Shukuru
JF-Expert Member
- Sep 3, 2007
- 747
- 16
Nilikuwa na mpenzi wangu kipingi cha nyuma, na tulifikia kuamua kufunga ndoa na nilikuwa katika mipango ya kupeleka posa ila tuliachana kwa sababu fulani fulani, nilijaribu kuurudisha uhusianai karibu mara tatu, ila naona kama siwezi kuwa na huyu mtu tena ila tatizo ni kuwa kwa nini kila ninapopata rafiki mwingine tukiwa pamoja japo kwa mazungumzo tu huwa najiwa na mawazo sana juu ya huyu wa mwanzo na najikuta na-conclude kuwa huyu mtu "wa sasa" hanifai, na hii ni kama mara tatu inanitokea yaaani kwa watu watatu tofauti tofauti imenitokea; sasa ni kwa nini hii memory inatokea na mara nyingi huanza na jina lake kisha husema irreplaceable niambieni ninyi wata'alam wa huu ukumbi au mi bwege? then nifanyeje?