ESCROW: Serikali kulifungia gazeti la CITIZEN wiki Ijayo

ESCROW: Serikali kulifungia gazeti la CITIZEN wiki Ijayo

Kama ndivyo, hizo habari walizonazo wazitoe kwenye makala maalumu hata kama watafululiza siku tatu, nina inamni itawalipa na hata taifa pia litapata faida.

Wafanyehivyo kabla hawajafungiwa ili wakifungiwa ijulikane ni kwa sababu hiyo. Kuwafungia kwa habari za Escrow ambazo ziko wazi tayari inakaa ki visasi zaidi na si control.

Ndugu Kikwete lazima ajibu japo si leo.
 
Anavyofanya ndio anazidi kujichafua, dawa pekee ya yeye kujisafisha ni kuacha ukweli utimie na wote wanaoenda kinyume na sheria za nchi wachukuliwe hatua bila kujali vyeo wala koo zao. Na hii hata kama yeye atabainika basi akubali utii wa sheria bila shuruti. @Nape Nauye, Mwigulu Nchemba MwanaDiwani na wengineo mlio karibu na Rais wetu mshaurini.
 
Last edited by a moderator:
East Africa ndugu yake citizen limeshapumzishwa tusubiri tuone
 
Kuna ambacho hamkusema ni uongo? Hata jana tu mngeambiwa huyu dalali wa escrow maji yashazidi unga mgesema ni uongo lakini kiko wapi sasa?

Hao wasikuumize kichwa ni waweza kuwa CCM farasi, si unajua kuna CCM imani na CCM masilahi (rejea J.S. Warioba)!
 
Acha rifungiwe tu kwanza ni gazeti la wakenya ambao hawana nia njema na taifa letu.
 
Serikali dhalimu inazidi kuweweseka.

#OkoaNchiYetuTokaKwaWahuninaMafisadi
 
Pia The Citizen la tar 14 mwezi huu limeandika simulizi ya aliyekuwa naibu balozi mdogo wa Marekani huko Zanzibar, Mr Petterson.

Huyu alisema pamoja na mambo mengine kuwa wanamapinduzi walionekana kuongozwa na John Okello, na kwamba siku hiyo Mzee Karume, Kassim Hanga na Mohamed Babu hawakuwepo Zanzibar bali walikuwa Dar.

Na hili nalo linaweza 'kuwaudhi'?
 
Hili gazeti limekuwa likiandika pia habari kuhusu madawa ya kulevya.
Wakaandike kwao kenya maana huko pia yapo wakafanye hiyo investigative journalism huko huko pambafu zao!!!!
 
Hampendi kuambiwa ukweli eheeee ccm bwana mijinga kweli.
 
soma hii habari halau tazama jinsi GAZETI LA SERIKALI linavyo waita mawaziri na viongozi wetu

B5Foxr-IUAAQOD-.jpg:large
Unaka waitweje na hilo ndio jina lake.
 
Wakaandike kwao kenya maana huko pia yapo wakafanye hiyo investigative journalism huko huko pambafu zao!!!!

Hahahaa. Hali imekuwa mgumu town eh?

Anyway ile wizara ile yule jamaa aliyejifanya kichwa mhumu kahamishwa kawekwa mwingine.

Hopefully, mambo yatakwenda swafiiii sasa.
 
Hahahaa. Hali imekuwa mgumu town eh?

Anyway ile wizara ile yule jamaa aliyejifanya kichwa mhumu kahamishwa kawekwa mwingine.

Hopefully, mambo yatakwenda swafiiii sasa.
Asubuhi Nimesoma kwenye gazeti la mwananchi, Naibu waziri wa habari na mkurugenzi wake walilitembelea gazeti hilo ghafla bila taarifa. Hai kupitia muda nikitafuta gazeti la the East African, nikapata taarifa kuwa limefungiwa kusambazwa Tanzania na sababu zilizotolewa naziona hazijitoshelezi. Kwa hiyo sishangai kusikia ya kufungiwa the Citizen. Inaonyesha safari ya kwenda mwananchi ilikuwa kupeleka ujumbe!
 
soma hii habari halau tazama jinsi GAZETI LA SERIKALI linavyo waita mawaziri na viongozi wetu

B5Foxr-IUAAQOD-.jpg:large
Siku hizi ukimwita kiongozi bila kutaja Mheshimiwa unaweza ukatolewa nje kwa kuwadharau viongozi
 
kikwete alipolifungia ----------- alidhani kamaliza,mwishowe atalifungia hadi uhuru siku wakimuandika ndugu kikwete badala ya dokta profesa kikwete..ajiandae kulifungia na mawio,kubenea katokea mlango mwingine..

Kwani na mtandaoni amelifungia?Kwa jinsi utandawazi ulivyo wamefanya kazi bure,litakuja tu hata kwa njia ya PANYA.
 
Back
Top Bottom