EVIL'S TRAMPING GROUND CAROLINA USA

EVIL'S TRAMPING GROUND CAROLINA USA

FM facts

Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
45
Reaction score
88
Eneo Hili Linaitwa 'Devil's Tramping Ground' Lipo Katikati ya Msitu Huko Greensboro, Takribani KM 80 Kaskazini Mwa Mji wa Carolina Nchini Marekani.

Jina la Eneo hili Linajieleza Kwamba ni Eneo la Namna Gani, inaelezwa Tangu Miaka Mingi sana Nyuma Eneo hili la Mzunguko wa Futi 40 Hapajawahi Ota Mmea Wowote zaidi ya Hizo Nyasi Ndogondogo Pembeni, Kama Panavyoonekana Katika picha Basi Pako hivyo hivyo Miaka Yote!. .
.
Kwa Mujibu wa Historia inaelezwa Kwamba Miaka ya Nyuma, Msitu huu Ulikua Maarufu Kwa Imani za Kishirikina Kwani Mizimu Pamoja na Sauti za Ajabu Zilikua zinatokea Katika Msitu huu na Hapo Katikati Kuna Shimo Dogo ambalo Ndio Mizimu Ilikua Ikitokea na Kwamujibu wa Waliowahi Shuhudia Wanasema Ukipita Usiku Kuna Macho Mawili Mekundu Yanaonekana Ndani ya Shimo Huku Kukitokea pia Viumbe wa Ajabu.. .
.
Zaidi ya Miaka 100 sasa Hakuna Chochote Kilichowahi Kuota hapo, na Hakuna Kiumbe yeyote Alikua aneweza Kuliruka Shimo hili na Hata Mnyama Akifika Hapa Ilikua Either Atarudi Alikotoka au Atabadirisha Njia.

Kuna Wataalamu walijaribu Kutaka Kuuchukua Mchanga wa Eneo hilo ili Kuufanyia Utafiti Kujua ni kwanini Hauoteshi Chochote lakini Hakuna Aliyewahi Kujua ni nini Kiliwakuta.

Miaka Michache Nyumba kuna Mwandishi wa Habari Kutoka Katika Gazeti la Greensboro, Aliamua Kufunga Safai Hadi eneo hilo na Kukesha Usiku mzima akiwa na Mbwa wake Wawili na Baada ya Kurudi Alikiri Kusikia Sauti za Ajabu ajabu Kama vile Sauti za Hatua za Watu Wakitembea Huku Mbwa wake Wakibweka Usiku Mzima!

Inaelezwa Kwasasa Hakuna Maajabu hayo na Watu Huenda Kukesha Usiku Hapo hasa Watalii, na Wanakatiza tu kama Kawaida
IMG_20190324_202332_239.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom