Evarist Chahali: Mambo mazito sana yanasemwa kuhusu usalama wa nchi lakini tunayapuuzia kwa ushabiki wa kisiasa

mkuu kweli kabisa.nakumbuka huko nyuma miaka.mingi sana imeshapita. nilisoma hii mission kupitia gazeti la rai la wakati ule kwamba USA wanamwandaa raisi wa nchi moja ya jirani ili wazitawale nchi zote kwa maana ya kumiliki mali kwenye great lake region.kwa maelezo ya bwana chahali na yako nimeweza kuunganisha japo dot kidogo kwa mbaali naona uhalisia wa makala yale
CIA project for sure, sasa mmekubali kuwa na ssoko moja. Hapa Dawa ni Mchina na mrusi kuwapa deal
 
Mungu kwa maksud alimwachia Sizonje awe rais hili kutuadhibu kwa ujinga wetu.

Yani jamaa nchi imemshinda kabisa. Cha kuhuzunisha hata mkwere DHAIFU approval rating yake iko juu Sana Na zaid kuliko huyu jamaa.
huo ujinga ndio tuuainishe maana ndio utakuwa mwanzo wa ufumbuzi juu ya hili.
Hivi vita vya chini chini pia vinaanziaga mbali sana baina ya nchi na nchi na nna hisi kama ni kweli basi wapo hatua fulani kwa sasa and tunamuda wa kuamua na tukidhani hatujali ni shwari basi tutaona matokeo.
 
Hili lilikuwa kosa No.1 mwaka 2015, sasa tunafanyaje ili kilisahihisha?
wenye macho tuliliona hili wenzetu wanaoenda kwa mihemko wakabisha , thank GOD kwamba ametuonyesha mapema ili tuyarekebishe tuliyoyaharibu wenyewe. tuweresponsible na taifa letu maana tulikuwa tunapuuzia puuzia sana swala la umakini.
 
Hapo namba mbili ndio huyu aliyeteuliwa kuwa Katibu tawala wa Tabora leo.
Hadi sasa nashindwa kabisa kuelewa kichocheo na lengo la mabadiliko haya ya Raisi Magufuli. Anaanza kuona aibu au kuogopa mambo fulani yanaweza kumgeuka?
 
Labda kama unachukulia ukubwa wa nchi ni eneo
RWANDA NI KAMA MKOA TU NA HAINA UWEZO WA KUIDHIBITI NCH KUBWA KAMA TANZANIA. MSIWAPE KICHWA.. HATA KAMA WAKIMDHIBITI RAIS, HAIMAANISH WAMEIDHIBITI NCHI... KUWENI NA AMANI.


KWANI MICHAEL SATTA YUKO WAPI?[/QU

Labda kama unachukulia ukubwa wa nchi ni eneo la ardhi ya nchi husika, lakn wenzako tunaoamini ukubwa wa nchi ni kiwango cha maendeleo ya kiuchumi, nguvu za kijeshi, teknolojia na kiwango cha elimu ya watu wa nchi husika. Eneo la ardhi bila nguvu za kiuchumi, kielimu na kijeshi, ubora wa huduma za kijamii hiyo nichi bado sana
 
Hata kama mambo yaliyoorodheshwa katika ile thread ya mwanzo yanaweza yakawa sio sahihi kwa 100%, lakini sio ya kuyapuuzia. Ni mambo mazito sana yanayokabili taifa letu na yanapaswa kupewa uzito unaostahili. Mambo haya yaliandikwa kama ujumbe kwa mkuu wa kitengo fulani cha usalama nchini, lakini ni mambo ambayo yanapaswa kwenda zaidi ya hapo. Nitanukuu mambo mazito matano yaliyoainishwa, na mtu inaonyesha alikuwa mtumishi wa idara ya Usalama wa Taifa.
  1. Huenda ukaumia nafsi kufahamu kuwa kuna operesheni iliandaliwa mwaka 2013 kutuma watu huku Uingereza kumdhuru Chahali. Unaweza kunihurumia baada ya kutafakari "walitaka kumuuwa kwa kosa gani hasa?"
  2. Na mwaka jana mwezi wa tano hivi Bwana Mkubwa hakupendezwa na makala flani ya Chahali katika gazeti la Raia Mwema, akamtuma poti wake (namba mbili hapo) aandae operesheni dhidi ya Chahali. Huyo poti wa Bwana nae hatosema kuwa nilimtumia barua ya kumuonya kuwa nafahamu anachopanga.
  3. Usikae kimya huku Bashite, poti wa Bwana Mkubwa, akaigeuza Idara kuwa ofisi yake binafsi. Akaitumia kwa maslahi yake binafsi.
  4. Usikae kimya huku maafisa wa idara ya nchi jirani wanaichezea Idara yetu tukufu kwa vile tu Bwana Mkubwa ni anapelekeshwa na kiongozi wa nchi hiyo, jasusi mzoefu ambaye yeye na kitengo cha nchi hiyo wana "kompromat" (compromising information) kuhusu Bwana Mkubwa na wanaitumia kama leverage (kama picha la Putin na Trump)
  5. Usikae kimya wakati unafahamu kuhusu kinachoitwa "Kikosi Maalum" ambacho kinafanya kila baya dhidi ya watu ambao aidha Bwana Mkubwa hawapendi au mwanae Bashite anataka kuwakomoa. Hicho "Kikosi Maalum" ni sawa na Idara nje ya Idara. Neno la kitaalam ni rogue element, na kamwe usiruhusu kitu hicho.
Sasa haya mambo matano ni mazito na ya kutisha sana kama ni kweli yanatokea katika nchi yetu. Kumbuka kwamba hayo mambo matano yanasemwa na mtu ambaye inaonekana alikuwa sehemu ya chombo cha usalama wa taifa. Si rahisi yawe ya kujitungia, au kutafuta kiki kama wengi wanavyosema. Yamesemwa na mtu ambaye inaonekana sio tu ana ufahamu wa ndani, bali pia ana hasira, na yuko desparate kwa kuwa maisha yake yako hatarini, hivyo kaamua kusema wazi aidha kama retaliatory measure au kama namna fulani ya kujihifadhi.

Sasa nini implications za haya yaliyosemwa? Kwa maoni yangu haya yaliyosemwa yanamaanisha kwamba;
  1. Tanzania kimeundwa "Kikosi Maalum" kwa ajili ya watu ambao wanamkorofishahuyo aliyeitwa "Bwana Mkuu". Hii sasa huenda ikatoa majibu kwa watu ambao wamekuwa wakitekwa na kupotea pamoja na kuuwawa. Huenda ikatoa jibu kuwa wale watu "Wasijulikana" ni kina nani, na kwamba ni kikosi maalum, "rogue element" kinachofanya kwa maagizo ya "Bwana Mkubwa" ili ku "eliminate" watu wanaoonekana kuwa ni tatizo katika nchi hii. Huenda ikatoa jibu juu ya kauli zilizowahi kutolewa kwamba huwezi ukawa tatizo nchini tukakuacha tu uendelee kuwapo! Huenda ikatoa jibu jibu nani alihusika na jaribio la mauaji ya Lissu, nk!
  2. Tanzania huwa inatuma vikosi vya maujaji kwenda nje kuwashughulikia watu ambao wanaonekana ni tatizo kwa uongozi uliopo madarakani
  3. Idara ya Usalama wa Taifa imekuwa compromised, na haifanyi tena kazi kama taasisi ya taifa kwa manufaa ya taifa bali imebinafsishwa na baadhi ya watu nchini na kutumika kwa manufaa binafsi ya hao watu wachache
  4. Kwamba uongozi wetu wa juu nchini, huyo "Bwana Mkubwa" aliyetajwa, umekuwa compromised na nchi jirani na sasa unafanya kazi katika mazingira ya kuwa "blackmailed". Inamaanisha uongozi wetu hauna sauti tena na uhuru wa kufanya dhidi ya jambo lolote linalofanywa na nchi jirani au litakaloathiri hiyo nchi jirani. Athari ya hili ni kubwa sana, inaweza hata kutia ndani usalama wa majeshi yetu (JWTZ) huko DRC. Huenda inatoa jibu kwa nini hadi sasa hii nchi jirani inatuhumiwa kuua zaidi ya raia 50 kule Kagera na serikali yetu imekaa kimya juu ya hili bila kufanya kitu au hata kutoa tamko. Ni juzi tu hapa Kigwangwala ndio alitoa tamko la hasira juu ya jambo hili.
Ndugu zangu Watanzania, bila kujali ni nani ameandika haya mambo, au historia yake ni nini, kuna mambo mazito sana hapa ambayo kila Mtanzania mwenye akili anapaswa kuogopa na kutafakari sana. Inaonekana nchi iko hatarini sana kuisalama kuliko ilivyowahi kutokea tangu tupate uhuru.

Rai yangu ni kwa wabunge, wakuu wa majeshi, na kila aina ya mtazania anayeweza kufanya kitu kuhusu jambo hili kutolipuuzia kwa kudhani kwamba yeye hahusiki. Ni lazima jambo hili lipewe uchunguzi unaostahili. Najua kwamba kama hizi tuhuma ni kweli, basi kushughulikia jambo hili inahitaji ujasiri na moyo mkuu, hasa kama kuna "Kikosi Maalum".

Desparate measures zinahitajika hapa kwa kuwa nchi yetu iko kwenye desparate times.

Mimi kama Mzalendo wa Tanzania nafurahi kuwa majukumu ya Usalama wa taifa yapo wazi...pia sheria inakilinda chombo hicho kwani raiti sheria ingekipa mbwembwe za kuonekana kama taasisi zingine basi hizo media zingekuwa hazitoshi...that is why kokote duniani sijawahi kusikia msemaji wa usalama wa taifa na ndio maana wanaonewa sana hawa watu yaani mambo mabaya yote huwa wanayabeba..
Utasikia mtu mmoja anajiita Usalama wa taifa mstaafu anachafua taasisi yake...!!ni uongo hakuna mtumishi kokote duniani wa taasisi nyeti kama hii akitokea kuachishwa au kustaafu kazi hiyo huwa anakuwa against na chombo hicho kama yupo basi huyo amekengeuka...

Mifano halisi tunayo hapahapa nyumbani kuna watumishi waliowahikuwa watumishi wa chombo hicho lakini sijawahi kuona wakiwa against na chombo hicho...
mfatilie mrema
mfatilie apson
mfatilie Ditopile na wengine wengi...,
So to me ninacho kiona kwa Chaali ni kutafuta umaarufu tena umaarufu wa kijinga...

Poleni watumishi wote wa taasisi ya usalama wa taifa najua mnapata tabu sana especial hamuwezi kutoka kwenye media na kuanza kujitetea,timizeni wajibu wenu kwa maslahi mapana ya taifa kwa kuishauri serikali na taasisi zake vema...

I rest my Case...!!
Mzalendo Tz
 
Mkuu sijasema wanatangaza, bali kila mission ya ku-eliminate mtu nje ya nchi inakuwa signed na president ili kuweka record kwamba hilo lilifanyika officially.

In fact inasemekana kuwa haifikiriwi kabisa kwamba kikosi cha mauaji cha Urusi kinaweza ku-hit mtu bila signature ya president. Ndio maana hata hii kesi ya huyu spy ambaye amepewa sumu pamoja na binti yake, wanasema ni lazima Putin amesign, la sivyo Urusi hawawezi kabisa kufanya kitu kama hicho bila Putin kusign go ahead.

Sasa suala la diplomasia, hata sasa kwa kesi hii ya tukio la Uingereza ndilo swali linaulizwa. Hata ikijulikana ndio Putin alisign, wataifanya nini Urusi? Vikwazo zaidi? Wanasema labda watamuondoa balozi "as a protest gesture". Na wanakiri kuwa Russia ina impunity na wako so arrogant kwenye hivi vitu unavyoona vitaharibu diplomasia, lakini so far nani kamchukulia hatua? Russia kwa makusudi wametungua ndege za abiria mara mbili, ya South Korea na ya Malaysia, na kuua mamia ya watu, wamefanywa nini? Russia wamechukua sehemu ya Ukraine, wamefanywa nini? Russia wamepiga mabomu raia huko Syria wakishirikiana na Assad, na kuua mamia ya raia kutia ndani watoto, wamefanywa nini? So hata mkijua Putin alisign kumuua huyu spay UK, na ana hiyo sheria, watamfanya nini?
Russia waliwapa Ukraine sehemu yao ya Crimea mwaka 1954 , by then ilikuwa ni United Socialist Soviet Of Russia( USSR). Russia hawajapokonya eneo la Ukraine tusipotoshe umma bali Russia wamerudisha sehemu yao ambayo Nikita Krushev (Ukranian by birth) aliwapa mwaka huo_On April 26, 1954 The decree of the Presidium of the USSR Supreme Soviet transferring the Crimea Oblast from the Russian SFSR to the Ukrainian SSR.
Lakini pia cha kujifunza ni kwamba Russia wala Assad hawajawahi kuwauwa raia kule Syria bali ni propaganda za West.
 
Russia waliwapa Ukraine sehemu yao ya Crimea mwaka 1954 , by then ilikuwa ni United Socialist Soviet Of Russia( USSR). Russia hawajapokonya eneo la Ukraine tusipotoshe umma bali Russia wamerudisha sehemu yao ambayo Nikita Krushev (Ukranian by birth) aliwapa mwaka huo_On April 26, 1954 The decree of the Presidium of the USSR Supreme Soviet transferring the Crimea Oblast from the Russian SFSR to the Ukrainian SSR.
Lakini pia cha kujifunza ni kwamba Russia wala Assad hawajawahi kuwauwa raia kule Syria bali ni propaganda za West.
the Union of Soviet Socialist Republics (USSR)
 
Umesema kiongozi wetu wa 2018 alikuwa compromised? Kwa hiyo sasa tuko salama? Always I wondered kwa nini Ben Saanane aliuawa,kwa sababu mambo alivyokuwa anaongea Ben yalikuwa boring, irrelevant na inconsequential.
Corruption ipo Usalama wa Taifa, Polisi,mtu yeyote anaweza kuona. Jeshini kule hatujui habari zao. Yule CDF aliyeapishwa juzi,I wish angeongea zaidi. Nilikuwa nasikiliza kile kiapo and I wondered,did he sound like an alcoholic.?
TISS yetu ni Mossad trained. Mossad wanajulikana ni very difficult people. Lakini sera ya Usalama wa Taifa siyo rocket science. Mambo wanayotakiwa kufanya siyo mystery.
 
Wakati mkuu unajaribu kuonya na kuhitaji mjadala wenye mawazo huru kwa suala nyeti kama hili cha ajabu huu uzi ukifikisha wachangiaji zaidi ya 15 utaona vituko na logic za ajabu za uchama na wanachama wa vile vyama pinzania wakianza balaa lao humu..

Pamoja na yoote hoja ni muhimu sana kuzingatiwa na Watanzania tuijadili na kuifikiria kwa mapana sana ili tusije kuwa na mwisho mbaya, kelele za wafia vyama kama sio wafia chama ni hatari sana kwa sasa kwa usalama wa nchi hii maana hata wale maadui kwa sasa wanapitia njia hiyo hiyo kutuzuga na ndio maana mpaka leo utasikia watanzania kuna wanaojiita Wazalendo na wapenda maendeleo na kuwaona wenzao sio wazalendo lakini ukizama kiundani juu ya hii dhana utagundua ni propaganda iliyopandwa kwenye akili za wasiojitambua ili mwisho wa siku adui afanikiwe.. immediate measures and actions needed in this scenario for majority interest. ZZK aligusia suala la kuvunjwa kwa TISS na iundwe upya kwa namna nyingine, binafsi naona moja ya muundo wake uwe mbali kabisa na siasa na wanasiasa maana tayari CCM walishafanya makosa kwa kuiacha hii taasisi iwe kama chombo cha kisiasa kwa manufaa ya CCM lakini kumbe ndio tulikuwa tunajitengenezea kabuli letu wenyewe..

Ni wakati sasa wa Serikali au CCM kujifunza na kuziweka mbali taasisi za usalama na ulinzi na siasa na kuwafanya wananchi wawe huru kuamua na taasisi za usalama zibaki kuangalia na kulinda amani na kudeal sana na maslahi ya Taifa na sio chama.. Vyombo vya usalama vyenyewe vibaki kutii mamlaka itakayochaguliwa na wananchi kwa maana ya kuilinda lakini vyenyewe vikiwa na mifumo au policy zake nyeti zenye maslahi kwa Taifa na sio interest za chama kilichopo madaraka.. Ni wakati sasa wa vyombo vya usalama kuwa na nguvu au uwezo wa kumtoa madarakani yeyote yule ambaye anaharibu au anaangamiza maslahi ya nchi bila kuangalia chama kwa maana ya mlengo ila cha muhimu iwe maslahi ya Taifa na sio unafiki, maana nina uhakika hivi vyombo kwa 100% vinajua maslahi ya taifa na nani msaliti na sio kufanya kazi kwa amri za wanasiasa..
Ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom