SoC02 Euthanated Education

Stories of Change - 2022 Competition

Tonny Godbless

New Member
Jul 28, 2022
1
2
ELIMU YA KITANZANIA NI TIKETI YA KWENDA DUNIA MPYA

Tanzania ni kati ya nchi hapa Africa ambazo zinapigana kukuza elimu yake ila bado ina changamoto nyingi. Wengi husema “Elimu ndio ufunguo wa maisha “ ila Watanzania wengi hupotea kwa sababu ya mfumo mbovu wa elimu ulioekwa na serikali ya Tanzania. Kila mwaka kati ya wanafunzi 3000 hadi 5000 wanaenda kusoma tahususi mbalimbali ughaibuni, wapo wanaoacha shule kwasababu ya mfumo wa elimu wa Tanzania katika ile ile asilimia 13 ya wanafunzi wanaoacha shule kila baada ya miaka miwili. Ikumbukwe mfumo mzima wa elimu ya kitanzania ni wa kipiramidi (pyramidal in shape) kwamba wanaanza wanafunzi wengi na ndo lengo la serikali lakini wanaofika katika nyanja za elimu ya juu yaani vyuo wanakuwa ni robo ya idadi ya walioanza darasa la kwanza kwanini inakuwa hivi :-

ADHABU ZA FIMBO (canes abuse). Tanzania ni nchi ambayo inatumia njia ya adhabu za fimbo kuhakikisha wanafunzi wanakua wasikivu na waelewa wenye maadili . Wakati huo huo ikumbukwe nchi kama Canada, South Africa, United Kingdom na Europe zinakataa vikali fimbo kutumika kama njia ya kumfanya mwanafunzi asome. Tanzania huamini kua njia hii hufanya wanafunzi kuwa wasikivu ila nyuma ya pazia ni fimbo zinaweza zikawa na madhara mengi sana kwa wanafunzi ikiwemo matatizo ya kihisia (emotional damage), Hofu na Uoga, matatizo kimwili, kiakili na kiafya na mashaka haya hufanya wanafunzi kua na nidhamu ya uoga na kutokujiamini. Pia njia hii huchangia utoro wa wanafunzi kwa kua fimbo hueka mbali ukaribu kati ya wanafunzi na waalimu.

Prohibition-of-corporal-punishment-in-20-rich-capitalist-nations_Q320.jpg

Juu ni baadhi ya nchi ambazo zimekataza adhabu na fimbo mashuleni.

UWIANO USIO SAWA KATI YA WANAFUNZI NA WAALIMU.

Tanzania ina changamoto kubwa yakua na wanafunzi wengi kuliko walimu, hususani shule zetu za serikali ambazo huchukua wanafunzi wengi ilihali (despite the fact ) mazingira ni mabovu . Wanafunzi wengi katika shule nyingi za serikali hupitia changamoto nyingi kama ukosefu wa msaada ( support ) wa kutosha kutoka kwa walimu wao kwakua walimu hao huzidiwa na wanafunzi , mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi 200 hadi 300 katika darasa moja . Hali hii husababisha wanafunzi kupoteza dira ya elimu , wanafunzi huishia kuona elimu ni mzigo na mateso na mwishowe kujenga chuki (towards) kujifunza
Screenshot_20220802-221812_Chrome.jpg
.

UFUATILIAJI USIO YAKINIFU KATIKA MASHULE HUSUSANI SHULE ZA SERIKALI. Ukiacha hii miaka ya karibuni, tunajua kwa mtaala wa elimu ya kitanzania hususani shule zetu za serikali mwanafunzi anatakiwa kuisaka asilimia 75 peke ake kwa kufanya vitu mbali mbali kama kujisomea, kutafuta vitabu, kushiriki mijadala mbali mbali na wanafunzi wenzake, na asilimia 25 itatolewa na mwalimu kwa kufundisha ubaoni, kutoa kazi, kufanya mifano na masahilisho lakini katika shule zetu mwalimu anaeza asiingie darasani kwa kipindi cha mda mrefu lakini bado mwisho wa mwezi mshahara unaingia na maisha yanasonga, inapelekea wanafunzi kupoteza dira nzima ya elimu na shule na kuona hakuna maana ya kusoma.

MTAALA ULIOSHEHENI MADA NYINGI ILIHALI UBOBEZI UNAKUJA KUWA WA MADA CHACHE.

Katika nchi za wenzetu mwanafunzi anasoma kitu anachokuja kubobea ( apply/specialize ) ilikusudi awe mzuri zaidi kwenye hicho anachosoma mf : USA, UK, CHINA, AUSTRIA ……N.K, Lakini Tanzania, Msingi utasoma vitu vingine, Sekondari utasoma vitu vingi, Pia elimu ya kidato cha tano na cha sita utasoma tena vitu vingi ambavyo hukusoma madarasa ya nyuma, na kadri unavopanda darasa masomo ndo yanapungua au yanaongezeka mpaka mwanafunzi anafika chuo anakuja kusoma udaktari kwa mfano hakuna mahali atazungumzia vita ya kwanza ya dunia aliyosoma katika somo la historia. Wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kuelewa vitu wanaona elimu ni mzigo wanaamua kuachana nayo na kujishughulisha na mambo mengine. Na hata hao wenye uwezo na uvumilivu wengi wa kukariri ambayo pia ina madhara maana mwanafunzi anakuwa aelewi anachofundishwa yeye anameza tu, kwaiyo ni ngumu mwanafunzi huyu kuishi alichofundishwa au alichojifunza

UPIMAJI WA KITAIFA. Sijui mitazamo ya watu na wanafunzi wengine ila upimaji wa kitaifa wa nchi ya Tanzania umekaa ki bahati nasibu, na sio kupima wanafunzi wameelewa nini mf : Mimi mwanafunzi wa PGM nina s.chand mbili za kusoma katika somo la fizikia ambazo kwa ujumla zina kurasa zisizopungua 2500, Natakiwa nizisome na kuzielewa ndani ya miezi 17 mwezi wa 18 nifanyie mtihani wa upimaji wa kitaifa ulio na maswali 16 natakiwa kujibu 14 lakini hapo hapo sijui ni mada ipi itatoka na kipimo cha miezi kumi na saba ya kusoma kinapimwa ndani ya masaa matatu. Unakuta mwanafunzi anafeli sio kwamba akusoma ni kwamba alichosoma yeye akijatoka katika mtihani ila ndo mtihani wa upimaji ushamuhukumu kwamba mwanafunzi huyu ni dhaifu au hajui.

SWALI NI NINI KIFANYIKE SASA ……. Kwanza tuanze kwa kuondoa fimbo na viboko mashuleni, tujaribu njia zingine kama shughuli za maendeleo ya kijamii ( community development actions ) kama katika mashule binafsi. Wanafunzi ni wengi wanaoanza elimu ya msingi ila vyuo wanafika wachache tuchukue hatua yakinifu ikiwemo kuajiri walimu wengi zaidi ili kueka uwiano sawa baina ya wanafunzi na waalimu, ili mwanafunzi aelewe zaidi uwiano unashauriwa uwe 1 : 40 kati ya mwalimu na wanafunzi, hii pia inatoa nafasi ya mwalimu kumfikia na kufanya mapitio ya kazi ya kila mwanafunzi katika darasa husika. Waalimu vivuli wachukuliwe hatua staiki, kama ilivyo kwa ustawi wa jamii na watu wanaonyimwa haki zao, na kwa wanafunzi iwe ivyo kuwa na uwanja wa kuripoti kwa urahisi iwapo swala kama ili litakuwa linatokea. Pendekezo sisemi mfumo ubadilishwe ila walifikirie swali “kwanini msingi wafaulu wengi kadri tunavyopanda juu wanafunzi wanaofeli wanaongezeka”. Upimaji wa kitaifa kwa ngazi zote za elimu ungekuwa kama wa chuo ingependeza kama anaekufundisha ndo angepewa idhini ya kukupima basi ufaulu ungekuwa mkubwa zaidi katika nchi.

HITIMISHO. Elimu ya Tanzania itaendelea kutengeneza wasaka ajira na kazi ( job seekers ), na sio wasomi wenye nia ya kujiajiri ( job makers ) kama isipo punguza elimu ya vitabu ( theories ) na kujikita katika elimu na vitendo ( practical )
 
Back
Top Bottom