Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Hata kama mambo yaliyoorodheshwa katika ile thread ya mwanzo yanaweza yakawa sio sahihi kwa 100%, lakini sio ya kuyapuuzia. Ni mambo mazito sana yanayokabili taifa letu na yanapaswa kupewa uzito unaostahili. Mambo haya yaliandikwa kama ujumbe kwa mkuu wa kitengo fulani cha usalama nchini, lakini ni mambo ambayo yanapaswa kwenda zaidi ya hapo. Nitanukuu mambo mazito matano yaliyoainishwa, na mtu inaonyesha alikuwa mtumishi wa idara ya Usalama wa Taifa.
Sasa nini implications za haya yaliyosemwa? Kwa maoni yangu haya yaliyosemwa yanamaanisha kwamba;
Rai yangu ni kwa wabunge, wakuu wa majeshi, na kila aina ya mtazania anayeweza kufanya kitu kuhusu jambo hili kutolipuuzia kwa kudhani kwamba yeye hahusiki. Ni lazima jambo hili lipewe uchunguzi unaostahili. Najua kwamba kama hizi tuhuma ni kweli, basi kushughulikia jambo hili inahitaji ujasiri na moyo mkuu, hasa kama kuna "Kikosi Maalum".
Desparate measures zinahitajika hapa kwa kuwa nchi yetu iko kwenye desparate times.
- Huenda ukaumia nafsi kufahamu kuwa kuna operesheni iliandaliwa mwaka 2013 kutuma watu huku Uingereza kumdhuru Chahali. Unaweza kunihurumia baada ya kutafakari "walitaka kumuuwa kwa kosa gani hasa?"
- Na mwaka jana mwezi wa tano hivi Bwana Mkubwa hakupendezwa na makala flani ya Chahali katika gazeti la Raia Mwema, akamtuma poti wake (namba mbili hapo) aandae operesheni dhidi ya Chahali. Huyo poti wa Bwana nae hatosema kuwa nilimtumia barua ya kumuonya kuwa nafahamu anachopanga.
- Usikae kimya huku Bashite, poti wa Bwana Mkubwa, akaigeuza Idara kuwa ofisi yake binafsi. Akaitumia kwa maslahi yake binafsi.
- Usikae kimya huku maafisa wa idara ya nchi jirani wanaichezea Idara yetu tukufu kwa vile tu Bwana Mkubwa ni anapelekeshwa na kiongozi wa nchi hiyo, jasusi mzoefu ambaye yeye na kitengo cha nchi hiyo wana "kompromat" (compromising information) kuhusu Bwana Mkubwa na wanaitumia kama leverage (kama picha la Putin na Trump)
- Usikae kimya wakati unafahamu kuhusu kinachoitwa "Kikosi Maalum" ambacho kinafanya kila baya dhidi ya watu ambao aidha Bwana Mkubwa hawapendi au mwanae Bashite anataka kuwakomoa. Hicho "Kikosi Maalum" ni sawa na Idara nje ya Idara. Neno la kitaalam ni rogue element, na kamwe usiruhusu kitu hicho.
Sasa nini implications za haya yaliyosemwa? Kwa maoni yangu haya yaliyosemwa yanamaanisha kwamba;
- Tanzania kimeundwa "Kikosi Maalum" kwa ajili ya watu ambao wanamkorofishahuyo aliyeitwa "Bwana Mkuu". Hii sasa huenda ikatoa majibu kwa watu ambao wamekuwa wakitekwa na kupotea pamoja na kuuwawa. Huenda ikatoa jibu kuwa wale watu "Wasijulikana" ni kina nani, na kwamba ni kikosi maalum, "rogue element" kinachofanya kwa maagizo ya "Bwana Mkubwa" ili ku "eliminate" watu wanaoonekana kuwa ni tatizo katika nchi hii. Huenda ikatoa jibu juu ya kauli zilizowahi kutolewa kwamba huwezi ukawa tatizo nchini tukakuacha tu uendelee kuwapo! Huenda ikatoa jibu jibu nani alihusika na jaribio la mauaji ya Lissu, nk!
- Tanzania huwa inatuma vikosi vya maujaji kwenda nje kuwashughulikia watu ambao wanaonekana ni tatizo kwa uongozi uliopo madarakani
- Idara ya Usalama wa Taifa imekuwa compromised, na haifanyi tena kazi kama taasisi ya taifa kwa manufaa ya taifa bali imebinafsishwa na baadhi ya watu nchini na kutumika kwa manufaa binafsi ya hao watu wachache
- Kwamba uongozi wetu wa juu nchini, huyo "Bwana Mkubwa" aliyetajwa, umekuwa compromised na nchi jirani na sasa unafanya kazi katika mazingira ya kuwa "blackmailed". Inamaanisha uongozi wetu hauna sauti tena na uhuru wa kufanya dhidi ya jambo lolote linalofanywa na nchi jirani au litakaloathiri hiyo nchi jirani. Athari ya hili ni kubwa sana, inaweza hata kutia ndani usalama wa majeshi yetu (JWTZ) huko DRC. Huenda inatoa jibu kwa nini hadi sasa hii nchi jirani inatuhumiwa kuua zaidi ya raia 50 kule Kagera na serikali yetu imekaa kimya juu ya hili bila kufanya kitu au hata kutoa tamko. Ni juzi tu hapa Kigwangwala ndio alitoa tamko la hasira juu ya jambo hili.
Rai yangu ni kwa wabunge, wakuu wa majeshi, na kila aina ya mtazania anayeweza kufanya kitu kuhusu jambo hili kutolipuuzia kwa kudhani kwamba yeye hahusiki. Ni lazima jambo hili lipewe uchunguzi unaostahili. Najua kwamba kama hizi tuhuma ni kweli, basi kushughulikia jambo hili inahitaji ujasiri na moyo mkuu, hasa kama kuna "Kikosi Maalum".
Desparate measures zinahitajika hapa kwa kuwa nchi yetu iko kwenye desparate times.