ESTIM Construction ni kampuni ya nchi gani?

Kwa theory za darasani wabongo tupo vizuri, akabidhiwe sasa hata kilometer 1 uone, nenda Alaf kiwanda cha mabati kaangali kampuni ya mswahili mwenzetu huu mwaka wa 3 km 2 hazifiki. Ndio maana nahisi huyo mtoa mada ameshangaa ubora wa Estim, kuongezea hata Nyanza Construction wapo vizuri na ni mtanzania mwenye asili ya India, sisi kwenye barabara zero, miradi ya maji zero, huko REA mpaka wakandarasi wawekwe lock up. Wenzetu wamebadilika kulingana na awamu ili wapate riziki ( Less cost, High Quality, less delivery time) ukifeli hayo njaa inakuhusu. Mbona Songoro Marine anajenga almost meli na vivuko vyote kilichombeba ni hayo na kuajiri technical team qualified toka nje.
 
Tatizo la kujenga miundombinu mibovu na isiyokuwa ya kiwango linaanzia kwenye tenda, ili ushinde tenda na kupewa kazi mnakaa mezani kwanza, mzabuni anaweka cost zote kukidhi viwango kutokana na TOR, anasema itagharimu 300bil, afu jamaa wanamwambia ili tukupe kazi 150bil ni zetu. Kwa kuwa mzabuni hataki kukosa kazi, anakubali anajibana na kutoa kitu kisicho na ubora kuhofia kukosa kazi siku za mbele.

Kuna co. Inajenga barabara kutoka sinza kijiweni kwenda tandale, kutoka tip top Hadi mtogole, anajenga mifereji kwa kwa zege na nondo zilizosukwa kwa uhakika. Akatokea mkuu mmoja kukagua akasema barabara zinajengwa kwa ghalama kubwa km chache. Hapo engeneer si itabidi aachane na viwango akidhi quantity? Siasa na rushwa ndivyo vinajenga barabara mbovu na si maengeneer
 
Hiyo ya less cost, high quality haijawai kutokea duniani. Labda itakuwa huku Tanzania. Ina Maana hata ule msemo wa bure ni ya ghali umekupita kombo.
 
Subash Patel. Ni kampuni kati ya Kampuni yao Tanzu yenye malumbano ya KIFAMILIA. Yawezekana Caspian ni mbia.
 
Kama na akili mbovu niambie mradi wowote ambao walau umelalamikiwa kwamba umejengwa chini ya kiwango.


Hata kampuni yako ingefanya vizuri ningefanya the same.

Kuna makapuni kibao yanachoma kodi za wananchi.
Hakuna kitu kama hicho, wewe umeleta mahaba tu.
 
Kama na akili mbovu niambie mradi wowote ambao walau umelalamikiwa kwamba umejengwa chini ya kiwango.


Hata kampuni yako ingefanya vizuri ningefanya the same.

Kuna makapuni kibao yanachoma kodi za wananchi.
Barabara ya Makuyuni mpaka Karatu
 
Estim na Ravji walikua ma engineer wa Konoike.Konoike walipoondoka wakawaachia vifaa hawa wahindi.Hawa wahindi wakawa weledi katika ujenzi.

Pia Walipewa ramani tuu wakakamilisha ujenzi wa mahali pa kuzeekea mstaafu msoga bure.Hivyo tenda nzuri wanalamba na jamaa wa sasa hakohoi hapo.

Ile ya msata-bagamoyo walijenga kwa 1.6bn per km
 
Naunga mkono hoja ya mleta mada. Kuna kampuni zimetuibia kwa kujenga miradi yao chini ya kiwango. Barabara ya Morogoro nakumbuka walijenga Wajapani na kampuni yao ya KONOIKE. barabara ilikuwa bora sana.

Sasa kaangalie barabara ya Kigoma to Uvinza ovyo sana sijui kampuni gani walipewa ile kazi. Hata barabara ya Tinde to Isaka ni bora sana kuliko ya Tinde Shinyanga.

Funika bovu ni Kahama to Rusahunga kupitia Ushirombo,Runzewe na Nyakanazi ni barabara bora sana sijui kwa kuwa inaenda Rwanda kwa Kagame.

Ile ya Nyakanazi Kakonko imeshaanza kuharibika hata kabla ya kumwaga lami na ina zaidi ya miaka minne lakini iko vile vile.

Watu wakifanya vizuri tuwapongeze regardless wanatoka wapi na ni upande gani. Hongera sana ESTIM kazi zenu zinapendeza na zinaonekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…