Wanaume wabaya sana, hapo utakuta kukutana na mvulana kwenye mitandao ya kijamii baada ya maongezi jamaa anaanza kuomba picha ya bidada. Utasikia piga picha ukiwa unaoga nitumie.... mara piga picha kwa nyuma ukiwa umejaa kaptura unitumie sasa mdada wa watu selfie ya nyuma hawezi kuipiga. Kapata shosti kampiga picha kaituma kwa bae wake...... ona sasa....
Bae anaianika picha ya mdada mitandaoni na ona watu wanavyomchambua kama karanga wengine wakifanya matani na masihara wengine wakiburudika ili mradi kila mtu na lake.
Ila bidada akiiona hii picha yake mitandaoni inavozagaa ataumia mnoo na hatafurahia watu wanavomnanga hapa. Hata kama hawamjui yumkini si mtanzania lakini kwa namna moja ama nyingine anaweza kuwa na ndugu yake au rafiki akaiona picha hii ikawa fedheha zaidi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.