Mleta mada wewe bado kuchinjwa tu.... maana kama bandani ushaingia mwenyewe
Niliachana nae kwa kashfa tena matusi juu maana alinisaliti baada ya kutembea na muhasibu wa shirika moja akawa ananipiga vijembe ooh mie sasa hivi nipo na mtunza fedha wewe huna shughuli.
Nikaamua kumpotezea ingawa iliniuma sana maana mie maisha yangu yalikuwa ni kuchezea vibuti tu kila siku kipindi icho.
Maisha yameendelea akaanza kutuma sms za mitego mara oohh mwenzio nakukumbuka sana.
Nikawa namchunia ila baadaye nikaanza kuchat nae.Tumeendelea kuchat ananirazimisha tukatiane mie namkatalia coz siwezi kula matapishi yangu ila amekuwa akinihadithia mambo yake mengi na anaombaga nimsaidie.
Mara nyingi ananiomba hela mwezi wa pili nilimtumia laki 1, mwezi wa tatu nikamtumia laki 2 katika vipindi viwili mwezi wa tano huu ameniomba laki 2 tena. Sasa je mimi ni mtu wa aina gani?
Ni mdhaifu au ninampenda huyu mwanamke maana siku hizi akinipigia simu tunaongea masaa mengi tunakumbusha tukicheka na kufurahi i dont know myself na sitaki turudiane kimapenzi.