EU yatoa mamilioni kusaidia mradi wa Eco - Fish ziwa Victoria

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,194
30 June 2021
Dar es Salaam,

EU YATOA MAMILIONI KUSAIDIA MRADI WA ECO - FISH ZIWA VICTORIA



Mkurugenzi Wizara Ya Mifugo na Uvuvi Bwana Emmanuel M. Bulai akizungumzia kuhusu Mkutano wa Usimamizi wa raslimali za Uvuvi Ndani ya Ziwa Victoria unaosimamiwa na nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinazonguka Ziwa Victoria (Lake Victoria Fisheries organization) gonga : East African Community | Lake Victoria Fisheries Organization, Mkutano uliohudhuriwa na wadau wa Sekta ya Uvuvi Na kutoa maoni mbalimbali.

Mkutano umefanyika Golden Tulip Hotel Jijini Dar Es Salaam Umoja wa Ulaya (EU) Umetoa takribani Euro Milioni Mbili kwa ajili ya kusaidia Mradi wa Kusimamia Raslimali za Uvuvi ECO-FISH katika Ziwa Victoria kwa lengo la kuwezesha nchi wanachama kukuza vipato vya wavuvi na Uchumi wa Nchi kupitia Raslimali za Uvuvi .

Akizungumza katika kikao kilichohusisha wadau wa Uvuvi, Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Emmanuel Bulai amesema Fedha hizo zitasaidia kupata takwimu sahihi za Uvuvi katika Ziwa Victoria na Kuimarisha Uhifadhi wa Mazalia ya Samaki. Takwimu kwa upande wa ziwa Victoria eneo la ndani ya mipaka ya Tanzania ina mialo 580 iliyo rasmi ,wavuvi 102,000, vyombo vya uvuvi 36,000.

Kwa Upande Mwingine Makamu Mkurugenzi wa Kituo cha Uvuvi cha Afrika Mashariki Bwana Anton Ntunganyaho amesema kupitia Mradi huo utawezesha kuwajengea uwezo wavuvi katika kuhakikisha Uvuvi haramu unatokomezwa.

Kongamano hilo limefanyika ndani ya Siku mbili katika Ukumbi wa Golden Tulip Hoteli Jijini Dar Es Salaam .

Source: KONCEPT TV
 
The Lake Victoria Fisheries Organization (LVFO) is a specialized institution of the East African Community (EAC) whose mandate is to coordinate the management and development of fisheries and aquaculture resources in the EAC region.

A Conference of Plenipotentiaries on the Establishment of the Lake Victoria Fisheries Organization, which was held in Kisumu, Kenya, on 30 June 1994, adopted the Convention for the Establishment of the Lake Victoria Fisheries Organization (LVFO). The Convention was registered with the Secretariat of the United Nations on 30 July 1996 under registration number 32987.

At its 9th Session held in Nairobi, Kenya, on 29 January 2016, the Council of Ministers of the LVFO adopted amendments to the Convention with a view to, inter alia, opening membership to all Partner States of the East African Community, and extending the competence of the LVFO to the fisheries and aquaculture resources of the East African Community water bodies.

The amendments entered into force thirty days after their adoption, that is, on 28 February 2016 and the Republic of Burundi officially acceded to the convention on 4th October 2017.

Source: Welcome to Lake Victoria Fisheries Organization | East African Community
 
Back
Top Bottom