Estelina Kilasi DC Wanging'ombe: Mmh tumeumia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Estelina Kilasi DC Wanging'ombe: Mmh tumeumia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mngendalyasota, May 10, 2012.

 1. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF,
  Kwanza nimesikitishwa sana na uteuzi wa Estelina Kilasi (mbunge wa zamani wa Mbalali) kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Wanging'ombe yenye makao yake makuu Igwachanya. Huyu mama alibwagwa vibaya sana na Mh Kilufi (mbunge wa sasa) kwenye kura za maoni 2010 kutokana na kushindwa kuwaletea Wana-mbalali maendeleo waliyoyataka. Miongoni mwa mapungufu aliyoyaonyesha akiwa mbunge ni kama ifuatavyo: kwanza wakati wafugaji wakihamishwa kutoka Ihefu kwenda mikoa ya kusini, rushwa ilitawala sana ktk kupembua nani ahame na nani abaki bonde la Usangu tena kinara wa kula rushwa akiwa mkuu wa wilaya wa wkati huo Hawa Ngurumo. Estelina Kilasi hakuwasaidia hata kidogo wale wafugaji kuona haki inatendeka. Pili wakati Gilbert Dololo(marehemu kwa sasa) mkuu wa wilaya wa zamani pia wa Mbalali alipokuwa anawaweka rumande wafanyabiashara ya mpunga wa Mbalali-Rujewa na Igulusi eti tu kwa kutokuelewana viwango vya ushuru wa magunia ya mchele yanayotoka nje ya wilaya, Estelina Kilasi alikaa kimya. Mwisho mama huyu huyu akiwa mbunge alikaa kimya wakati wakulima wa mpunga wa Mbalali na Kapunga walipokuwa wananyanyaswa na wawekezaji kwa kupandishiwa kodi ya kukodi majaruba ya mpunga na kunyimwa maji ya kunyweshea mipunga yao kwenye matoleo.
  Huyu ndo leo kateuliwa na JK aende akaijenge Wanging'ombe wilaya mpya kabisa wakati jimbo lake lilimshinda.
  Nawasilisha.
   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Hivi unadhani JK anamuda wa kujali yote uliyo andika? Siku hizi ili uonekane mtumishi uliyetukuka wewe kuwa yes man tu kwa kila ccm inalofanya. Ukifanya hivyo hata wewe next time utakuwa mkuu wa mkoa
   
 3. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu si ndo kwenye kampeni za 2000 alijulikana kama Bar medy pale Mbarali?.Huyu alikuwa chakula cha Mzee wa"ubinafsishaji" enzi zile.Na promotion hadi kupata Ubunge ilikuwa ni kum-please 2nd lady.Hakuna kitu hapo,Wanging'ombe wasahau maendeleo.
   
 4. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu si ndo kwenye kampeni za 2000 alijulikana kama Bar medy pale Mbarali?.Huyu alikuwa chakula cha Mzee wa"ubinafsishaji" enzi zile.Na promotion hadi kupata Ubunge ilikuwa ni kum-please 2nd lady.Hakuna kitu hapo,Wanging'ombe wasahau maendeleo.Vp ule mnada mkubwa wa kila tarehe 27 upo pale kando ya lami?.Kilasi atauhujumu na huo
   
 5. k

  kimeta cha ufisadi JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kweli kuwa huyu mama hana uwezo huo ni mtazamo wenu na kilufi, huyu mama alikuwa mtetezi wa wana mbarali hadi siku moja aliongea kwa kulia, sema ilikuwa ni mipango tu ya serikali ilikuwa vigumu kuipinga that why hata kilufi atamaliza muda wake bila kurudisha ardhi.
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  :biggrin1: hapo juu mnajua kuua kweli...
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  pole ndugu yangu mgendalyasota. Hivi wewe ulikuwa unategemea jk afanye nini!!! Hiyo ndo tabia ya sisi m ....kwamba ukikosa ubunge ama ukikataliwa kwenye kura za maoni. Usihofu kabisa maana either ukuu wa mkoa,au wilaya,au ukurugenzi kwenye makampuni ya umma,au mwenyekiti wa bodi ya makampuni ya umma utaupata! Huo ndio utawala bora wa sisi

  ndugu yangu vua gamba vaa gwanda!
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hvi kuna watu bado wanafikiri kuwa Ma-DC na RC wanaleta maendeleo?? hahahahaaaaa ............... hizo ni post za ulaji tu. Ndiyo maana zinatolewa kwa fadhira kwa wanahabari na watangazaji. Subirini muone ............ zamu ijao ni ya KIBONDE!!!
   
 9. E

  Edy New Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu nakutahadhalisha leo kateuliwa unamuandika vibaya na akifanya vizuri pia usisite kumsafisha maana ufikiriavyo kuhusu huyu mama sivyo hata kidogo atawaaibisha na mawazo yenu potofu kumhusu yeye
   
 10. a

  annalolo JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  arali wakapa

  ha ha ha imebidi nicheke alilia. kwahyo alivyolia ndo mbarali walipata maendeleo
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Ccm huwa hawana kizuri, always wanatoa watu kwenye recycle bin, sasa utaona watu walivyooza
   
 12. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  wewe acha roho usaliti, yote uliyoyasema ni dhahiri una kaajenda ka siri? na kama si hivyo ingekuwa ni vema turudi mabarari, kwani kilufi ni mbunge kwa sasa nini kafanya kama mbadala wa kilasi? majimbo mengine wote tunayajua, swala la ihefu ni la kitaifa zaidi na utaratibu uliratibiwa na serikali, wale waliotekeleza vibaya tuliona kilasi alivyohangaika na mwisho wake kuwajibika kwa dc hawa ngurume. na pili kilasi ni msomi mzuri kabisa (Holder wa CPA-T), labda ungenishawishi kuwa nafasi ya ukuu wa wilaya kwake ni ndogo ningekupata, na pengine ningekuwa mimi ningependa angepewa kuwa mkurugenzi wenu.
   
Loading...