MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,596
Mbu nafikiri kila kitu kinawezekana ili mradi tu kuwe na makubaliano! Mf kaka wewe unahitaji mtoto mwingine zaidi wakati mwenzako anahisi ameshafika kikomo si kuna kukubaliana na kumake some sacrifices?
Kuhusu kuwa na cheti cha ndoa kusema ukweli nadhani inategemea na tamaduni ya mnakoishi! Hebu nambie pale ambapo tunakubaliana kuishi 'hewani' mpaka uzeeni! Hebu nambie na hizi extended zetu kuna kutambulika pande zote haya bila 'kuhalalisha' mnakuwaje?!
Mwe mie nadhani bado ni wa zama za mawe za kati. Nisaidieni tafadhali
...nikikuoa urafiki wetu utaendelea?
Nimejikuta nacheka kwa nguvu !! Swali gani hili we Mbu! Akhaa!
Labda mie sijakuelewa ni urafiki gani huo unaouongelea? Unamaanisha waliooana wote wamepoteza urafiki wao walokuwa nao kabla hawajaoana?
Yaani hiyo sio issue kabisa, kuna dada ni mke wa mtu, ila yuko tayari kuzaa na jamaa mmoja kwa kuona kuwa jamaa anaweza mzalisha mtoto mzuri.Duh aksante kiraka so hapa nahisi hatojali kama ni mume wa mtu au lah!! mwe!!
Hapa naona naishiwa hoja sijui kwa kuwa umenichekesha?!
Seriously, mimi nafikiri mkiweza kuziidentify zile factors zinazowafanya muwe marafiki na kuzimaintain..... Kuhalalisha umoja wenu kihalali hakutobadilisha kitu.
Kuhalalisha pia kunakufanya mtiu uwe more committed (hata kama utaruka na kuchakura jalalani) unakuwa makini na hakika kuwa unapo pa kueleweka kukilaza kichwa chako! - stable relation.
Lakini pia inakusaidia kuweka limitation eh! Ingawa wanasema kuoa au kuolewa si mwisho wa kupenda lakini inakuwa kama kamba flani ya kukushtua unapotaka kupotoka!
Hahahahahaaaaaaa Mbu bwana wee!
...mwj1,....kwa muono wako...kwanini ndoa nyingi hazidumu miaka hii kama zamani?
swali la ziada,....kwanini wanandoa wengi baada ya kuvuka salama kipindi cha urafiki, na uchumba
kwenye ndoa ile furaha waliyokuwa nayo awali inafifia na kutoweka?...
correct me if am wrong bana, mwenzio nimepitia bad breakups baada ya ndoa niliyodhani tutazikana!
---hapa natafuta mbinu za kufukia mashimo yote kwa ndoa niitarajiayo, nisijetambulikana kama
"mbu yule wa kuoa na kuachwa!"--
Hahahahahaaaaaaa Mbu bwana wee!
Mie sina ninalowezasema juu ya ndoa za siku hizi kusema ukweli but nadhani wengi wetu wa siku hizi tunaingia kwenye ndoa kwa malengo tofauti. Kila mtu anaingia kwenye ndoa akiwa na ndoto zake za alinacha, kuwa anatama mwenz wake awe malaika wakati si rahisi. So kwa wengi hatutake time kufahamiana vizuri, kujifahamu, kumfahamu mwenzi na kujifahamu kama wawili wa pamoja.
Hahaha eti Mbu wa kuoa na kuachwa.............sio unaacha?!