Eti Tuma MPESA bure! Tanzania nchi ya ajabu sana!

qq.com

JF-Expert Member
Jan 9, 2012
368
123
Hivi TCRA wapo wanafanya kazi? makampuni ya cm yanaibia watu kwa kutoa matangazo kuwa unatuma PESA bure kupitia Mpesa wakati ni uongo na jamaa wa TCRA wanakwenda kazini kila siku nao wanapokea hizo SMS? kwakweli ningeomba wawekezaji dunia nzima wanaotoka kupata faida kwa KUIBIA WATEJA waziwazi waje katika JAMHURI YA MUUNGANO WA (t)DANGANYIKA.

-re-enw[wmm sana
 
COURTESY

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
2,007
703
Makampuni ya simu ya Tanzania ni ya kipuuzi sana yaani utadhani hamna sheria maana
wanaamua kitu chochote wanachotaka,wanakukata kipuuzi sana kwa mfano mtandao wa tigo
mtu akikurushia muda wa maongezi unakatwa hela,mamlaka ya mawasiliano hamna policy au
huu upuuzi sijui utaisha lini kwenye hii nchi,inakera sana.
 
dapo

Senior Member
Oct 26, 2012
100
10
Hivi TCRA wapo wanafanya kazi? makampuni ya cm yanaibia watu kwa kutoa matangazo kuwa unatuma PESA bure kupitia Mpesa wakati ni uongo na jamaa wa TCRA wanakwenda kazini kila siku nao wanapokea hizo SMS? kwakweli ningeomba wawekezaji dunia nzima wanaotoka kupata faida kwa KUIBIA WATEJA waziwazi waje katika JAMHURI YA MUUNGANO WA (t)DANGANYIKA.

-re-enw[wmm sana

kama airtel
 
nlambaa

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
361
55
Ni kweli kabisa hawa voda mpesa ni wezi wanaoshirikiana na mawakala, kwa mfano kilichinikuta ni kuwa last week ijumaa niliweka mpesa kwa wakala nikiwa mbeya mjini. Baada ya kuweka na kuonekana kwangu nikatuma kwa mtu, nikapata msg kuwa hela niliyokuwa nayo haitoshi kutuma, basi nikapunguza kiwango, ikatuma ma kukata toka akaunti yangu, lakini cha kushangaza ni kuwa niliye mtumia hakupata. Baada ya kurudi dar nikaenda vodashop, wakaangalia kwenye compute wakaona kuwa ile transaction ilikuwa incomplete hivyo wakaniambia kuwa ile hela ilirudi kwa wakala. Sasa mtihani uko hapo, mie niko dar wakala mbeya. Jne nikaunganishwa na huyo wakala, yeye anadai haikurudi, mimi nimekatwa sijui ni nani hasa ana hela yangu. Nikafuatilia tena voda juzi, mpaka sasa sijapata jibu. Ombi langu kwa TCRA ni kuwa wa tanzania wengi tunalizwa na hii mitandao ni nyie kamw regulator hamtusaidii. Kinachoniuma ni mkuwa hela nilikuwa namlipa fundi aliyenifanyia kazi fulani hivyo ilibidi nitume amount nyingine kwake. Hata hivyo pamoja ni kidogo nitahakikisha nafuatilia hadi ukweli ujulikane maana inawezekana ni wapiga dili hawa.
 
ndomyana

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
5,005
1,139
Wakuu mi jana nimetuma hela wakanipa hiyo ya kutumia sh1500. Leo asbuhi wameichukua huu usanii wa hii mitandao unauzi sn
 
chumvichumvi

JF-Expert Member
May 6, 2010
1,208
293
kama airtel
Kwa airtel chini ya laki moja ni bure kweli sema mawakala wengi wanagoma kufanya izo transactions za airtel as wana-claim hazina faida kwa mfano jana nilikuwa kariakoo imagine nilitembea kwa mawakala zaidi ya 9 wote hawana airtel ni voda na tigo
 
chumvichumvi

JF-Expert Member
May 6, 2010
1,208
293
hapa Tz kuna taasisi zingine huwa najiuliza uwepo wake unamaana gani kama hawa TCRA bajeti wanapewa vitendea kazi wanavyo hadi ushaidi ambao ni unajitosheleza upo sasa nini wanasubiri ili wafanye kazi au amri ya raisi au waziri husika na sekta hiyo nae mpiga deal wao nn maana inachosha sasa yani nobody is there for anybody kwenye hizi matatizo but ingekuwa ni maswala ya kura hapa fasta hii ingekuwa vice versa nobody is there for anybody
 
Kiyoya

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,625
788
Afadhari makampuni haya wangekuwa wanalipa kod sawsawa-lakin tatizo ni kwamba ndugu zetu,kaka zetu,dada zetu na na nihii zetu wanafaidika na huu utaratibu we huoni mijengo yao
 
Butho Mtenzi

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
331
22
Hawa ni wez tu hawana lolote wanakata hela wana kupa vocha nayo ina limitation ni kutaka kuwafanya watu wawe wanapiga cm ata ambazo hazna tija
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,499
9,908
TCRA-Tanzania Communications Rotten Authority
Makampuni hya yanafanya yakatavyo kwa kuwa hakuna WATCH DOG wa kuwakemea au kuratbu nyenendo zao, TCRA hiko likizo kabisa - familia yangu imekwisha honja joto la jiwe kutokana na mambo haya ya kutuma pesa kupitia Airtel - tulimtumia mtu laki tatu kumbe hela hazikwenda kunako husika na wenyewe wanakili kwamba walifanya makosa, lakini mpaka sasa hivi tunapo zungumza hela hizo hatujarudishiwa tunaingia mwezi wa nne, tunapigwa danadana TU.
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,499
9,908
hapa Tz kuna taasisi zingine huwa najiuliza uwepo wake unamaana gani kama hawa TCRA bajeti wanapewa vitendea kazi wanavyo hadi ushaidi ambao ni unajitosheleza upo sasa nini wanasubiri ili wafanye kazi au amri ya raisi au waziri husika na sekta hiyo nae mpiga deal wao nn maana inachosha sasa yani nobody is there for anybody kwenye hizi matatizo but ingekuwa ni maswala ya kura hapa fasta hii ingekuwa vice versa nobody is there for anybody
Mkuu jamaa wa TCRA nilisha wavulia kofia kabisa, ukiangalia kwa umakini utaona kana kwamba wana woga fulani wa kuwakemea makampuni haya ya simu, yanafanya yanatavyo. Kinacho udhi zaidi ni pale wanapo taka kuamua kitu au kuweka sheria fulani za kuzibana kampuni za simu wanagwaya sana, kabla hawaja fanya uhamuzi wowote lazima waite kampuni hizo za simu eti ziwashauri wafanye nini, raia wana lalamika kutumiwa ujumbe ambao mtu haja subscribe na wakati mwingine kulazimilka kusikia sauti za matangazo kabla huja kuwa connected na client mwenzako, ukiwa na emegency call unaweza kukwama vibaya sana kwa kulazimishwa kusikiliza matangazo na mambo mengine ya kipuuzi ya kupoteza muda, kwani vipeperushi kazi yake ni NINI? Mtu unaweza kufikili labda hakuna watu wenye ujuzi wa tekinolojia ya mawasiliano, wapunguze makongamano yasiyo na TIJA kwa Taifa letu, wawe wakali na makampuni haya yasiachwe kuliweka Taifa letu kwenye rehani.
 
Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
9,565
11,938
Wakati mwingine najiuliza kama haya malalamiko ya wateja labda hawayapati,lakini nikagundua ni kiburi tu na kufanya wanavyojisikia,kwa kuwa hao TCRA wamelala au kwa namna moja au nyingine wananufaika na huu usanii.
 
Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
574
139
Nchi ishakuwa shamba la bibi, hakuna wa kuisimamia kana kwamba haina wenyewe. Serikali yenyewe inafyata kwa kampuni za simu.... Hivyo madai ya wananchi ni kama CHOZI LA SAMAKI BAHARINI
 
keybroked

Member
Apr 6, 2012
21
5
Mkuu jamaa wa TCRA nilisha wavulia kofia kabisa, ukiangalia kwa umakini utaona kana kwamba wana woga fulani wa kuwakemea makampuni haya ya simu, yanafanya yanatavyo. Kinacho udhi zaidi ni pale wanapo taka kuamua kitu au kuweka sheria fulani za kuzibana kampuni za simu wanagwaya sana, kabla hawaja fanya uhamuzi wowote lazima waite kampuni hizo za simu eti ziwashauri wafanye nini, raia wana lalamika kutumiwa ujumbe ambao mtu haja subscribe na wakati mwingine kulazimilka kusikia sauti za matangazo kabla huja kuwa connected na client mwenzako, ukiwa na emegency call unaweza kukwama vibaya sana kwa kulazimishwa kusikiliza matangazo na mambo mengine ya kipuuzi ya kupoteza muda, kwani vipeperushi kazi yake ni NINI? Mtu unaweza kufikili labda hakuna watu wenye ujuzi wa tekinolojia ya mawasiliano, wapunguze makongamano yasiyo na TIJA kwa Taifa letu, wawe wakali na makampuni haya yasiachwe kuliweka Taifa letu kwenye rehani.

Mi nadhani January Makamba katika sehemu ambayo ingemtoa kiumaarufu ni hii, haoni wenzie kina Mwakyembe? Angelivalia njuga hili jambo la wizi wa haya makampuni na huduma zao za hovyo bila shaka nae tungemwona ni mjanja lakini toka aeingie madarakani yupo kimyaaaaaa! Au kwa kuwa dada yake yupo kwenye tasnia hiyo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom