GE2025 Esther Matiko ataja sababu za kujiunga CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,267
Reaction score
3,921
Aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Esther Matiko Jumapili Juni 29, 2025 ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime Mjini kupitia chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na wanahabari, Matiko kando ya kuwashukuru Watanzania kwa kumuungano mkono katika safari yake ya kisiasa, amebainisha kuwa maamuzi ya kuhamia CCM na kuwania nafasi hiyo hayajatokana na jazba ama kutafuta maslahi binafsi na hajadhamiria kuwakatisha tamaa Watanzania wanaomuunga mkono

Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na tafakari yake, hali ya Tarime Mjini na matarajio makubwa ya wananchi, akibainisha kuwa kupitia CCM anaamini kuwa ndoto hizo zitatimia na kutafsiriwa kwa vitendo, akiahidi kuwa sehemu na suluhisho la maendeleo ya Tarime Mkoani Mara

Akiwahakikishia kuwa safari yake ya sasa ni ya matumaini, Matiko amebainisha kuwa Ilani ya CCM ya mwaka 2025/30 ni miongoni mwa mengine yaliyomfurahisha, akisema Ilani hiyo imetoa kipaumbele kikubwa katika huduma za kijamii nchini, huku pia akionesha kuvutiwa na dhamira njema ya Rais Samia na maendeleo makubwa aliyoyafanya ndani ya miaka yake minne ya awali kama Rais wa Tanzania

Soma pia: Esther Matiko sasa ni mwanachama wa CCM


Your browser is not able to display this video.
 
wasiasa malaya malaya
 
Hana kosa kugombea ubunge ndani ya CCM kwani hata Baba Levo, Mwijaku, Shilole, na Bulaya nao wanagombea. Ni haki yao.
 
Hana sababu zozote za msingi zaidi ya msingi wa umalaya wake.
 

Hana sababu wala ya kujielezea, aende tu huko ccm wajumbe washughulike naye, Chauma, Kiko wapi? Mrema na Salum, Kiko wapi?????
 
Am
Tapeli mkubwa, alimbambikia watoto mumewe kumbe watoto ni wa Salum Mwalimu Katibu Mkuu wa Chaumma.
Amekutapeli nini, acha makasiriko ya ******* huwezi kumpangia, we bwege pambana na hali ya ufukara wako. Mmejaa roho za kimaskini za chuki, za kihasidi mambwa km nyie hayatoboagi mtakufa na masononeko.
 
Siwapendi CCM ila mkimpiga chini huyu nitafurahi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…