EU, Marekani wajitosa mgogoro wa Katiba

Kwa level ambayo mgogoro huu umefikia sasa inatakiwa rais kikwete aingilie kati.Kikwete amekua na historia ya kwenda tofauti kidogo na maamuzi ya wanachama wenzake wa CCM,tukumbuke kwamba wana CCM karibu wote walikua wanapinga ishu ya kuundwa kwa katiba mpya,ni kikwete ndiye aliyeamua kwamba katiba iundwe.Kwa mtazamo wangu,huu ni wakati mwafaka raisi asiridhie hii sheria pale itakapopitishwa na wabunge wa CCM.Kutokutia sahihi kwake kuwe ni sababu ya kuurudisha kwa wannchi ili kuweza kupata "People owned Constitution". Kama Rais hatasoma alama za nyakati,hii issue itakua ni mgogoro mkubwa sana hapo baadaye.

Nawasilisha.
 
Hekima na uvumilivu vinahitajika mno sasa kuliko wakati wowote ule kwani vikikosekana nchi hii inaweza kutumbukia katika mgogoro na machafuko ambayo si CCM na serikali wala wananchi watakaofaidika.
Ni wajibu wa CCM (hasa hasa Spika wa Bunge na Rais) kukubali kuwa walipitiwa kwa kudhani kuwa wanaweza kufanya wapendavyo na wengine wote wakanyamaza kwa sababu tu wao wako wengi bungeni.
Kulikuwa na sababu gani kwa Bunge kushindwa kutekeleza maelekezo yake kwa kukusanya maoni zaidi ya wananchi kama kuagiza muswada utafisiriwe kwa kiswahili ilikuwa kuwawezesha wananchi hao hao kuuelewa? Sidhani kuna mbunge au mjumbe wa kamati ya sheria na katiba alikuwa hauelewi muswada ule ulipokuwa umeandikwa kwa kiswahili.
Nilidhani baada ya kutafisiriwa wananchi wangepewa nafasi ya kuujadili na kutoa maoni yao kabla ya bunge kuujadili na kuupitisha kuwa sheria, ni ubabe tu ambao kwa sasa hauna nafasi kwani uelewa umeongezeka siku za ndiyo mzee zimeshapita.....
TUNATAKA KATIBA YETU AMBAYO SOTE TUTAJIVUNIA KUWA TULISHIRIKI KUITENGENEZA,,, ukiwemo mchakato wa kutengeneza utaratibu!
 
Ama ni KATIBA MPYA YA WANANCHI BILA UDALALI wa ikulu humo au hakuna kabisa zoezi zima la upatikanaji wa katiba kupitia bunge Dodoma!!!

Kwa level ambayo mgogoro huu umefikia sasa inatakiwa rais kikwete aingilie kati.Kikwete amekua na historia ya kwenda tofauti kidogo na maamuzi ya wanachama wenzake wa CCM,tukumbuke kwamba wana CCM karibu wote walikua wanapinga ishu ya kuundwa kwa katiba mpya,ni kikwete ndiye aliyeamua kwamba katiba iundwe.

Kwa mtazamo wangu,huu ni wakati mwafaka raisi asiridhie hii sheria pale itakapopitishwa na wabunge wa CCM.Kutokutia sahihi kwake kuwe ni sababu ya kuurudisha kwa wannchi ili kuweza kupata "People owned Constitution". Kama Rais hatasoma alama za nyakati,hii issue itakua ni mgogoro mkubwa sana hapo baadaye.

Nawasilisha.
 
KATIBA MPYA YA WANANCHI IKISIMAMIWA NA WANANCHI WENYEWE LAZIMA IPATIKANE KUANZIA SASA NA SASA HIVI TU 'BILA HARUFU YOYOTE YA UDALALI NDANI MWAKE'!!!!

Makamanda wetu wooote CHADEMA na hivi sasa nako TLP na NCCR-Mageuzi, ukweli ni kwamba hivi sasa TUNAHITAJI KATIBA MPYA YA WANANCHI BILA UDALALI WA IKULU kwa leo na sasa hivi bila CCM wala bunge lake.

Cha msingi njooni kwetu nyinyi wenyewe pamoja na wanaharakati wengineo mkatuulize maoni yetu juu ya NJIA IPI KUFWATWA kupatikana kwa katiba mpwa yetu sote kama wananchi wa Tanzania bila mizengwe zaidi ya CCM.

Mkija kwetu bila shaka tutawapeni idhini yetu ya moja kwa moja juu ya kitu gani cha kufanya KUPITIA KWENYE KUKUSANYA SAHIHI ZETU ZAIDI YA MILIONI 1 na baada ya hapo kazi iendelee kwa misingi ya RATIBA YA WANANCHI PAMOJA NA HADIDU ZA REJEA.

Dr Slaa tunaomba kazi hii ianze sasa na SASA HIVI BILA KUENDELEA KUUZIWA MANENO MATUPU NA WAZEE WA CCM.
 
Wakilumbana waliosoma na kuona mbele kuliko sisi ni njia sahihi ya sisi kupata mwanga wa kweli....
 
KAMANDA LEMA VIJANA TUNAKUOMBA UJE VYUO VIKUU NA MIKOA YOTE KUTUPA SOMO JUU YA MADA YA 'UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA'

Kamanda Lema vijana wenzako hivi sasa tunahitaji elimu yako juu ya katiba mpya ya wananchi na jinsi itakavyotusaidia kulinda kile ulichokiita 'UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA'.

Kile kinachoendelea bungeni Dodoma ni kule CCM na maswahiba wake wachache kuchagua kujifurahisha wenyewe huko juu ya hili jambo la kufa na kupona kwetu sisi vijana.

Makanda Lema tunaomba uzunguke mikoa yote kutueleza
somo juu ya HAKI NA UTU WA MTANZANIA na jinsi ambavyo tutaweza kupata katiba ya wananchi bila udalali wa ikulu ili tukafikie azma hiyo hapo juu.
 
Msijaliii.. wamekuja kuangalia namna ya kumuandalia faili la mashitaka ocampo atakapoanza kuwapeleka ccm kwenye mahaka ya kimataifa kwa mauaji ya kimbari wanayoyaandaa kupitia kwa shamswi naoza!
 
kipofu akikutukna mwache aende zake maana hata akitangulia siku 100 mbele anweza bado kuwa nyuma yako
 
Kwa level ambayo mgogoro huu umefikia sasa inatakiwa rais kikwete aingilie kati.Kikwete amekua na historia ya kwenda tofauti kidogo na maamuzi ya wanachama wenzake wa CCM,tukumbuke kwamba wana CCM karibu wote walikua wanapinga ishu ya kuundwa kwa katiba mpya,ni kikwete ndiye aliyeamua kwamba katiba iundwe.Kwa mtazamo wangu,huu ni wakati mwafaka raisi asiridhie hii sheria pale itakapopitishwa na wabunge wa CCM.Kutokutia sahihi kwake kuwe ni sababu ya kuurudisha kwa wannchi ili kuweza kupata "People owned Constitution". Kama Rais hatasoma alama za nyakati,hii issue itakua ni mgogoro mkubwa sana hapo baadaye.

Nawasilisha.
Unamwamini huyo? janja yake huwa hataki kuonekana mbaya atalianzisha then yeye anasikilizia akiona moto anajifanya si yeye, kumbuka alivyowageuka kina EL kwenye mtandao, umesahau kaanzisha dhana ya Gamba lakini wanaoumia ni kina Nape yeye amejiweka pembeni.
 
Bora spika wa zamani kimakonde kinapanda je jenista aliyezoea kupokea miongozo ya kina Lusinde wa form seven?

Maoni ya kafulila ni mwiba kwa ccm. Nashauri cdm uwashirikisheni hawa vijana wa nccr muangalie namna ya kuendesha mchakato wa katiba sambamba na huu wa serikali ili kuondoa uhalali wa huu mchakato wa serikali na ccm. Mkifanya hivyo mnaweza kuisumbua ccm hapa mpaka uchaguz ujao.big up kafulila. Tunajua we ni mwanachama wa cdm huko nccr uko uhamishoni.
 
Nadhani weupe wanawasiwasi na miradi yao ya kifisadi iliyopo nchini!!

Kumbuka wao ndo wafadhili wakubwa naamini hata hela kwa ajili ya mchako mzima wa katiba mpyta watatoa wao, Serekali hii ya MKwee..haina uwezo wa kutoa hela kwa ajili ya mchakato mzima,
Kwahiyo wazungu wakisema hapana na amini itakuwa hapana.
 
CHADEMA, NCCR-Mageuzi pamoja na wanaharakati wengine wengi tunaojali UBINADAMU, HAKI na UTU WA KILA MTANZANIA kuheshimiwa, kazi ianze sasa hivi kukusanya sahihi milioni 1 ili wananchi tukajianzishie Mchakato wetu wa moja kwa moja kujitungia katiba.

Hao wanaopendelea Katiba Viraka kupitia udalali wa ikulu wao tutakutana kwenye REFERENDUM kupigia kura Rasimu mbili tofauti za Katiba Mpya; (1) Rasimu ya Katiba ya Wananchi wenyewe bila UDALALI ikishindanishwa na (2) Rasimu ya Katiba ya CCM na Ikulu kwa ajili ya Wa-Tanzania.

Katika hili la Katiba Mpya ni bora kieleweke kimoja na wala hakuna salia mitume hadi hapo!!!
 
Back
Top Bottom