Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Escrow kumuumbua Rais Kikwete

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete, anahaha kujiokoa na kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow, ndani ya Benki Kuu (BoT).

Mpango wa sasa, ni kuwakamata baadhi ya waliopewa fedha na James Rugemalira, mmoja wa wamiliki wa IPTL ili kuzima mjadala.

Profesa Anna Tibaijuka, mbunge wa Muleba Kusini (CCM), yumo katika orodha ya wanaotakiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote wiki hii.

Tayari Prof. Tibaijuka amehojiwa zaidi ya mara moja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), kuhusu Sh. 1.6 bilioni alizopewa na Rugemalira.

Mkakati wa kumfikisha mahakamani Prof. Tibaijuka, unasukwa kwa ustadi mkubwa na waziri mmoja mwandamizi katika serikali ya Rais Kikwete.

"Watanaka Prof. Tibaijuka apelekwe mahakamani kwa hoja kuwa, kwa hadhi aliyonayo kimataifa, sakata zima la Akaunti ya Tegeta Escrow litakuwa limezimwa," anaeleza mtoa taarifa.

Anasema, "Lakini nataka nikuhakikishie, kitendo hicho kitasababisha tatizo kukua. Rais Kikwete anafahamu fika Harbinder Singh Sethi wa IPTL kuwa alitokea ikulu kabla ya kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya Escrow."

Anasema, "Ni vigumu kwa Rais Jakaya Kikwete kufanikiwa kujitenga na kashfa ya ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 321 bilioni zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow."

Kiasi cha Sh. 321 bilioni zilikwapuliwa kutoka akanti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT), kati ya Septemba na Novemba 2013; na Prof. Tibaijuka alipewa Sh. 1.6 bilioni na mmoja wa waliokuwa wabia katika kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni "mmiliki mpya wa IPTL/PAP," Harbinder Singh Sethi, aliletwa nchini na mmoja wa wanafamilia wa Rais Kikwete.

Taarifa zinasema, wanaoshinikiza Prof. Tibaijuka kufikishwa mahakamani wanajenga hoja mbili. Kwanza, kwamba hatua hiyo italegeza msimamo wa wahisani wa kuinyima misaada Tanzania; na kwamba kelele zote za ndani zitakuwa zimezimwa.

Pili, hatua ya kumfikisha mahakamani waziri huyo wa zamani wa ardhi, kutasaiidia kumkingia kifua waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo na kuzima mjadala bungeni.

Rais Kikwete alimfuta kazi Prof. Tibaijuka katika mkutano wa "Wazee wa Dar es Salaam," tarehe 23 Desemba 2014.

Inaelezwa kuwa singasinga alikutana na rais, ikulu jijini Dar es Salaam; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni ya shilingi BoT hata bila kumfahamisha Rugemalira – mbia mwenzake.

Taarifa zinasema, sasa rais anashinikizwa kumfukuza Prof. Tibaijuka kutoka Kamati Kuu (CC) ya CCM na baadaye kumfikisha mahakamani kwa madai ya wizi na utakatishaji wa fedha.

Kupatikana kwa taarifa kuwa serikali ya Rais Kikwete inapanga njama za wizi kwa kupeleka baadhi ya waliochotewa fedha na Rugemalira, kumekuja wiki tatu baada ya Kikwete kudai kuwa fedha katika akaunti ya Escrow, hazikuwa za umma.

Akihutubia wanaoitwa, "Wazee wa Dar es Salaam," katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema, mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow yalilipwa kwa PAP baada ya Mahakama Kuu kutoa "amri" tarehe 5 Septemba 2013."

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa ili kusubiri kumalizika kwa mgogoro kati ya Tanesco na IPTL, uliohusu madai ya udanganyifu katika uwekezaji; na hata gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge – ambavyo vilifanywa na kampuni hiyo ya kigeni.

Kampuni ya IPTL ni muungano wa kampuni mbili – VIP Engineering and Marketing Limited ya James Rugemalira, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa na MECHMAR ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70 za hisa.
 
Kama ni kweli ndivyo kinachoendelea... Anna Tibaijuka is a SCAPEGOAT... na Anajulikana fika alikuwa hana Makundi ndani ya CCM hence ni rahisi kumsengenya na kumuangusha...

Sababu, ni kwanini CHENGE hawamjadili huko CC aondoke kwenye CCM ? kwanini Anna Makinda bado anamtumia CHENGE kwenye maamuzi mengi tu BUNGENI ni kwasababu alisoma HARVARD ??? Anna Tibaijuka is Bright as well!!!

Nchini Kenya Wanasifia Uamuzi wa Rais Kikwete sababu -- Rais katoka kabila dogo na kamfukuza kazi mtu wa kabila kubwa na hakuna mtafakuru wa kikabila nchini...

Is there ENOUGH is ENOUGH ??? Yeye Hakuiba hizo PESA... Wezi wapo na Wengine around Rais wetu na hakuna wa kuwashitaki... Is there a REAL JUSTICE in OUR BELOVED NATION ??
 
Prof Anna alipewa hela kama zawadi na yeye hakuwa na maamuzi yoyote hama Wizara Fedha, BoT wala Tanesco. Kwa nini yeye tu ndo ashikiwe bango. Kama ni kiasi cha pesa alichopewa mbona Chenge haguswi. Kama Prof Tibaiijuka anasakamwa kwa kuwa ni Mwanamke na ni Mhaya na kwa sababu ya kupewa hela na Mhaya (kaka yake kama alivyosema yeye) basi hapa Wahaya wote tunasakamwa.
 
Nchini Kenya Wanasifia Uamuzi wa Rais Kikwete sababu -- Rais katoka kabila dogo na kamfukuza kazi mtu wa kabila kubwa na hakuna mtafakuru wa kikabila nchini...

Is there ENOUGH is ENOUGH ??? Yeye Hakuiba hizo PESA... Wezi wapo na Wengine around Rais wetu na hakuna wa kuwashitaki... Is there a REAL JUSTICE in OUR BELOVED NATION ??
It will be a bit too harsh to say that your observations are based on stupidity. So, I 'll just say that your observations are baseless.
Phew!! .. What an a$$!
 
....

......Zimwi limevimba ndani ya nyumba ...kalikuwa ka mjusi tu sasa LIMAMBA !!
 
rais hana maamuzi yoyote zaidi ya kujisafisha kwa wananchi vilaza kama yeye
 
Kubenea ni mchekeshaji tu na anaandika haya kumfurahisha bosi wake
 
Hivi ni shilingi ngapi zilizokuwepo kwenye account ya Tegeta ESCROW na ngapi zilichotwa? Nimesoma ripoti ya CAG inasema bilion 203 ndio zilikuweno na hizo ndizo zilichotwa. Magazeti mengine yanasema bilioni 306, mengine bilioni zaidi ya 300, Kubenea naye anasema bilioni 321, nani mkweli?
 
Hapa nikujiliwaza tu, ukweli wa sakata la ESCROW hata siku moja hauwezi kuzimwa na watanzania waleo hawadanganywi.

1. ESCROW nikashifa ndani ya shirika la umeme TANECO, waziri mwenye dhamana MUHONGO, sasa kuwajibisha waziri wa Ardhi ni maajabu tena yakutisha.

2. Waliotakatisha fedha ni viongozi wengi wakuu serikalini, akiwemo, aliyekuwa AG nk, kuwaacha hawa nje nikuichafuwa zaid serikali ya kikwete, nahapo ndipo watu watataka kujuwa undani zaidi

3. Ndani ya ccm kunamgawanyiko wakutosha, wapo wasiopenda anavyotendewa nakuadhiriwa Anna Tibaijuka ilhali akina chenge, Werema nawengine wengi wakihifadhiwa. Tusubiri bunge lianze tutaona hili varangati, si ajabu ccm kupasuka

4. Watanzania kuambiwa fedha sio za umma wakati huo huo tunaambiwa kodi yetu ipo mle, sasa kodi sio mali ya umma, tunaambiwa sio mali ya umma vipi CAG alingiaje kufanya ukaguzi wa fedha zisio za serikali?

5. Inakuwaje mama Tibaijuka na wengine vidagaa wapelekwe mahakani, wakati huo huo Singasinga hatajwi wala kuguswa? tusubiri kuona wabunge wa bunge la Jamhuri wataendelea kuwa wapole, kufanywa wajinga wakishuhudia mbunge mwenzao Anna akiadhiriwa majizi yakiponda raha tena mvamizi/mlowezi, zaidi Ikulu ikifaidisha jamii na familia yake bila kuguswa?

Kwa hili serikali ya Kikwete inasafari ndefu, na mwisho wake isipokuwa makini itaanguka vibaya ama kusambaratika kwa kulindana na kutowana kafara. Tusubiri.
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete, anahaha kujiokoa na kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow, ndani ya Benki Kuu (BoT).

Mpango wa sasa, ni kuwakamata baadhi ya waliopewa fedha na James Rugemalira, mmoja wa wamiliki wa IPTL ili kuzima mjadala.

Profesa Anna Tibaijuka, mbunge wa Muleba Kusini (CCM), yumo katika orodha ya wanaotakiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote wiki hii.

Tayari Prof. Tibaijuka amehojiwa zaidi ya mara moja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), kuhusu Sh. 1.6 bilioni alizopewa na Rugemalira.

Mkakati wa kumfikisha mahakamani Prof. Tibaijuka, unasukwa kwa ustadi mkubwa na waziri mmoja mwandamizi katika serikali ya Rais Kikwete.

"Watanaka Prof. Tibaijuka apelekwe mahakamani kwa hoja kuwa, kwa hadhi aliyonayo kimataifa, sakata zima la Akaunti ya Tegeta Escrow litakuwa limezimwa," anaeleza mtoa taarifa.

Anasema, "Lakini nataka nikuhakikishie, kitendo hicho kitasababisha tatizo kukua. Rais Kikwete anafahamu fika Harbinder Singh Sethi wa IPTL kuwa alitokea ikulu kabla ya kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya Escrow."

Anasema, "Ni vigumu kwa Rais Jakaya Kikwete kufanikiwa kujitenga na kashfa ya ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 321 bilioni zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow."

Kiasi cha Sh. 321 bilioni zilikwapuliwa kutoka akanti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT), kati ya Septemba na Novemba 2013; na Prof. Tibaijuka alipewa Sh. 1.6 bilioni na mmoja wa waliokuwa wabia katika kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni "mmiliki mpya wa IPTL/PAP," Harbinder Singh Sethi, aliletwa nchini na mmoja wa wanafamilia wa Rais Kikwete.

Taarifa zinasema, wanaoshinikiza Prof. Tibaijuka kufikishwa mahakamani wanajenga hoja mbili. Kwanza, kwamba hatua hiyo italegeza msimamo wa wahisani wa kuinyima misaada Tanzania; na kwamba kelele zote za ndani zitakuwa zimezimwa.

Pili, hatua ya kumfikisha mahakamani waziri huyo wa zamani wa ardhi, kutasaiidia kumkingia kifua waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo na kuzima mjadala bungeni.

Rais Kikwete alimfuta kazi Prof. Tibaijuka katika mkutano wa "Wazee wa Dar es Salaam," tarehe 23 Desemba 2014.

Inaelezwa kuwa singasinga alikutana na rais, ikulu jijini Dar es Salaam; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni ya shilingi BoT hata bila kumfahamisha Rugemalira – mbia mwenzake.

Taarifa zinasema, sasa rais anashinikizwa kumfukuza Prof. Tibaijuka kutoka Kamati Kuu (CC) ya CCM na baadaye kumfikisha mahakamani kwa madai ya wizi na utakatishaji wa fedha.

Kupatikana kwa taarifa kuwa serikali ya Rais Kikwete inapanga njama za wizi kwa kupeleka baadhi ya waliochotewa fedha na Rugemalira, kumekuja wiki tatu baada ya Kikwete kudai kuwa fedha katika akaunti ya Escrow, hazikuwa za umma.

Akihutubia wanaoitwa, "Wazee wa Dar es Salaam," katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema, mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow yalilipwa kwa PAP baada ya Mahakama Kuu kutoa "amri" tarehe 5 Septemba 2013."

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa ili kusubiri kumalizika kwa mgogoro kati ya Tanesco na IPTL, uliohusu madai ya udanganyifu katika uwekezaji; na hata gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge – ambavyo vilifanywa na kampuni hiyo ya kigeni.

Kampuni ya IPTL ni muungano wa kampuni mbili – VIP Engineering and Marketing Limited ya James Rugemalira, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa na MECHMAR ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70 za hisa.
Watampleka Tibaijuka mahakamani, atawashinda huko mahakamani, na baada ya hapo atawafungulia kesi ambayo hatma yake watamlipa tena mabilioni pengine zaidi ya hayo aliyopewa na Ruge.

Serikali inayoendeshwa ki-mazingaombwe kama alivyosema Mwanakijiji.
 
Ukweli upo kwenye ripoti ya CAG. HAO WENGINE AKIWEMO KUBENEA ni wazushi na wazandiki
 
Watampleka Tibaijuka mahakamani, atawashinda huko mahakamani, na baada ya hapo atawafungulia kesi ambayo hatma yake watamlipa tena mabilioni pengine zaidi ya hayo aliyopewa na Ruge.

Serikali inayoendeshwa ki-mazingaombwe kama alivyosema Mwanakijiji.
Inavyoelekea kuna mkakati ambao unaendelea ili Tibaijuka aonekane hana hatia. Mbona hawa akina Kubenea hawawataji akina Ngeleja, Chenge na wengine waliokula fedha hizo? Kubenea ni mpuuzi tena amepindukia
 
It will be a bit too harsh to say that your observations are based on stupidity. So, I 'll just say that your observations are baseless.
Phew!! .. What an a$$!

How ??
Kobello Educate me please... that's why we are here...
 
Werema amesamehewa kwa sababu alikubali kuondoka mwenyewe huu Tibaijuka ameshakuwa mbuzi wa kafara
 
Back
Top Bottom