EU, Marekani wajitosa mgogoro wa Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EU, Marekani wajitosa mgogoro wa Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Nov 17, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  WAKUTANA NA OFISI YA SPIKA, UPINZANI BUNGENI DODOMA

  MVUTANO baina ya wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi kwa upande mmoja dhidi ya Serikali na wabunge wa CCM kwa upande mwingine, umevuta nchi wahisani ambao wametuma maofisa wake mjini Dodoma kuchunguza kiini cha mvutano uliopo. Ujumbe wa maofisa watano ukiongozwa na Balozi wa Sweden nchini, Lennart Hjelmaker ulifika katika Ofisi ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na baadaye kukutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila.

  Imeelezwa kwamba ujumbe huo wa nchi ambazo ni wafadhili wa Tanzania, umehoji masuala mbalimbali kuhusu mchakato unaoanza sasa wa kuiwezesha Tanzania kupata Katiba Mpya.

  Taarifa hizo zinasema, maofisa hao wengi wakiwa ni wale wanaohusika na ushauri wa masuala ya siasa katika balozi hizo, wamekuwa wakihoji hatima ya msimamo wa upinzani ambao waliamua kususia Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.

  Chana akizungumza na kwa simu jana alikiri kukutana na ujumbe huo ambao pia uliwajumuisha maofisa kutoka balozi zilizopo kwenye mabano, Logan Wheeler (Marekani), Veslemoy Lothe Salvessen (Norway), Mark Polatjko (Uingereza) na Dk Carol McQueen (Canada).
  Maofisa hao wakiambatana na wengine kadhaa, jana asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni, walitambulishwa na mmoja wa wenyeviti wa Bunge, Janister Mhagama wakiwa kwenye Ukumbi wa Spika.

  Chana jana alisema: “Ndiyo nilikutana nao na walichotaka kufahamu tu ni jinsi mchakato mzima wa sheria hii ulivyokwenda na hatua zote tulizopitia kama kamati hadi kufikishwa kwake bungeni.

  Alipoulizwa iwapo walihoji suala la Wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi kususia mjadala wa muswada huo, Mwenyekiti huyo alijibu kwa kifupi tu: “Ndiyo, hata hilo walitaka kufahamu lilivyokuwa.”Imeelezwa pia kwamba ujumbe huo ulifika Ofisini kwa Spika Makinda, lakini haikufahamika mara moja kama walipata nafasi ya kuzungumza na kiongozi huyo wa Bunge, kutokana na jana kutokuwepo ofisini.

  Wabunge wa upinzani

  Juzi usiku, ujumbe huo ukiongozwa na Balozi Hjelmaker ulikutana na Lissu pamoja na mambo mengine ukihoji sababu za kutoka nje ya ukumbi wa bunge. Ujumbe huo pia ulihoji hatua ambazo wapinzani hao wanakusudia kuchukua ikiwa Bunge litatumia wingi wa wabunge wa chama tawala kupitisha muswada huo, kisha kupata baraka za Rais na kuwa sheria ya nchi. Pia walihoji iwapo kuna dalili zozote za kufanya mazungumzo ya kuwezesha pande husika kufikia mwafaka wa pamoja, ili wote waweze kushiriki katika mchakato wa kuwezesha nchi kupata Katiba Mpya.

  Akizungumzia kukutana ujumbe huo Lissu alisema: “Ndiyo, nimekutana nao na wamehoji mambo mengi kwelikweli lakini niseme kwamba inavyoonekana wana hofu kuhusu investiment (uwekezaji) ikiwa hakutakuwa na makubaliano.”

  “Nimewaambia kwamba sisi msimamo wetu ni kwenda kwenye mahakama ya wananchi, kuwaambia kwamba tumekataa kuhalalisha mchakato haramu wa upatikanaji wa Sheria maana tangu mwanzo kanuni na sheria za nchi zilikiukwa.”

  Kwa upande wake, Kafulila pia alikiri kukutana na ujumbe huo jana, bila kuwapo kwa Balozi wa Sweden ambaye aliondoka Dodoma kurejea Dar es Salaam, baada ya kipindi cha maswali na majibu.

  “Kwangu ni kama walitaka kufahamu kuhusu mambo matatu, kwanza kwa nini tuliamua kutoka nje, nilivyotumia nafasi yangu ndani ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala nilipoteuliwa na Spika kuingia kwenye kamati hiyo na nini kinafuata ikiwa muswada huo utapitishwa na baadaye kuwa Sheria,” alisema Kafulila na kuongeza:

  “Kwa kifupi nimewaambia kwamba sababu za kuondoka ziko wazi na tumezisema mara nyingi, lakini kubwa nimewaambia kwamba mimi mawazo yangu ni kuwahamasisha wanaharakati na hata wabunge wenzangu wa Chadema kuona kama tunakuwa na mchakato wetu, sambamba na ule unaofanywa na Serikali.”

  Kafulila alisema mchakato huo utawawezesha wanaopinga wa Serikali kuwa na mfano wa bora na kwamba matokeo ya kazi hiyo, yatatumika kuushawishi umma wa Watanzania kupiga kura ya hapana dhidi ya Katiba ‘haramu’, inayokusudiwa kutungwa kutokana na mfumo ‘haramu’.

  Siku za mjadala zaongezwa

  Mjadala kuhusu muswada huo uliendelea jana na umeongezewa siku hadi leo utakapohitimishwa majira ya mchana.Habari zilizopatikana zinasema kuongezwa kwa muda wa majadiliano kunaweza kuathiri ratiba ya Bunge na kwamba upo uwezekano wa kuongezwa kwa siku moja ili Bunge liahirishwe Jumamosi.

  Mkutano wa Tano wa Bunge, bado unakabiliwa na kazi ya kujadili muswada mmoja wa sheria na kupokea taarifa mbili za kamati ambazo kimsingi zinaweza kuhitaji kujadiliwa.

  Taarifa hizo ni ile ya Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa akichunguza tuhuma za Wizara za Serikali kuchangisha fedha kutoka katika taasisi zilizoko chini yake kwa lengo la kupitisha bajeti bungeni na ile ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusu sekta ya gesi nchini.

  ::Mwananchi::
   
 2. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani weupe wanawasiwasi na miradi yao ya kifisadi iliyopo nchini!!
   
 3. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  EU,USA sawa kuhoji demokrasia yetu na pengine kutupa mawazo..si ushauri...lakini si sawa kuingiza maslahi yao ndani SIO SAWA. haijakaa vizuri kwani mambo ya occupy wall street yanazungumzia juu ya ulafi wa 1% ya watu wanaofaidi 99% ya uchumi wakati asilimia 99% wanatozwa kiwango cha kodi sawa na hao 1%
   
 4. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nadhani hao wakisema mswada usomwe kwa mara ya kwanza bungeni basi watasikilizwa lakini sisi wananchi tunaambiwa tukae kimya tulishaujadili! Lini? hatuambiwi, wakinanani? hatuambiwi... kwa maslahi ya nani hatujui! Mama Anne Makinda anaweza kulitumbikiza taifa kwenye maafa makubwa!
   
 5. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wasiwasi wangu isikute hata budget ya kuendesha shughuli za mchakato wa katiba inawategemea hao eu na usa.coz mbali ya hawa jamaa kuwa na wasiwasi na investment zao pia wanahofu misaada yao pia.
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  'NATIONAL CONSTITUENT ASSEMBLY' THE ONLY WAY TO SAVE CCM HEADACHE OF UNCORKING COUNTRYWIDE VIOLENCE ON DRIVE TO NEW CONSTITUTIONAL MAKING

  A quick survey out there; upcountry and in most of our streets are by no doubt a direct confirmation that Tanzania is currently ripe for and at best is in top yet irreversable gear toward attaining OWN popularly designed people constitution for the people and by the very ranks and files our entire citizenry, for the first time in history.

  This way, it all explain itself as to how much opposition-led call for new constitutional reforms is highly revered by a larger majority that would jelously NOT LET anyane - not even the president - to seek to monopolise the stage toward this endeavour. This means that losts of selfless sucrifices could very well be on the air, greater steaks though notwithstanding, in order that this monumental goal is achieved with minimal hurdles today or tomorrow.

  It is fo this reason that the opposition forces, the international community and the expansive civil society in the country are adamantly insistent that Constitutional making both today and now and with every other stakeholder brought on board as an ACTIVE PARTICIPANT throughout the entire exercise on equal steps with all other colleagues to the whole process in question.

  Hence, it is for this sole reason tha we hereby point out tha constitutional making in Tanzania MUST this time around be indeginous, TOTAL, and most SWEEPING COSTITUTIONAL OVERHAUL an experince in the best interest of common citizen and NOT being turned into a government project of any sorts.

  Yes, we would indeed love to see the entire constitutional processes being as transparent, highly participatory common-citizen modelled as the directing and managing force at all time. In other words, constitutional making in Tanzania MUST just take the approaches that are purely divorced of the ruling authorities and be replaced by the subjects of the nation as the core everything that goes on in there.

  Even though getting the much awaited constitution so important to everyone of us out here, THE PROCESSES AND PROCEDURES through which it is to be realised are even more crucial than anyone would imagine of it all.

  Just like any other social contract for puposes of governance, the constitutional making must be a product of National Constituent Assembly to which the current governt also just get a seat or two to be represented of its divergent opinions BUT NOT as the big brother to other equally interested groups of that kind of people and not championing the whims of chosen few who would wish to defeat any move of putting people at the centre stage as the mainstream architects of a constitution of own dreams and hopes over years.

  Indeed, we expect to see and it is everyone's wish as well as being that of the entire international community to see the current parliament undertake its founding role to the best wishes of the general public and NOT to the best wishes of the ruling CCM that is equally one of the many interested entities to the wider constitutional making phases and processes yet to come.

  We would want to take a glimpse of an ordinary persons a being on the driver's seat spearheahed by ordinary members of the public in their various interest groups, we want to see more and more of people in the grassroots taking centre-stage as the key drivers of the process and to see lesser and lesser of the GOVERNMENT taking back-seat on the entire exercise.

  However, any move take from outside these democratic frameworks may most miserably fall on its nose by way of simply collecting 1 million signatures from members of the public to reject any insinuation of a constitutional making WITH ANY OR SEVERAL GOVERNMENT OFFICIALS SUPPERIMPOSING themselves to act for and on behalf of all other interested groups out thtere without any prior consent of any kind. A turn of event like that would squarely mean a waste of time and financial resources.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wanataka kuona na spika...wangeongea naye kwa kiswahili au kingredhaa...
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Juhudi za kupatikana kwa KATIBA MPYA YA WANANCHI bila udalali kupitia ikulu, wanaharakatiki na sauti huru zote nchini - you will never walk alone on this most tedious exercise but a multi-generational gift into the future.

  Wakwamishi wa matakwa ya umma ni bora wakajihadhari maan mambo ni mazito mno hapo mbeleni kidogo. Haya yalioanza bado ni cha mtoto tu hivyo na sisi tukaongeze juhudi zaidi kukataa KATIBA MPYA kupitia ikulu na badala yake tuseme hewala upatikanaji wa KATIBA MPYA kwa njia ya Baraza la Taifa la Wadau wote wa Katiba.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KATIBA MPYA NCHINI BILA CCM INAWEZEKANA!!

  CHADEMA pamoja na Wanaharakati wote nchini, tunahitaji kukusanya sahihi milioni 1 ya wananchi wenye umri wa ya miaka 18 na zaidi na kutufanyakufanya maamuzi mazito kama vile kutupilia mbali maamuzi yoyote ya bunge kumhodhisha Rais Kikwete (mtumishi namba moja wa katiba) kujipa mamlaka ya kujimilikisha haki ya umma kujitengenezea katiba mpya bila udalali maana katiba si mali ya ikulu wala bunge bali hivyo vyombo viwili ni uzao tu wa katiba.

  Naomba nirudie, wenye katiba ni sisi wananchi tutakaotilia sahihi maamuzi kama hayo hapo juu. Najua wanasheria ndani ya CCM wanajua fika maana ya hatua hii pindi tukifika mbele ya chombo chochote huru chenye maamuzi kisheria ama kitaifa au kimataifa.

  Na kwa njia hiyo hiyo, vile vile UWEZO TUNAO wa kujikusanyia maoni juu ya utaratibu upi utumike kupatikana kwa katiba mpya na hivyo hizo hizo sahihi hizo zaidi ya watu milioni 1 ikafanya maoni hayo yakawa ni
  Authoritative Dacument inayoruhusu mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya kuendelea hata bila ya wale ambao wanapendelea kutumia udalali wa ikulu kwenye zoezi zima kwemo katika mchakato.

  Hadidu za rejea nazo zikakusanywa na kupitishwa na idadi kama hiyo hiyo ya sahihi milioni 1 na mchakato kuendelea kama kawaida bila zengwe.

  Hebu tufikiri mbele zaidi na tufikiri nje kabisa ya mifuniko ya mdau mmojawapo tu wa Baraza la Katiba Taifa aitwaye CCM.
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ZIBA SANA TUNDU LA HEWA SAFI YA 'KATIBA MPYA BILA UDALALI' TUFE NA WEWE!!

  Siku si nyingi sana siasa za KATIBA MPYA nchini kupanda daraja nyingine kabisa isiotarajiwa hasa na baadhi ya watawala ving'ang'anizi ya ukale endapo MAWAZO MGANDO NA HOFU YA BAADHI YA WATAWALA hayatapitisha Nguvu ya Umma kusikika matakwa yake.

  Haya malalamiko mengi nchini, ufisadi serikalini, umasikini wa kutwishwa, ukatili wa vyombo vya dola na mauaji holela ya raia kila kukicha yote majibu yake ni KATIBA MPYA bila udalali nchini.

  Tanzania kwa sasa unyeti wa swala la KATIBA MPYA na wale wenye kuweka vizuizi vingi njiani, kwetu sisi wananchi ni tunawaona sawa tu na mtu yeyote yule ambaye anajaribu kutuzibia hata ka-tundu pekee la kuingizia hewa shimoni mithili.

  Watanzania kwa mahitaji yetu ya KATIBA MPYA BILA UDALALI hatuna tofauti kbisa na hali aliyokua nayo Saddam Hussein na kuhitaji kwake hewa shimoni wakati akijificha Wa-Marekani wasimtie nguvuni.

  Endelea kuziba tundu pekee la hewa safi ya KATIBA MPYA BILA UDALALI na wananchi tufe na wewe bila ajizi!!
  [​IMG]
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Canada wana wasiwsi sana na mipesa wanayoipata through Barick kwenye Gold yetu!!
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,172
  Trophy Points: 280
  Hao ccm inawaogopa wakishauri itasikia
   
 13. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usiwe na hofu wakalimani wapo wengi tu.
   
 14. M

  Marytina JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kazi imeanza
   
 15. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Si rahisi kama wanavyolichukulia CCM, migogoro mingine ni bora kuiepuka mapema tujifunze kwa jirani zetu Kenya. Hatutavumilia kuona katiba ikitungwa na CCM! What is CCM by the way? Si ni kama vyama vingine? iweje wao wanajiona wanahaki na kila jambo? IKO SIKU NAO WATAKUWA NJE
   
 16. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  wasituchanganye hawa wawekezaji....sisi ndio tutaamua hatima ya nchi yetu
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kama alivyosema kafulila, muswada mbadala wa katiba uandaliwe kisha ulinganishwe na uliopo. Wananchi wapewe wausome, wahubieiwe kwenye majukwaa na ndio waamue kati ya hayo mawili
   
 18. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Ndilo tatizo la hawa wezi.
   
 19. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda sana hii alternative ya Mh. Kafulila. Kama kweli wapinzani wako serious they should follow this path,
  believe me hii itakuwa ni mwiba mkali kwa muswaada huo wa CCM. Kweli wapinzani wana wabunge makini. Go Kafulila,
  Go wapinzani. Katiba ni haki yetu wa msingi ni sio hisani ya JK wala CCM kama wanavyopotosha akina Hamad na CCM.
   
 20. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mashambulizi kwa upinzani
  Jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliungana na Mawaziri Profesa Anna Tibaijuka wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu kuchangia muswada huo na kutuhumu kauli zilizotolewa na Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba, Tundu Lissu akisema ni mpotoshaji.

  Wassira alisema anakishangaa Chadema kwani wakati wanagombea Urais mwaka 2010, walisema “Wakichukua tu madaraka nchi hii watahakikisha wanatubadilishia katiba ndani ya siku 100 lakini sasa hivi wanabadilika tena wanasema haraka ya nini.”

  Alisema hata wasomi na wanaharakati nao pia wanawapotosha wananchi kwa kusema mambo yasiyo ya kweli kuhusu mchakato huo. Alisema wasomi wanadai kwamba Bunge linatunga Katiba wakati wanajua halina mamlaka hayo, badala yake wanatakiwa kupelekewa wananchi waipitie na kutoa maoni yao.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge alisema kuna kundi la watu linapotosha wananchi kwa kujiona wao wanachokitaka lazima kiwe hivyo hivyo. Chenge ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema kundi hilo linashinikiza wananchi kufuata maoni yao kwa sababu limejiaminisha kwamba wao pekee ndiyo wanaoweza kutoa maoni yao yakasikilizwa na zaidi ya Watanzania 40.

  Profesa Shivji
  Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma ya Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji alisema unatakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza. Alipendekeza Tume ya Katiba kuwa na wataalamu wasiozidi 20 badala ya 30, kwani idadi hiyo ni kubwa mno akitaka pia majina ya wanaotakiwa kuiunda wapendekezwe na vyuo vikuu na vyama vya kitaaluma na Rais ateue majina kutokana na mapendekezo hayo.

  Waziri Nahodha aonya
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata wote wanaotishia hali ya amani kwa kutangaza kuitisha maandamano bila kikomo.

  Nahodha alisema jeshi hilo linatakiwa kuchukua hatua hiyo ya kuwakamata wanaotishia usalama wa raia kwa kutoa maneno ya uchochezi kwa wananchi ya kuandamana kuhusu katiba kwani ni kosa.

  Wakati Nahodha akisema hayo, Baraza la Vijana la Taifa la Chadema (Bavicha), kupitia kwa Mwenyekiti wake, John Heche limetangaza kufanya maandamano katika majimbo ya wabunge wote watakaounga mkono muswada huo.Habari hii imeandaliwa na Neville Meena, Dodoma Keneth Goliama, Hussein Issa na Geofrey Nyang'oro, Dar

  Source: Mwananchi.


  Binafsi najiuliza, kuna nini hapa mpaka EU na Marekani waingilie? Ni rafiki zetu sawa lakini kuna usemi unasema 'waache waliwali wale wali wao', mpaka kufikia kwao kuingilia then this is not a national issue anymore. Mengi yatajiri kwa sababu ya hili.

  Lakini pia, hayo mapendekezo ya wapinzani ni sahihi kwa Tanzania tunayoitaka kwanini serikali hailioni hilo yet inajiita "serikali sikivu" hapa usikivu uko wapi?
  Its about time peoples power take charge, period!
  Tupo nyuma yenu wapinzani.
   
Loading...