Eti mwalimu wa shule ya msingi haruhusiwi kujiendeleza na fani nyingine?

UZZIMMA

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
414
481
Ni kweli kwamba, ukiwa mwalimu wa shule ya msingi huruhusiwi kujiendeleza na kozi nyengine?

Nina rafiki yangu kamaliza kidato cha nne mwaka jana(2016), matokeo yake ni Phy f, chem c, math D, bio c, kisw b, eng C, geo c, hist b, civ C. (Div2 ya 19).

Lengo lake alitaka asomee Clinical Medicine, ila phys ameharibu.

Hivyo akaona asomee ualimu kisha baadaye anaristi phy kisha anaenda kupiga C.O. Sasa ana wasiwasi aliambiwa kuwa UKIWA MWALIMU SHULE YA MSINGI HURUHUSIWI KUJIENDELEZA NA FANI NYENGINE. Je hio sentensi niloandika kwa herufi kubwa ina ukweli?
 
Haruhusiwi na nani?
Au ni uoga wake tu wa kuogopa kuacha kibarua aende akasome
 
Akiona hafanikiwa kuomba ruhusa akasome ha masomo ja jion,kwa kumsaidia aombe vipind vyake viwe mwisho saa 6 ama 7
 
Siyo tu wa msingi. Hata sekondari hakuna mkurugenzi anayekuruhusu waziwazi uende kusoma kozi isiyo na uhusiano na ualimu. Hata hivyo watu wanakomaa na kozi zingine kibishi.
 
Ni kweli hakuna mkurugenzi anayemruhusu mtumishi wake aende kusomea fani tofauti na ile anayoifanyia kazi, lakini ni kwamba unaongea naye kikubwa au unamdanganya kuwa unaenda kusoma kozi sanjari na kazi yako, sasa jinsi ya kumdanganya ni kwenda chuoni pale unapoenda kusomea kuleta joining instruction na kuipeleka kwa mkurugenzi ili akupe kibali, sasa ile form ya joining unaifoji iseme unaenda kusoma kozi sanjari na uliyoajiriwa nayo, hii ni mbinu rahisi sana pale ambapo hakuna shushu wa kukuchongea kwa mkubwa wako
 
Ukiambiwa peleka matokeo ya kila semester hapo ndo utajuta.
 
Kwani si wanataka matokeo ya mkao mmoja, sijui hapo kwenye kurisiti
 
Back
Top Bottom