Eureka: Kumbe Push up za Magufuli ilikuwa danganya toto!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,710
9,063
Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mbwembwe za Rais wetu wakti wa kampeni alivyokuwa akipiga push up mwaka 2015 kwenye majukwaa!!
Push up za JPM ilikuwa kuwashawishi Watz kuwa kazi ya Urais ilikuwa ni rahisi na ataiweza pasipo shaka yoyote!
Lakini cha kushangaza leo mwaka 1 na miezi kadhaa JPM anaonekana kuelemewa na kazi za Ikulu! Rais ameanza kuonyesha dalili za kuchoka na kukata tamaa mapema kuliko Watz walivotazamia!
Angalia matukio yanayofuatana mfululizo ambayo yako kinyume kabisa na Katiba na Sheria za nchi hii!
Kwa kifupi tunaweza sema kuwa kumbe zile push zilikuwa za kuja kupambana na Wapinzani kwa kuwasweka ndani na kuua upinzani! Alipomtumbua Mama Malecela, Waziri Kitwanga, Watumishi hewa na Walioghushi vyeti. Lakini leo kashindwa na kijamaa kidogo kilichozungusha ZERO form 4 na kukiona kama mungumtu wa Darisalama! Hakiguswi,hakikemewi wala kutumbuliwa! Kila anachofanya Bashite kiwe kibaya au kizuri anasifiwa kwa kuambiwa APIGE KAZI! Akivamia Studio za Media Achape Kazi, akisingizia Watu kuwa wana Dawa za kulevya lakini Polisi wakichunguza na kukuta ni uongo, Chapa Kazi maana Hapa ni Kazi Tu!
Media wakiandika na kutangaza kuhusu Migogoro ya Wakulima na Wafugaji ni Uchochezi, wakitangaza kuna Ukame na Njaa ni Uchochezi, wakihoji hela za Tetemeko la Ardhi Kagera kwanini hazikusaidia wahanga, ni Uchochezi! Ukweli ni kwamba Magufuli Ikulu imemchosha bado mapema asubuhi! Tumwombee ili Mungu amtie nguvu.
 
Na ubaya kina anapohutubia huwa mtu wa Hasira na kinyongo. Mwalimu Nyerere hakuwa hivyo...Hakika: Tumwombee ili Mungu amtie nguvu.
 
IMG_20170325_094111.jpg
 
Unajua ukifuatilia historia ya dola zilizowahi kuanguka, sababu zake huwa ni za kipuuzi sana kiasi hata huwezi kutarajia. Halafu Mungu alivyo mwema hutanguliza dalili kwanza. Lakini kwa kuwa watawala wanakuwa washakunywa divai ya madaraka, huwa wabapuuzia dalili hizo na hatimaye inabaki historia tu. Hivi kweli Makonda au Bashite kama anavyoitwa ana credentials gani za kuitikisa nchi na kumfanya Rais adharaulike kwa kiwango hiki? Kweli? huyu bashite huyu wa kolomije amekuwa chanzo cha kila mmoja kujua rangi halisi ya rais.

Hakuna jambo lolote atakalisema leo rais likaonekana credible. Leo kuna watu ukisoma post zao kwenye mitandao ya kihamii, haki ya nani utaduwaa kwanza kwa mshangao. Utadhani akaunti zimekuwa hacked. Lakini yote hiyo ni dalili za nyumba inayoporomoka.
 
Mtoa mada kwa hiyo unatakaje sasa
Magufuli ampe funguo za Magogoni Lowasa kesho?
Mbona mnakua mazuzu kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom