Ethiopia: Msiba Wageuka Kuwa Sherehe

Ethiopia: Msiba Wageuka Kuwa Sherehe

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,067
Wanakijiji wa kijiji kimoja nchini Ethiopia washeherekea kufufuka kwa mwanaume mmoja ambaye alidhaniwa kuwa amekufa.

1543162230695.png


Hirpha Negero, ambaye ni baba wa watoto watano alitangazwa kuwa amefariki siku ya jumanne majira ya saa nne na nusu.

Kulingana tamaduni zao katika vijiji vya pembezoni mwa miji vilivyopo Sibu Sire na mkoa wa Oromia,bunduki ilipigwa mara mbili na hiyo ni ishara kuwa kuna mtu amefariki hivyo watu wanaitwa kuhudhuria katika msiba.

Ndani ya saa moja, mwanakijiji mmoja kwa jina la Etana Kena alimuweka kwenye jeneza tayari kwa mazishi. Ingawa wakati wa mazishi katika majira ya saa tisa na nusu, walisikia mtu akigonga kutoka katika jeneza.

''Watu walishangaa na huku wengine wakikimbia na hata sikupata mtu wa kunisaidia," bwana Etana alieleza namna alivyohitaji msaada ili aweze kulifungua jeneza.

Mtu aliyefufuka aliiambia BBC jinsi alivyojisikia akiwa ndani ya jeneza: "Nilisikia sauti ya mtu akilia. Nlikuwa sina nguvu kabisa na hata sikuweza kuongea." Lakini badaye aliweza kuanza kuita.

Baada ya mshtuko ambao uliwapata wengi katika msiba, mazishi yaligeuka kuwa sherehe. Hirpha alieleza kuwa alishawahi kuzika maiti zaidi ya 50 lakini hakuwahi kukutana na tukio kama hilo.

Chanzo: BBC
 
Hii hasa kwa waislam wanazika watu hai!
Bora wakristo tunakaa hadi siku 3 pengine anaweza kurupuka endapo alizimia!
 
That's called near death experience. Mtu anakuwa hajafa kabisa bali mapigo yake ya moyo na flow of blood vinakuwa chini sana kufikia hatua it is hard to detect them.
Kwa Africa tumeshazika watu wengi sana wakiwa hai alafu wanafia huko huko chini ya ardhi kwakukosa oxygen.
Wamshukuru Mungu walichelewa kwenda kuzika
 
That's called near death experience. Mtu anakuwa hajafa kabisa bali mapigo yake ya moyo na flow of blood vinakuwa chini sana kufikia hatua it is hard to detect them.
Kwa Africa tumeshazika watu wengi sana wakiwa hai alafu wanafia huko huko chini ya ardhi kwakukosa oxygen.
Wamshukuru Mungu walichelewa kwenda kuzika
Daah so sad
 
Back
Top Bottom