EU na WB ni kama wanawajibu Tundu na Zitto...

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
239
500
EU na WB KAMA WAMEJIBU WA ZITTO NA LISU....

Na Elius Ndabila
0768239284

Ikumbukwe hivi karibuni baada ya uchaguzi mkuu kufanyika, vyama vya siasa vilivyoshindwa Uchaguzi huo hasa CHADEMA NA ACT waliandika barua kwenda UN, Umoja wa Ulaya na kwenye mataifa mengine kushinikiza Tanzania kuwekewa vikwazo. Walienda na hoja dhaifu kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Lakini walipojaribu kuhalalisha hoja zao dhaifu kwa kutaka kuwapeleka wananchi kwenye maandamano wananchi waliwagomea kwa kuwa waliridhika na mchakato huo.


Pigo kubwa kwao ni kuwa EU na WB zimetoa msaada kwa Tanzania kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo njia ya umeme wa KV 400 kwenda mpaka wa Tanzania na Zambia. Hili ni pigo kwa viongozi ambao wanaamini wasiooshinda basi uchaguzi si huru na haki na kuanza kuzurura kuisingizia nchi mambo mabaya ili tu kuona nchi inakwama kupiga hatua za kimaendeleo.

Tanzania tuna upinzani ambao tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 hawajawahi kusema uchaguzi ni huru na haki. Lakini jambo la kushangaza pamoja na kila mwaka kusema Uchaguzi si huru na haki lakini wamekuwa wakigombea. Kitendo cha EU na WB kuendelea kuisaidia Tanzania kama mikataba ya Umoja wa Mataifa inavyosema ni uthibitisho tosha kuwa wamechoshwa na wanasiasa wa Tanzania ambao ni washirika wa Mabeberu kutaka kuikwamisha Tanzania. Beberu ni mtu yeyote anayepinga maendeleo na kutaka kunyonya damu ya mwingine. Kwa sisi watanzania beberu ni mtu wa rangi yoyote anayeweza kuhujumu maendeleo ya Taifa.
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,529
2,000
Sasa hivi wamekuwa Wadau wa Maendeleo na ninyi mmebadili usemi wenu kuwa hamhitaji msaada toka kwa Mabeberu kwani hamko tayari ku suport mapenzi ya jinasia moja. Aibu sana ninyi msiojua mnapinga na kukubali nn.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom