'Eti mkewe mbaya...!'

'Eti mkewe mbaya...!'

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,502
Reaction score
6,460
Habari wana JF?

Jamaa na mkewe wamenialika kwao mimi na mheshimiwa mwingine mtaani kwa ajili ya kikao, kikao kilipoanza mwanamke akalalamika kunyanyaswa na jamaa bila sababu zozote za msingi. Jamaa namuuliza vipi anayosema mkeo mpendwa, tena mke halali wa ndoa takatifu yana ukweli wowote? Jamaa akajibu nataka kuachana nae mi simpendi tena!!

Nikauliza tena, kisa cha kutaka kuachana nae ni nini? Jamaa bila soni wala utani akajibu `mwanamke ni mbaya mi simtaki tena`

Nikauliza kwa mara ingine ubaya kwa namna gani hebu fafanua! Akajibu umbo na hata sura we humuoni?

Nikampachika swali la mwisho, ulipomuoa alikuwa vipi na kipi kilikuvutia ambacho sasa hana? Nikajibiwa zamani alikuwa mzuri sana na picha za binti kabla ya kuolewa na jamaa na siku za mwanzo za ndoa yao nikaziona kweli binti alikuwa mrembo hasa!!

Nikasema `sasa jirani kwa ufupi twende haki kwa haki, si mnataka tufanye haki hapa?` Wote kwa pamoja wakajibu `ndiyo!

Nikasema tena `Jirani nimeona ni kweli ulioa binti mrembo toka kwa wazazi wake ila ni wazi kabisa kaja kukongorokea kwako then unataka umuache! unadhani ni jambo la kiuanaume hilo?` Baada tu ya kusema hivyo nilishtukia jamaa kanirukia na kuanza kuvurumisha migumi kama mvua!! Yaani kama si mambo ya kushindia gym kila jioni leo ningechakaa maana nashukuru niliweza kumdhibiti hakuna ngumi hata moja iliyofikia uso wangu.

Kwa mtiririko huo unahisi kosa langu ni lipi? Sikuwaita wamejileta wenyewe kwa kuheshimu jinsi wanionanvyo!!

NB:Jamaa kapiga simu kuomba tuonane tena kwa kikao kingine nikamjibu tukakalie kituo cha polisi ndo tutakuwa salama zaidi but kaomba samahani kwa vurugu zilizojitokeza
 
Mwambie umemsamehe ila mpaka akubali umchape at least viboko vinne vya kurudishia ngumi alizokutupia.
 
kaka unamoyo...
kwa ufupi huna kosa, ila jamaa ailitaka kukimbia majukumu...!
 
Habari wana JF??

Jamaa na mkewe wamenialika kwao mimi na mheshimiwa mwingine mtaani kwa ajili ya kikao, kikao kilipoanza mwanamke akalalamika kunyanyaswa na jamaa bila sababu zozote za msingi. Jamaa namuuliza vipi anayosema mkeo mpendwa, tena mke halali wa ndoa takatifu yana ukweli wowote? Jamaa akajibu nataka kuachana nae mi simpendi tena!!

Nikauliza tena, kisa cha kutaka kuachana nae ni nini?? Jamaa bila soni wala utani akajibu `mwanamke ni mbaya mi simtaki tena`

Nikauliza kwa mara ingine ubaya kwa namna gani hebu fafanua! Akajibu umbo na hata sura we humuoni??

Nikampachika swali la mwisho, ulipomuoa alikuwa vipi na kipi kilikuvutia ambacho sasa hana?? Nikajibiwa zamani alikuwa mzuri sana na picha za binti kabla ya kuolewa na jamaa na siku za mwanzo za ndoa yao nikaziona kweli binti alikuwa mrembo hasa!!

Nikasema `sasa jirani kwa ufupi twende haki kwa haki, si mnataka tufanye haki hapa?` Wote kwa pamoja wakajibu `ndiyo!!`

Nikasema tena `Jirani nimeona ni kweli ulioa binti mrembo toka kwa wazazi wake ila ni wazi kabisa kaja kukongorokea kwako then unataka umuache! unadhani ni jambo la kiuanaume hilo?` Baada tu ya kusema hivyo nilishtukia jamaa kanirukia na kuanza kuvurumisha migumi kama mvua!! Yaani kama si mambo ya kushindia gym kila jioni leo ningechakaa maana nashukuru niliweza kumdhibiti hakuna ngumi hata moja iliyofikia uso wangu.

Kwa mtiririko huo unahisi kosa langu ni lipi?? Sikuwaita wamejileta wenyewe kwa kuheshimu jinsi wanionanvyo!!

NB:Jamaa kapiga simu kuomba tuonane tena kwa kikao kingine nikamjibu tukakalie kituo cha polisi ndo tutakuwa salama zaidi but kaomba samahani kwa vurugu zilizojitokeza
Huwa wanawake wanapendeza zaidi wakiolewa,ukiona mtu anachakaa baada ya kuolewa ujue jamaa anamfrastrate mama na matunzo sifuri
 
kaka unamoyo...
kwa ufupi huna kosa, ila jamaa ailitaka kukimbia majukumu...!

Kaka mambo ya kusikia haya mabaya sana, jamaa aliambiwa mke akiwa mzuri sana atakusumbua!! So, akaamua amchoshe kidizaini but bahati mbaya akajikuta na yeye anamchoka baada ya mwanamke kuwa mbaya/kuchoka zaidi.

Tumeyasolve, tunakunywa bia pamoja na maisha yao yameanza kuwa ya furaha tena.
 
Mwambie umemsamehe ila mpaka akubali umchape at least viboko vinne vya kurudishia ngumi alizokutupia.

Hahahaaa!! Sisi binadamu bana huwezi jua alikwazika na nini zaidi ya hapo ni majirani!! Tuko sawa mkuu
 
Huwa wanawake wanapendeza zaidi wakiolewa,ukiona mtu anachakaa baada ya kuolewa ujue jamaa anamfrastrate mama na matunzo sifuri

Exactly, na mwanaume kamilifu ni yule anayerudi nyumbani na kukuta familia yake ina furaha, imenona/wana afya na wanakupenda wanafamilia wote.
 
Pole kwa yaliyokukuta, kwa kweli wewe huna kosa lolote

Binadamu tunabadilika kila umri unaposogea sasa yeye alitegemea mkewe abaki alivyo tangu/kama siku ya kwanza walipokutana
 
pole kwa yaliyo kukuta .kama wamekuita ili uwapatanishe kwa mara ya pili kuwa makini .
 
Wanaume, wanaume!!!! shikamoooni wanaume! Ndo maana naiogopa sana ndoa!
 
Wanaume, wanaume!!!! shikamoooni wanaume! Ndo maana naiogopa sana ndoa!

Changamoto haikimbiwi, bali unaikabili!! Usiogope ndoa, yupo mwanaume wa kukufanya uishi maisha mazuri na yupo mwanaume kwa ajili kukutumia atakavyo!! Choice ni muhimu sana mdada, we unapenda wanaovaa kata k akuoe???
 
Ningekuwa wewe ningecheka sana hadi jamaa anikodie majambazi
 
Akikuita tena na km bado analengo la kumuacha we mwambie utamchukua we we utamaliza tatizo dk 2 tu
 
pole sana mkuu kwa makonde na hongera kwa uamuzi wako wa kufanyia polisi lol. Wanaume wanaona binti mrembo akiwa kwao akishawekwa ndani hata matunzo ni shida. Mwanamke matunzo jamani, ukimtunza atakuwa zaid ya queen kila siku
 
"Mtumee, kakataa kumtambulisha mke wake kisa ana figure ya kiumeee" - TMK Wanaume Family
 
Back
Top Bottom