Ethical hacking must be legal?

Kaliro X

JF-Expert Member
Apr 18, 2013
749
440
Unajua tunapozungumzia hacking (udukuzi) ziko katika namna mbili tofaut.
Aina ya kwanza ni udukuzi usio na madhara au ethical hacking hii hufanyika kwa malengo mazuri mfn kujifunza, kuboresha mifumo ya usalama katika databases zako n.k.

Hii kwa wenzetu walioendelea kama Wamarekani ni kitu cha kawaida sana kwao lkn tukija katika aina ya pili ambayo udukuzi wa uharibifu, hii iko illegal na kwa hapa Tza kuna sheria imepitishwa na bunge hivi karibuni kuratbu shughuri za kimtandao mfn ukishtakiwa na kuthibitika kuwa umeingilia mawasiliano ya siri ya mtu pasipo ridhaa yake kuna adhabu ipo kwa mujibu wa sheria.. Anyways sitaki kujudge sana katika hilohilo.

Lakn ninachokiona mm kuwa ni cha ajabu na kinachosikitisha ni kwamba hapa kwetu hii sheria iliyopewa jina "Sheria za makosa ya kimtandao"
Iko very harsh

Tofaut na ilivyo kwenye nchi za wenzetu serikali na mamlaka husika hawataki kuzitambua hata hizi 'white hat hacking' ambazo kimsingi zina lengo la kupanua uwezo wa kibunifu kwa wataalamu mbalimbali..

Ningependa kusikikia maoni yenu wadau katk hili.. Uwanja uko wazi kwa majadiliano
 
Kuingilia mawasiliano ya mtu sio ethical hacking, kwenye ethical hacking lazima uwe na idhini ya mwenye system unayojaribu kuihack.

Hii inafanywa sana sana na makampuni yanayotaka mtu afanye audit ya IT security yao ikoje.
 
Kuna habari nilisoma kuhusu hacker mmoja wa Anonymous alihack na kuachia information za watu walio husika na ubakaji wa mwanamke katika shule moja huko Marekani lakini mwisho wa siku huyo hacker akakamatwa na kufungwa sasa nielezee hizo "Nchi za wenzetu" zenye sheria za mtandao bora vipi kwenye hilo?

Google search: "Anonymous Hacker Who Exposed the Steubenville Rapist"

Hiyo ethical hacking hata bongo ipo mfano tigo leo wakitangaza bounty ya million 10 kwa yoyote hata kaeweza ku infiltrate their tigo pesa system au website yao hamna kifungu cha cyber crime kitakacho zuia hii.. Maana sio "unauthorized entry tena".

Naomba kabla ya ku judge cyber crimes law ya Tz kasome ya USA, Britain, South Korea, Germany, Russia, China, Japan "aka Nchi zilizoendelea" ndio urudi hapa maana nakuona kama vile tuko kijiweni na ile "Nchi za wenzetu haiko hivi" Mentality wakati sheria za hizo Nchi hata kuzisoma hamjawahi.
 
Back
Top Bottom