Eti ombaomba wanatutia aibu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti ombaomba wanatutia aibu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Omugasi, Jun 21, 2009.

 1. O

  Omugasi Member

  #1
  Jun 21, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi wanasema wanachafua mazingira, kwanza kwa nguo chafuchafu wanazojivika,pili kwa kutupa ovyo masalio mbalimbali kama ya vyakula, 'makopo',mabox n.k
  Wapo wanaowaangalia kama wavivu wanaokimbia kujishughulisha.Watoto wa ombaomba wataishia kuwa kama wazazi wao.Hili kundi pia liko kwenye hatari mbalimbali ikiwemo maambukizi ya magonjwa sugu kama ukimwi, kubakwa na kulawitiwa n.k
  Ombaomba wengi ni wagogo, ukipita mitaa ya by road dodoma utashangaa kuona mabox na railon zilizounganishwa mifano ya vijumba vibovu.
  Lakini hasa tatizo ni nini? umasikini? upofu wa macho ?au?
  Wadau nini kifanyike kwa hawa watu? tuwachangishie michango? itasaidia?

  jitihada za makamba wakati ule hazikuzaa matunda, kandoro mambo yakamshinda, sijui mambo yakoje huko leo! ila manispaa nyingi kama morogoro hata dodoma kwenyewe hawa jamaa wapo tele
   
 2. L

  Limbukeni Senior Member

  #2
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Omba omba yupi huyu anayepanda ndege kila mwisho wa mwezi kwa wahisani au yupi?????!!!!!!!!!!!!
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Unapozungumzia omba omba lazima utumie herufi kubwa......Omba Omba ni tatizo la taifa....achana na wale wanaosimama kwenye mitaa....sasa yule anayekwenda na hazina ya taifa kuomba unamwitaje?
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuna omba omba ambao kweli wanashida na kuna wale matapeli, tatizo ni kujua yupi ni yupi. Ingejulikana wakweli ni wapi hapo ndiyo ingekua mwanzo maana mnajua wangapi wa kuwasaidia na mtawa saidiaje kutokana na matatizo yao halali. Sasa ukichanganya na matapeli huwezi kujua ypi mwenye tatizo halali na yupo tapeli. Na kwa tanzania siyo mambo ya statistics, research and recording mh kaaazi ipo.
   
 5. locust60

  locust60 Senior Member

  #5
  Jun 21, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  WanaFJ suala la ombaomba mitaani si suala kwetu bongo tu hata huku ughaibuni kwa wazee wa feki wapo.Tofauti na kwetu ni hiari ya mtu kusaidia au kutosaidia huku nimeshakumbwa na vituko kazaa vya kulazimisha nitoe chochote.
  Juhudi za kuwaondoa katika miji yetu ya dar,moro zinakuwa ngumu kwasababu hakuna sehemu maalum ya kuwahifadhi ambako wanawe pata huduma muhimu kitu ambacho kinafanya warudi mitaani kuombaomba.Kwa maoni yangu kama wangeanzishiwa makazi pengine wesingerudi tena mtaani.
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Ombaomba kwa kila level wanakera! hasa wale wanofanya kwa kujitakia, ukute mtu ananguvu zake tele lakini kiguu na njia kwenda kuombaomba. Angalia Tanzania, imejaaliwa kila aina za mali asili madini, mbuga za wanayama, kuzungukwa na maziwa makuu kila pande , bahari nk nk. Huu ndiyo uomba omba wa kujitakia!
  Kweli ombaomba ni tatizo la kidunia lakini sisi hapa kwetu halikutakiwa liwe kubwa hivi, na tatizo ni lie lile tumeshindwa kugawa rasilimali kwa angalau uwiano sawa, na kibaya zaidi hata hizo rasilimali hatujui kuwa tunazo au hatujui umuhimu wake, eti tena kila siku na sisi kama taifa tunaombaomba!!
   
Loading...