Eti bora vita kuliko udhalimu wa CCM

Eti bora vita kuliko udhalimu wa CCM

Kwa mfano tukisema tuchapane tutachapana baina ya nani na nani?

Tuanzie hapo

Baina ya viongozi wa CCM na upinzani. Maana ndo wanaotuibia. Wananchi tutakuwa tunafuata CCM walipo na kuwachapa
 
wakati huo wao washasafirisha familia zao nje ya nchi, mnaoshabikia vita wote hawajielewi, huko burundi tu hata mwezi haujaisha tayari watu zaidi ya laki moja wamekimbilia tz, haya semeni mnataka tuwe kama syria, sudan , burundi? chagueni
 
aisee hicho kichwa cha habari kilinishtua sana 'eti bora vita kuliko utawala wa ccm' nilikasema duu kweli wewe hata taarifa za habari huwa hauangalii.

Kwa ukweli vita za wenyewe kwa wenyewe hazifai hata kidogo mfano mzuri ni siera lione, liberia, sudan, rwanda na jirani zake, afrika ya magharibi na kwingineko duniani.

Yaani nawaomba watanzania wenzangu chonde chonde tusikubali kuingiza nchi yetu kwenye janga la vita ya wenyewe kwa wenyewe

Kwani haujui kuwa ufisadi ni sawa na vita tena zaidi sema inaua indirect na slowly, hata zaidi ya Ebola kaka
 
Ndugu zetu wangapi wamekufa kwa kukosa dawa?wangapi wamekufa kwa vipigo vya polisi?
Tayari vita ipo ila ni ya watawala dhidi ya wanyonge
 
Baina ya viongozi wa CCM na upinzani. Maana ndo wanaotuibia. Wananchi tutakuwa tunafuata CCM walipo na kuwachapa

Hapo tunajidanganya, vita nimeziona sana.

Kiukweli vita ikianza wengi wataogopa kutoka makwao na watakaotoka ni kuvunja maduka na kuiba vyakula na chochote watachokiona hutakumbuka chama wala serikali ila TUMBO lako tu

Utakwepa risasi huku unakimbia na mfuko wa unga kuwahisha watoto wale.
Tuombe amani, vita naijua vizuri, mpaka iishe watu watakuwa wameisha sana na kuanza upya ni kazi ngumu maana kila ataeshika madaraka itakuwa vitisho kwake kuwa TUTAANZA TENA OOHOOO
 
Kwahyo unasema tuwape tena ccm awamu nyingine ya kutugaragaza? We na magufuli mna akili sawa za kulinganisha upinzani na vita.
 
Mazombie ni wapuuzi sana. Eti mimi sio ccm wala sio chadema lakini chagua ccm ndiyo bora. Huu upunguani wa kusema huna chama halafu unatuambia bora ccm unamdanganya nani. Ndiyo kama yale mabunge yao yanasema naunga hoja 100% lakini jimbo langu lina tatizo hili na hili...... Upumbavu mtupu.
 
Kabla ya yote mimi sio CCM wala CDM,ila ninakereka sana na wajinga kadhaa wanaosema ni bora nchi iende vitani kuliko kuendelea na utawala "dhalimu" wa CCM,mimi napingana nao ingawa ndio CCM imefanya machafu mengi sana kuanzia EPA,Richmond, Meremeta.Escrow, Radar na mengine kibao.

Hao watu wanaijua vita lakini?vita vya wenyewe kwa wenyewe wanavijua? Kwanza kama walikua na mipango yao ya kimaendeleo yote inabidi waifute na waanze kuishi kama ndege achilia mbali vifo vya uwapendao na mara nyingi nchi ikishaingia kwenye civil wars pia mataifa makubwa yanajipenyeza kuchochea pande flani ili wajinufaishe kama Prof Kalamaganda(yule wa law aliekua kwenye tume ya warioba) alivosema kua nchi pekee yenye utajiri inayongojewa iende vitani mabeberu waje wajichumie ni Tanzania.
Ni bora CCM waendelee kuliko kuingia vitani.

Maviiii yako!! Kwa garama zozote zile ccm hatuitaki
 
Utakua ni mpumbavu wa hali ya juu kupigana na kuuana kwa ajili ya lowassa na magufuli. Ukisikia mtu anasema bora vita basi huyo atakua nyaru au mcongomani.
 
Hii naona sio viroba ni ile iliouwa watu kenya mmekunya wote mnaosema bora vita ni bora kukosa mali upate elimu
 
Mnaongea kuhusu nini? Amani? Mh!
MAPIGANOARUSHA_CHADEMA8.JPG
 
Back
Top Bottom