Free ideas
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 3,508
- 2,060
Unajua katika mifumo mbalimbali ya maisha binadamu tunayoishi inaweza kulingana au kutofautiana kulingana na vile mtu apendavyo kuishi. Suala la huyu jamaa kununua hiyo Samsung Galaxy Note (1,2,3) kwa mtazamo wangu siwezi kumshangaa hasa ukiangali kila mtu ana vipaumbele vyake katika maisha ya kila siku. Si ajabu wewe ukanunua kiwanja kwa ajili ya ujenzi na mtu mwingine akakushangaa. Cha msingi ni kutoingilia maisha ya mtu kwani haitakusaidia zaidi ya kukuletea machungu (makwazo).
Wakati niko mwanafunzi niliwahi kuapa kwamba siwezi kumpa mwanamke Tsh. 100,000/- kamwe hat iweje.Lakini mambo yanabadilika.Maisha na kutumia inategemea na wakati na nafasi.Ikiwa unapata laki moja kwa mwez ni hakika huwezi kutumia laki mbili kununua simu.,Ukiwa unaingiza laki saba kwa siku ama masaa,si ajabu kutumia million mbili kununua saa ama simu.kwa hiyo huyo ndugu hapo juu itakuwa anashangaaa kwa kuwa eidha,hana hicho kiasi ama haingizi kiasi kikubwa .