Waziri alia washindani kutumia computer, hashangai ATCL kuongeza gharama za uendeshaji kwa kuweka kikao cha Baraza la wafanyakazi ATCL.
Yaani pamoja na ATCL Kupewa ndege za buree na ruzuku kibao toka serikalini na abiria wa uhakika kutokana na maelekezo ya serikali kuwa wafanyakazi wa umma waitumie ATCL kama chaguo la kwanza! Bado ATCL wanapiga kelele kuwa hakuna fair competition !
Maneno haya toka kwa Mh. Waziri na pia Mkurugezi Mkuu wa ATCL inaonesha mambo siyo mazuri ktk kupata mapato na shirika mpaka sasa halijajipanga vyema kibiashara ktk ushindani ndani ya soko hili la usafiri wa anga.