMBUA THAMANI YAKO.

EWE BINTI TAMBUA THAMANI YAKO.

Deinstein 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
2,087
Reaction score
3,916
Habari wakuu!

Kama kichwa cha uzi kinavyojibainisha, kwenye jamii ya leo kumekuwa na mabinti au wanawake wengi wasiotambua thamani yao. Ndo maana leo hii huko mashuleni, vyuoni na makazini mabinti wengi wamejengewa sifa zisizo nzuri.

Mabinti wengi wanaruhusu miili yao kuchezewa na wanaume kwaajili ya tamaa zao. Unakuta binti anagawa kitumbua chake ili anunuliwe pombe au apewe hela, hajui ya kuwa kitu anachokitoa kina thamani kuliko hata hela au pombe anayopewa.

Inashangaza kuona binti anabananishwa kichochoroni na kuanza kuambiwa maneno matamu na mwanaume anayemuonaga tu mtaani na yeye bila kufikiria kwa kina anakubali kuingia na huyo mwanaume kitandani. Ama kweli mwanamke asiye na akili zitakazoumia ni sehemu zake za siri.

Ewe binti shida unazozipitia zisikufanye upoteze thamani yako. Unapopitia matatizo ni vyema ukawaeleza hata wazazi au marafiki zako ila usiwe tegemezi kwa mwanaume. Ukiwa tegemezi kwa wanaume mwili wako utatumiwa na shida zingine zitaibuka kama vile mimba zisizotarajiwa na mwishowe unakuwa single mother.

Pia hakikisha unaingia kwenye mahusiano na mwanaume anayejitambua na anaramani yake ya maisha. Sio unagawa kitumbua chako kwa mwanaume asiyejielewa. Lose your virginity to a worthy man sio unainamishwa vichochoroni na wavuta bangi.

Daima wanawake ni jeshi kubwa, nafasi yao lazima ionekane kwenye jamii. Ndo maana hata shuleni fasihi inazungumzia sana nafasi ya mwanamke kwenye jamii kuliko ya mwanaume. Mwanamke anayejua thamani yake hata jamii inamheshimu na anakuwa na misimamo yake na hapelekeshwi na mtu yeyote.

Kwa kuhitimisha, wazazi hasa wakina mama mnatakiwa mhakikishe mabinti zenu wanajua thamani yao. Hakikisha unamsaidia binti yako katika kila hali ili masela wasije wakamuwahi.

Yangu ni hayo tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom