Eti Million 10! kwa wamachinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Million 10! kwa wamachinga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hassan J. Mosoka, Feb 7, 2012.

 1. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana Jamvi!
  Nimeshangazwa sana na habari kuwa Rais wa nchi amekutana na wamachinga wa Mwanza na kuwapa Tsh.10 ili kuongeza kwenye mitaji yao. Rais amenifanya nijiulize kama anatazuguka nchi nzima kuwagawiwa wamachinga wa kila mkoa Tsh.10 kama njia ya kuwakwamua.
  Sikuamini wala sitaamini kuwa hizo fedha zimetolewa na rais wa nchi kwa utashi wake, nadhani hapa mkuu kaingizwa chaka kama ilivyo ada. Kitendo alichofanya rais hakina tofauti na vitendo vinavyofanywa na nchi tajiri kwa nchi maskini kuwapa fedha za misaada kwa miradi isiyo na tija ili kesho tena warudi aitha kuomba au kukopa. Nilitarajia Rais kama taasisi ya juu kabisa katika mfumo wa utawala wa nchi yetu angeboresha zaidi mazingira ya small firms wakiwemo wamachinga uwezo wa kushindana kwenye soko huria, mazingira yatakayopunguza kama sio kuondoa kabisa mapambano na maaskari wa majiji, kuwahakikishia usalama wa kazi na mali zao kujenga uwezo wa miundo mbinu itakayowainua watu hawa kutoka kutembea toka Nyegezi hadi airport na kurudi kwa siku, mbezi mpaka gongolamboto, ngaramtoni to Usa river nk, nk. Rais wa nchi, katika mambo muhimu kama hili la kupambana na umaskini awe anaacha mizaha ya kutoa hela kama vile unachangia harusi. Wakati umefika watu wawambie watawala kuwa mizaha imetosha na tunataka kusonga mbele.
  Nawasilisha
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  utani mpaka ikulu?
  nchi ipo rehani.
   
Loading...