Eti… kuna sumu ya mapenzi…!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti… kuna sumu ya mapenzi…!?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fidel80, Aug 27, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Sumu ya mapenzi jamani ni…

  1. Ni maudhi…
  Uliza watakwambia, hakuna kitu kinachoporomosha penda kama maudhi ya kila kukicha, na hii inakuwa sababu kuu ya kwanza kuliko zote ambazo nitazitaja hapo chini. Kila kukicha kuna hiki, mara kile mara hiki.

  Mwisho wa siku Pendo huota mbawa bibi upo hapo. Basi kama kuna cha kuepuka cha kwanza hiki hapa. Epuka kugeuka kuwa kero.

  2. Sumu ya mapenzi ni Ufitini…
  Anayekuja kukwambia mumeo hivi jua kakubebea kichupa cha sumu amekuja nacho ukimalize. Najua hii wengi mtachukulia tofauti, lakini ukweli unabaki pale pale, fitina siku zote hana jema katika mapenzi yenu, tena mkishamjua mchemshieni maji ya moto mmumwagie (Natania).

  Tukiweka utani mbali mambo ambayo huua mapenzi ya watu ni watu ambao hawapendi kuiona meli yenu ya mapenzi baharini. Chukua hiyo.

  3. Sumu ya mapenzi ni usaliti…
  Hiki ni kidonda shosti, tenda donda sugu katika mapenzi, na hata kikipona basi kovu lake huwa kubwa pengine kuliko hata kovu la jeraha la panga. Hakuna anayejua maumivu ya usaliti isipikuwa yule uliyemfika.

  Na katika mapenzi imani ikipotea basi kuirejesha itakugharimu zaidi ya mapenzi. Nauliza chai ikiingia chumvi itaitwa chai au itageuka kuwa supu. Nadhani mpaka hapa ushajua kuwa hii nayo ni sumu kali zaidi ya chatu.

  4. Sumu ya mapenzi ni Gubu…
  Mwanamke mwenye gubu kwa maana nyingine hujulikana kama mwanamke mwenye nongwa, mwanamke dizaini hii kuwa kwake la kheri nongwa la shari nongwa.

  Nazungumzia hulka ile ya kuwa msununu kwako jema halijulikani wala baya halijulikani. Mwanamke huyu ni Yule aliyetaja katika bibilia kuwa huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.

  5. Sumu ya mapenzi ni Uchafu na Uvivu wako… Hivi vitu viwili ni baba moja na mama mmoja. Ukiwa mvivu bila shaka utakuwa mchafu, na ukiwa umchafu unasababu nyingine ya kwanini unakiwambiwa. Mwanamke usafi bibi asikudanganye mtu. Kifupi na hayo tu.
  By Asma

   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Yaani ukizingatia hayo dada basi umemaliza kila kitu.
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hiyo namba tatu ndo sumu kali kuliko zote kwenye mapenzi
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Fidel umesomeka ndugu yangu....
  1.Haya ni mambo ya kawaida sana kusemwa kama ngonjera..ila kwa vile na wewe umeinukuu hukooo unakojua siwezi kuanzisha mdahalo....

  2.Ningependa labda kuongezea kuwa hizo kero ni msumeno ukatao kotekote...bila kujali mtenda ni mwanamke na mtendewa ni mwanaume.Hakuna binaadamu apendae maudhi, gubu, fitina, usaliti,uchafu wala uvivu.Sote tunapenda raha na hatupendi karaha.
  kwa kifupi ni kwamba ...ili penzi lishamiri inabidi kufuata the golden rule:
  DO UNTO OTHERS WHAT YOU WOULD LIKE THEM TO DO TO YOU....
  USIMTENDEE MWENZIO LILE AMBALO WEWE LITAKUUMIZA.

  3.Binadamu kwa ubinafsi tuliokuwa nao mara zote atataka yeye tu ndio atendewe mema ilhali yeye yu mwepesi kumtendea mwenzake yaleyale asiyopenda kutendewa.Ni mpaka hapo watu watakapojaaliwa kuwa na moyo usio wa ubinafsi ndipo kutakuwa na mapenzi ya kweli yasio na chungu ya aina yeyote ile.Kama hili linawezekana ama la SIWEZI KUJIBU kwa maana inahitaji mtu mkamilifu 100%.Kama yupo binadamu wa aina hiyo tufahamishwe ili tumtumie kama role model wa "YES IT IS POSSIBLE CAMPAIGN!"
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Unajua dada WOS umepotea sana sijui mzee amekuchimba mkwala usiingie JF tunakumiss dada michango yako ni muhimu sana akina Nyamaya,MJ1,Agika,Chaku wanasubili sana nashukuru kwa comment.
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante sana Fidel leo of all the days umenifurahisha. Umesomeka vilivyo sina cha kuongeza ila tu hapo kwenye gubu sina la kusema maana mh
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  WOS kamaliza yote, hayo mengine unaweza vumilia kidogo lakini kwangu mie inapofikia swala la usaliti nachoka kabisaaa....
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  kuna watu wana gubu balaa, nina frnd wangu anakoma na huyo mr wake....
   
 9. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2009
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  jamani tena ukikutana na mwanaume mwenye Gubu ,ndio hatari,unless uwe na Yesu moyoni
   
  Last edited: Aug 27, 2009
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama ulikuwepo Fidel! Umejuaje?
  Kidding Lol.Ni majukumu tu ..usipoangalia utaua familia kwa kuganda JF bila kufanya kitu kingine.Nimewamiss wote wa jukwaa hili muhimu!
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Uombe usikie tu kwa watu ukiwa naye wewe mbona utajuta! Maana akilianzisha ukaamua kumjibu kosa, ukimkalia kimya kosa yaani ilimradi ngoma inachezeshwa tu
   
 12. GP

  GP JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  WIVU
  wivu nao mkuu ni sumu mbaya, ongezea hapo,
  usichukue uamuzi wa ghafla pasipo kufanya uchunguzi, umeona mkeo/mumeo kasimama na mtu huulizi unaanza kuwaka, labda ndugu yake je?

  UBINAFSI
  usijipende wewe mwenyewe, show love kwa mwenzako bana hata kama anakipato kikubwa au kidogo.
  kingine kwenye malovedavee mpe raha mwenzako nae akupe!!, sio watu mko kama magogo raha unajipa mwenyewe tu, ala.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Sasa nini dawa yake hapo kama vyote ngoma droo.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hehehehe haya shukrani lakini nafrahi kama iwa unakuja kuchungulia na kuondoka
   
 15. a

  agika JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Well said dada!..... yaani umenifumba mdomo vibaya mno maana nilishaanzakuandika na macho kabla ya vidole fidel anapotuelekezea shutma sie wanawake tu wakati na wao wanaume wanazo hizo tabia hapo zooote na zaidi na hilo gubu ndo usiombe , yeee mwenyewe hapa jamvini ana gubu ile mbaya sembuse huyo mwenza wake (MWJ1) mtarajiwa sijui itakuwaje.
  but all in all haya mambo yanavuruga mahusiano mengi , mmoja wapo akiwa na moja kati yaliyotajwa hapo juuu, msione watu mapenzi yao yana miaka 20 jamani wanavumiliana tuuuuu huo 100% kama anaosema dada WOS ni adimu , unachofanya kumvumiliaa tu menzio ilimradi maudhi hayavuki mpaka
   
 16. a

  agika JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mhhhh weee nawe? akuuu nikapike ftari mie nisiharibu saum yangu
   
 17. a

  agika JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Usaliti mamiii unaona si mchezo , bora hayo mengine unaweza umwache abwatuke mwenyewe lakini usaliti huna jinsi ya kukimbia maumivu .Mungu atunusuru
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Usaliti nafikiri unakuja pindi mtu amekuoa/kuolewa kwa kulazimishwa na hakuwa na namna anaamua kudondokea kwenye ndoa ambayo hakutarajia matokeo yake ndo haya sasa mnaanza kusalitiana.
   
 19. a

  agika JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  weeee fidel weeee temea mate chini kaka, usaliti haujalishi kama mwanzo mlikuwa mnapendana au vipi ni shetani tu anapoamua kufanya kazi yake kuwaingilia wenye ndoa, ukitaka kujua ukweli weee tafuta unayempenda na kuamini na wewe anakupenda atleast utakuwa sured kwa upande wako halafu talk to me baada ya miaka miwili ya ndoa, tena nyie wanaume ndio kwenye hili hamna muamana kabisaaa hata mtu kama MWJ anapojikusulu kukupa mapenzi yote lakini bado utamsaliti, sababu za usaliti ziko nyingi tena complex inategemeana tu na mazingira waliyopo wanandoa wale.
  kesho tutajadili zaidi saa hizi naenda kupika ftari. na hassa nataka kuongelea lile la usafi maana japo linatuhusu wote mwanamke na mwanamme anaeplay big part ni mwanamke.
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ama kweli u care my sistah!
  Wanaume mwezi mtukufu mnawapa special treat wake zenu kwa kuwajali au? Haya ndio mapenzi ya dhati eti asikudanganye mtu.
   
Loading...