Evarist Chahali: Mambo mazito sana yanasemwa kuhusu usalama wa nchi lakini tunayapuuzia kwa ushabiki wa kisiasa

Jamani hata mimi nilikuwa nampenda sana huyu Raisi lakini kwa sasa sina hamu naye. Kwa hali ya kawaida kabisa jamani saa nyingine unampenda hata mumeo au mkeo mkiwa mnachumbiana lakini mkisha juana tabia mapenzi hayawagi sawa, kwa wengi huwa yanapungua. Wazungu wanasema let look at the big picture, people evolve. Ndiyo maana kuna kuokoka pia katika dini zetu, mtu unaweza kuona kwamba umekosea na kuamua kumrudia Mungu.
Duh
 
Kwa huyu Chahali, watu wa usalama sasa wawe makini zaidi katika kurecruit watu wao. Kwa Chahali ni failure over and over! Jamaa alifaa kabisa kwenye Mchiriku na sio Usalama wa Taifa!
ww wa wwapi ww...yaani mtu asiongee kuiponya nchi yake...punguza ujinga
 
RWANDA NI KAMA MKOA TU NA HAINA UWEZO WA KUIDHIBITI NCH KUBWA KAMA TANZANIA. MSIWAPE KICHWA.. HATA KAMA WAKIMDHIBITI RAIS, HAIMAANISH WAMEIDHIBITI NCHI... KUWENI NA AMANI.


KWANI MICHAEL SATTA YUKO WAPI?
kwa hiyo wakimdhibiti Rais maamuzi yenye kuhusu nchi utayafanya ww?,kama maamuzi watayafanya wao bado watakuwa hawajawadhibiti...tumia akili ndugu
 
Mkuu hapa tusifanye personal attacks kwa jamaa!! Hata kama maslahi yake yalibanwa, hoja ya msingi hapa ni usalama wa nchi yetu na kitengo cha usalama wa taifa!!

Swali la kujiuliza je Alichosema ni kweli? (hasa ukizingatia ukweli kwamba alishawahi kuwa mwana usalama)
We mwenyewe umekuwa personal zaidi ya anacho eleza unae mjibu.

Soma uelewe anacho wakilisha mwenzio.
 
Mkuu kama kweli unaelewa kunaweza kutumika kikosi kazi cha nchi jirani? Je kuna ukaribu gani na nchi jirani mpaka wakupe rasilimali watu adimu na zenye gharama namna hiyo? Kwa nini wao? Wana nini mpaka wako radhi kuweka rehani roho za walioapa kulinda taifa lao kwa ajili ya mgeni? Wao wana maslahi gani
Rejea hatakati za ukombozi za mwalimu nyerere
 
Pamoja na mengi aliyoandika, mimi nina maswali kadhaa kwa Chahali:

Mbona mwanzoni alimsifia sana Rais, hadi kuipongeza hotuba yake ya kwanza kwa Bunge kuwa ya mfano?

Kumetokea nini hapo katikati mpaka kumezuka tofauti kubwa sana kati yake na Rais?

Wakati akimsifia, alikuwa amelenga kupata nini ambacho aidha amekikosa au anaelekea kukikosa?

Ametoa clues kadhaa ambazo ni hatari kwa usalama wa taifa. Kwa kuwa yeye amejitambulisha kama aliyewahi kutumika kama Afisa Usalama wa taifa, je hizo clues alikuwa anazifahamu before au la? Kama jibu ni ndiyo, kwa nini shutuma ziletwe sasa? Kama jibu ni hapana, kwa nini alimsifia kabla ya kujiridhisha kama taaluma yake inavyomtaka?

Kwa nini asitoe hizo compromising information ambazo anadai 'The slim brother' anazo kuhusu 'Mkuu' wetu?

Lakini pia angedokeza kidogo (mengine yanaweza kuwa magumu kueleza hapa kutokana na kiapo), aliacha kazi kwa sababu gani na kwa nini hakubaki nchini?

Pengine majibu ya haya maswali yanaweza kutupanua mawazo tukachangia mada hii tukiwa na uelewa mpana.
We jamaa kweli hisabati
 
Rejea hatakati za ukombozi za mwalimu nyerere
Kwanza hujabu hayo maswali unaniambia nirehee, yajibu kwanza. Pili ni miaka karibia 60 sasa tangu tumepata uhuru.
Kipindi hiko kwa uchache wa rasilimali Afrika tulihitaji kuwa pamoja kusaidia kumuondoa Mkoloni. Hauwezi kutumia hali hiyo miaka hiyo ufananishe na leo, tena mazingira tofauti. Haya sasa niambie kwenye ulinzi na Usalama sisi tumepungukuwa nini?
 
Siku hzi Watanzania hata haki yakupita pale ikulu hatuna. Nilipita siku usawa wa bahari kule nikakuta jamaa wanalishwa push up wakiwa ma mademu zao kisa walipita jirani na ikulu.

Sasa hapo tutaacha kusema Nchi iko mikononi mwa Jasusi wa jirani
 
Back
Top Bottom