ESTIM Construction ni kampuni ya nchi gani?

Kuna kampuni ilikuwa inaitwa KOJIFA. Ilikuwa ni kampuni ya kiitaliano ilijenga bara bara Mwaka 1996 kutoka Sirari wilaya ya Tarime mpaka Makutano wilaya ya Musoma, ile kampuni ilikuwa inajenga bara bara zenye ubora wa kiwango cha hali ya juu, mpaka leo hii ile bara bara ni imara. Kwangu Mimi ile ndo kampuni bora.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ohooo tayari usharambishwa asali kwa kidole cha kati

Haya tumekusikia ila mwambie aliekutuma kwamba kampuni za ujenzi zina mamna ya kutathmini ubora wake na sio kuangalia kwa macho yako halafu unapitisha wapewe !!!

Nafkiri Ma'engineer na wadau wa barabara huwa hawatumii utaratibu wa kuangalia kwa macho na kupitisha kwamba APEWE !!! kuna vigezo vingi wanaangalia Ndg. Yangu Tabutupu Wakuvanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama na akili mbovu niambie mradi wowote ambao walau umelalamikiwa kwamba umejengwa chini ya kiwango.


Hata kampuni yako ingefanya vizuri ningefanya the same.

Kuna makapuni kibao yanachoma kodi za wananchi. Gullam,
Mwanzoni niliamini ni mtu anayetaka tu kujua hii kampuni, ila kwa comment hii, wewe ni sehemu ya hiyo kampuni na ulikuwa unafanya matangazo hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wame secure tena Tender ya Kujenga Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, Tambuka Reli Dodoma
Kama Mkandarasi Mkuu
 
Ipewe barabara zote za tz tuachane na hawa watching
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…