Eti Tanzania inaogopa kuongelea mambo ya Libya ili isiharibu mahusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Tanzania inaogopa kuongelea mambo ya Libya ili isiharibu mahusiano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Feb 26, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Tanzania yaogopa kuzungumzia ya Libya


  na Shehe Semtawa
  TANZANIA imeogopa kuzungumzia mgogoro unaondelea nchini Libya kwa madai kuwa kitendo hicho kinaweza kuvuruga uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili.

  Akizungumza na wandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe hakusita kueleza bayana kile kilichotokea katika nchi za Tunisia na Misri lakini akashindwa kuzungumzia juu ya kile kinachotokea hivi sasa nchini Libya.

  Kuhusu Libya, Membe alisema kwa kifupi tu kuwa Tanzania kama nchi haiwezi kujitokeza wazi wazi kuunga mkono ama kupinga kinachotokea nchini humo kwa sababu ina raia wake wanaoishi huko hivyo kitendo chochote cha kushabikia kwa kuunga mkono ama kupinga kinahatarisha maisha yao.

  “Unajua tuna raia wetu kule sasa siyo vizuri kuonyesha utashi wetu inaweza kuhatarisha maisha ya wananchi wetu kwani hii ilitokea kule Misri kwa wale waliojitokeza kuunga mkono waliweza kushambuliwa na kuharibiwa biashara zao,” alisema Membe.

  Isipokuwa Membe aliishia kusema: “Nyie waandishi wa habari na taasisi mbalimbali mnayo haki ya kujadili bila kuingiliwa na chombo chochote.”

  Aidha, Membe alisema kuwa pamoja na vurugu zinazoendelea nchini Libya, hadi sasa hakuna raia wa Tanzania aliyeathirika.

  Akizungumzia idadi ya Watanzania walioko nchini Libya, alisema wako 26 miongoni mwao 22 ni wanafunzi ambao wako salaama na wameomba kurudi hadi hapo hali itakapotengemaa.

  Kwa zaidi ya wiki moja sasa yameibuka maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali iliyo chini ya Kanal Muammar Gaddafi.

  Kumeelezwa kuwapo kwa vifo vingi tangu vuguvugu hilo lianze, hali kadhalika miili mingi ya watu waliouawa ikiwa imeachwa mitaani huku wakazi wengine wakilazimika kukimbia makazi yao kutokana na jeshi la serikali kufyatua risasi kwa yeyote anayeonekana akiwa anaandamana.

  Mara zote, Gaddafi ambaye ametawala nchini humo kwa karibu miaka 30 sasa, akiwa na sifa ya kujiamini na kujigamba kana kwamba hakuna mtu anayeweza kumtoa madarakani.

  Lakini maandamano yaliyoibuka sasa yanaonekana kutishia mustakabali mzima wa utawala wake.

  Mbali na hilo, Membe ambaye alizungumzia mgogoro wa Misri alisema kuna Watanzania walioko nchini humo na kwamba amejaribu kuwasiliana na ubalozi wa Kenya kutokana na Tanzania kutokuwa na ubalozi nchini humo kuwarejesha Watanzania wapatao 50 wakati wowote kuanzia sasa.

  Akizungumzia kuhusu Ivory Coast Membe alisema jopo la Usuluhishi la marais watano wanaoshughulikia mgogoro wa nchi hiyo walisema kuwa nchi imo kwenye mgogoro mkubwa ambao unahitaji ufumbuzi wa haraka.

  Aliwataja marais hao waliounda jopo hilo la usuluhisho wa mgogoro huo kuwa ni pamoja na Mwenyekiti Mohamed Abdulaziz wa Mauritania, Rais Jakaya Kikwete, Blaise Compaore wa Burkinafaso, Idris Deby wa Chad na Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

  Membe alisema marais hao walipokuwa nchini Ivory Februari 21 hadi 22 walikutana na wadau mbalimbali wakiwamo Rais Alasan Quatara na Raurent Gbagbo huku wakiwasikiliza na kubadilishana mawazo kwa nyakati tofauti.

  Alisema mgogoro huo umesababishwa na baraza la katiba ambalo limemtangaza Gbagbo kama rais baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza rais aliyechaguliwa kwa matakwa ya wanchi ambapo walipiga kura bila tatizo lolote.

  Alisema jopo hilo hadi sasa halijapata ufumbuzi wa mgogoro huo hivyo basi wanatarajia kukutana tena pamoja na wadau wengine wanaohusiana na mgogoro huo katika mkutano utakaofanyika Februari 28 mwaka huu katika sehemu itakayopangwa baadaye lakini nje ya Ivory Coast ili kulinda usalama wa viongozi wengine.
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kwa mantiki hiyo Serikali ya Tanzania ni ya kinafiki..
  Hizo nchi ambazo zimetoa msimamo na raia wake wakateseka ni zipi?

  Huyu jamaa naye kumbe Mbwiga tu!
   
 3. k

  kayumba JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa Gbagbo (Ivory Coast) kungekuwapo na mafuta mbona nako tungekaa kimya!

  Tanzania siku hizi ni kama nchi za Magharibi, maslahi ya nchi kwanza!
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Huyo Membe ni vuvuzela kwelikweli anadhania sisi ni vilaza kama yeye?
  atoe sababu za kushindwa kuongelea Libya?
  kwanza hizo sababu zimeanzia lini? mbona Nyerere siku zote alikuwa mstari wa mbele kukemea uovu sehemu yeyote duniani??
  Huyo Membe hana lolote jipya zaidi ya unafiki tu
  Ivory cost hakuna watz?
  Tunisia hakukuwa na watz?
  Misri hakuna watz?
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ni zaidi ya miaka 41 kwa sasa ,wewe unaandika karibu miaka 30..kazi kweli kweli
  "When Africa is burning and the African Union is silent you begin to wonder whether this Organization is serious" - Phandu Skelemani
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hayo ndiyo yaliyofanyika Tanzania pia, kwani hatujui??
  NEC walijifungia na kutoa matokeo yao kwa matakwa yao, si hat EU wamesema?
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hamna lolote, but full unafiki!
   
 8. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Membe kaficha ukweli maana wakilaani mauaji ya libya yanawasuta yale mauaji ya kule Arusha hawana ujasiri wa kukemea hayo.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Hawana lolote wanasalandia hela za mafuta tu na kushadadia hisani za muuaji huyu. Umenotice vikao vya AU Gaddafi na Kikwete walivyo extra chummy ?

  Problem is, they are backing the wrong horse, mijitu hata haifikirii beyond pua zao. Waafrika weusi wote walio Libya wako equally jeopardized sasa, unafikiri racists wanaogeneralize kwamba mamluki wa Gaddafi ni "Waafrika" (WTF, Walibya si Waafrika?) unafikiri wanauliza wewe umetoka nchi gani?

  Hawa jamaa wanachekesha sana na excuses zao za kitoto.

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mbona Membe hajazungumzia serikali inawasaidia vipi hao watanzania kuweza kurudi nyumbani kwa salama?

  Anasema wkamba wako salama kwa sasa lakini hali inabadirika kila siku kule na kama hawatowasaidia haow atanzania kuondoka kule kama nchi zingine, wanaweza kupata matatizo.
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Meanwhile it's being reported that Gaddafi is weighing up his options in terms of which country to flee to for sanctuary. Zimbabwe is emerging as a firm favourite, with London-based Libyan political activist Guma el-Gamaty, telling the Australian ABC news channel that "quite reliable sources" believe Gaddafi is readying to flee his country and heading to Zimbabwe.
  "Gaddafi's own private plane is loaded with gold bullion and lots of hard currency, mainly dollars, and is preparing to flee to Zimbabwe to stay there with his friend Robert Mugabe. We think this could happen very shortly because the (UN) Security Council is threatening to impose a no-fly zone and we think that Gaddafi will try to escape before this no-fly zone is imposed," Guma el-Gamaty said.
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Kweli hao jamaa wanabwabwaja tu.
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Honestly speaking all what Membe tried to convey was totaly nonsense!!

   
Loading...