Eti hapa haki yangu ni ipi?

eity 4

Senior Member
Dec 7, 2014
148
209
Baba yangu alimuoa mama yangu kwa ndoa ya kikristo( roman Catholic) baada ya kuzaliwa mimi baba akamuacha mama kwao(kwa kina baba) akaenda chuo ambako alikutana na mama yangu wa kambo aliyezaa naye watoto watano, then wakaachana akamchukua mama mwingine waliyezaa naye watoto wawili. Mimi nimelelewa na mama miaka 7 mingine yote nimekaa na baba sasa hivi MTU mzima. Sasa baba yangu amefariki na hakuna wosia. Baba kaacha nyumba mbili.
Ni nani mrithi halali na mgao unakuwaje?
 
kwanza unaweza ukaomba usimamizi wa mirathi katika mahakama ya mwanzo kwa niaba ya ukoo wako kama wataona inafaa.. baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ndio issue za kugawana mali zitafuata kwa kuzingatia pia utambuzi (kuhalalishwa) kwa hao watoto wa nje ya ndoa kulingana na taratibu za jamii au ukoo wenu..

kwa upande wa pili, who ever atakayechaguliwa kuwa msimamizi wa mirathi..basi lazima katika ugawaji wa mali azingatie swala kuwa wewe ni mtoto halali wa ndoa ya kikristu na maisha yenu yalikuwa kikristu. hivyo ugawaji wa mali utatumia sheria ya Indian Succession Act..

I stand to be corrected
 
Mkuu kama mali haukuhusishwa nayo Baba yako alivyokuwa hai usiichukue. Wala kuing 'ang'ania achana nayo maana itakuharibia sawa we kazana na mambo yako ipo siku utatoka.
 
Ninachomaanisha hata kama ungekuwa wewe na baba yako na mama yako tu ndo familia pekee usiing'ang'anie mali maana haukufundwa jinsi ya kuimanage labda Mama kwa kiasi fulani ana huo uwezo mara nyingi utajiri wa mali za kurithi haudumu kaka kwa sababu hii. Mali zinarithishwa kwa watu ambao hawajui kuzitunza na kuziendeleza.
 
Wewe ni mtoto halali wa ndani ya ndoa mpaka hapo maana ndoa kati ya baba yako na mama yako haijavunjwa! Kwa kuwa wewe ni mkristo ni vyema sheria India zikatumika una haki katika huo urithi!
 
Sheria inayoendesha masuala ya mirathi kwa wakristo ni sheria ya mirathi (India ) ya mwaka 1865...

Ambapo wewe kama mtoto wa una haki ya kurithi hata kama baba yako amefariki bila kuacha wosia, sheria ya mtoto ya mwaka 2009 na yenyewe inampa haki hata mtoto wa nje ya ndoa kurithi.

Hivyo basi tambua haki yako ya kurithi haijapotea hata kama mzazi wako amefariki bila kuacha wosia..
 
Na mke vipi ana haki km hakuna wosia
 
Baba yangu alimuoa mama yangu kwa ndoa ya kikristo( roman Catholic) baada ya kuzaliwa mimi baba akamuacha mama kwao(kwa kina baba) akaenda chuo ambako alikutana na mama yangu wa kambo aliyezaa naye watoto watano, then wakaachana akamchukua mama mwingine waliyezaa naye watoto wawili. Mimi nimelelewa na mama miaka 7 mingine yote nimekaa na baba sasa hivi MTU mzima. Sasa baba yangu amefariki na hakuna wosia. Baba kaacha nyumba mbili.
Ni nani mrithi halali na mgao unakuwaje?
Haki yako ipo, no wewe tu uende kwa wakili
 
Unawaza urithi wakati mshua amepata nafuu.. Huendi mbinguni, ndiyo ushafail hvyo!
 
Baba yangu alimuoa mama yangu kwa ndoa ya kikristo( roman Catholic) baada ya kuzaliwa mimi baba akamuacha mama kwao(kwa kina baba) akaenda chuo ambako alikutana na mama yangu wa kambo aliyezaa naye watoto watano, then wakaachana akamchukua mama mwingine waliyezaa naye watoto wawili. Mimi nimelelewa na mama miaka 7 mingine yote nimekaa na baba sasa hivi MTU mzima. Sasa baba yangu amefariki na hakuna wosia. Baba kaacha nyumba mbili.
Ni nani mrithi halali na mgao unakuwaje?
Inawezekana wewe ndo unahaki kisheria ikiwa baba yako hakufunga ndoa na huyo mama mwingine.Kwa sheria ya ndoa na sheria ya urithi ,mtoto wa nje ya ndoa kama hajarithishwa na baba aliyekufa intestate hana haki ya kurithi.
 
Back
Top Bottom