Escrow: Kumbe PAC walituingiza choo cha sokoni (Part I)

Escrow: Kumbe PAC walituingiza choo cha sokoni (Part I)

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,149
UONGO WA RIPOTI YA PAC KUHUSIANA NA SAKATA LA ESCROW - PART 1.

Ripoti ya PAC Ukurasa wa 6 (kwa nakala iliyokuwa kwenye tovuti ya Bunge) unanukuliwa hivi:

“Mheshimiwa Spika, gharama hizi zilikoma kulipwa moja kwa moja kwa IPTL mwaka 2007 baada ya TANESCO kubaini kuwa IPTL inakokotoa gharama hizo kwa msingi wa USD 38.16 milioni (ambayo ni sehemu ya mkopo wa USD 105 milioni uliochukuliwa na wanahisa kutoka Umoja wa Mabenki ya Malaysia (Consortium of Malaysian Banks) ambao baadaye ulinunuliwa na Standard Chartered Bank ya Hong Kong) badala ya mtaji wa uwekezaji wa kiasi cha Sh. 50,000 uliosajiliwa BRELA na hivyo kufanya tozo ya capacity charges kuwa kubwa. Endapo ungetumika mtaji wa uwekezaji wa Sh. 50,000/= katika kukokotoa capacity charges TANESCO ingekuwa inalipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa Spika, kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha capacity charges kilichokuwa kinatozwa na IPTL mnamo mwaka 2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya capacity charges. Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo.
Mheshimiwa Spika, mpaka tunapowasilisha Taarifa hii Bungeni, Uamuzi wa ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa, hivyo TANESCO wanaendelea kulipa USD. 2.6 milioni (sawasawa na shilingi 4,511,000,000/= kwa mwezi) kila mwezi kama capacity charges kwa IPTL izalishe au isizalishe umeme. Hivyo, utekelezaji wa Mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya IPTL na TANESCO umetawaliwa na migogoro toka ulipoanza mpaka sasa.”

NOTE:

Paragraph ya kwanza iliyonukuliwa hapo juu inadai mwaka 2007 TANESCO ilibaini tatizo halafu kwenye paragraph inayofuatia TANESCO ikaamua kufungua shauri ICSID mwaka 2004 kutokana na kutoridhishwa yale waliyoyabaini mwaka 2007. Tatizo linagunduliwa 2007 halafu unaenda kulifungulia shauri ICSID mwaka 2004?

FACTS:

• Hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa ICSID mwaka 2004 na TANESCO.
• Kesi pekee iliyopata kufunguliwa ICSID na TANESCO ni ile kesi/shauri namba ARB/98/8 iliyofunguliwa mwaka 1998 na kutolewa uamuzi mwaka 2001. Kesi/shauri hilo linarejewa (referred as) kama ICSID-1 kwenye Ripoti ya PAC.

USHAHIDI:

• Ripoti ya PAC haijaweza kutuambia hiyo kesi iliyofunguliwa mwaka 2004 na kurejewa kama ICSID-2 ilikuwa kesi/shauri namba ngapi. Kwenye Ripoti yaPAC, ICSID-1 ilitajwa kama kesi iliyofunguliwa mwaka 1998 na namba yake kutajwa kama ARB/98/8 lakini Ripoti hiyo hiyo imeshindwa kutuambia namba ya kesi ya ICSID-2.
• Hivyo hivyo, hukumu ya kesi/shauri la ICSID-1 iliambatanishwa kwenye Ripoti ya PAC kama Kiambatanisho Na. 2 lakini Ripoti hiyo ya PAC haikuambatanisha hukumu ya hiyo kesi ICSID-2.
• Hata kwenye tovuti ya ICSID, hakuna kesi/shauri lolote lililofunguliwa na TANESCO 2004 ama kutolewa hukumu/maamuzi February 2004. Isitoshe hakuna kesi/shauri lolote lilifunguliwa na TANESCO zaidi ya ile kesi/shauri la ICSID-1.

HUKUMU YA ICSID-2 INACHANGANYWACHANGANYWA:

• Kwanza kwa sababu kulikuwa hakuna na kesi/shauri lililofunguliwa na TANESCO mwaka 2004 ICSID, ina maana pia kulikuwa hakuna hukumu ya hiyo kesi/shauri. Japo hiyo hukumu haipo lakini hukumu ya hiyo kesi/shauri imekuwa ikitajwa mara kadhaa. Kwenye paragraph ya pili hapo juu hiyo hukumu ya kesi isiyokuwepo inaelezwa kama “Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo” na kwenye paragraph inayofuatia kama “Uamuzi wa ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa...”. Kuna tofauti ya kukubaliana “kanuni ya ukokotoaji” na “kukutoa upya”. Kwa kiengereza ni “agree on formula to calculate” na “recalculate”.

TAREHE YA HUKUMU YA ICSID-2


Ukurasa wa 6 wa Ripoti ya PAC ulidai kuwa “mnamo mwaka 2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga” na kwenye Ukurasa wa 34 wa Ripoti ya PAC inadai inadai “.. (a) Kutekelezwa kwa uamuzi uliotolewa na Kituo cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Kimataifa (ICSID) mwezi Februari 2004 (ICSID 2). Aidha ICSID 2 ilielekeza TANESCO na IPTL kukokotoa upya kiwango cha capacity charges”. Ni vigumu kuamini kuwa shauri linafunguliwa ICSID mwaka 2004 (hata kama lilifunguliwa tarehe 1 January 2004) likaja kupata ufumbuzi February 2004. Kama ilivyoelezwa hapo juu kulikuwa hakuna shauri lililofunguliwa na TANESCO kule ICSID mwaka 2004.


UZITO WA ICSIDI-2 KWENYE RIPOTI:


Hoja kuu ya Ripoti ya PAC ni kuwa fedha za Escrow zilikuwa “zimechotwa” kwa sababu makubaliano kati ya TANESCO na IPTL hayakuzangatia madai ya TANESCO yaliyopelekea kufungua ICSID-2 na uamuzi uliotolewa kwenye hukumu ya hiyo kes/shauri la ICSID-2. Tumeona hakuna ICSID-2 lakini uamuzi wa hukumu ya ICSID-2 imetumiwa kujenga hoja kuu mara kadhaa kwenye ripoti. Hiyo hukumu imetajwa kwenye ukurasa wa 6 (mara mbili), 23, 26, 34, 40 (mara mbili).


HITIMISHO:

Tuhuma kubwa zinatolewa kuwa fedha za Escrow zilitolewa kuilipa IPTL bila ya kuzingatia maamuzi ya kesi/shauri ICSID-2 kwenye kurasa hizo zote juu. ICSID-2 haiko, na hukumu ya ICSID-2 na tuhuma zote zinazohusisha ICSID-2 nazo ni TUHUMA ZA UONGO. Ripoti ya PAC imelidangaya Bunge na Taifa zima kwa ujumla.
Documents zote hapa: http://www.orcis.com/escrow

*Imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Salim Khatri.
 
Sasa hapa hawa jamaa sijui watasemaje.
Salary slip, ukuye pande hii.
 
Last edited by a moderator:
Kumbe kina yerico na saanane walikua sawa asee,zito hafai
 
Wawe walituingiza Chaka au vp...ishu ni kuwa kulikuwa na upigaji uliopita kiwango.. Yaani utadhani nchi haina hata chombo kimoja cha ulinzi na usalama ambacho kilitakiwa kishtukie mchezo


Hata mjitetee vipi hapa kwenye TEGETA ESCROW kuna ufisadi na wizi uliopitiliza na kama ndy hivyo mbona utetezi wa serikali uliotelewa na Pro MUHONGO haukutaja haya unayo tuambia. TATIZO NINALOLIONA HAPA MPO WATZ WACHACHE SANA AMBAO MNACHEZA NA MAISHA/UHAI WAZALENDO WENGI WA NCHI HII YA HAYATI BABA WA TAIFA - Lala mahali pema peponi Baba, ila taifa lako kwa sasa amani haipo kabisa.
 
Hata mjitetee vipi hapa kwenye TEGETA ESCROW kuna ufisadi na wizi uliopitiliza na kama ndy hivyo mbona utetezi wa serikali uliotelewa na Pro MUHONGO haukutaja haya unayo tuambia. TATIZO NINALOLIONA HAPA MPO WATZ WACHACHE SANA AMBAO MNACHEZA NA MAISHA/UHAI WAZALENDO WENGI WA NCHI HII YA HAYATI BABA WA TAIFA - Lala mahali pema peponi Baba, ila taifa lako kwa sasa amani haipo kabisa.
Vipi kama uache ya muhongo kasema nini,uchambue hizi fact hapa,
 
Jupitia post hii ndio tutajua tofauti kati ya TRUE GREAT THINKERS NA MAKANJANJA wa jukwaa hili. Thanks mleta mada ila subiri wajinga watakavyo divert.
 
aliyejiuzulu na asiyekua na nidham ya uongozi "hata mwanae kuongea lugha mbaya"....wametekeleza hayo kwa nini...WARUDISHIWE NYADHIFA ZAO TUSONGE MBELEEEeeeeeeeeeeeee
 
Hiviiiiiiii,let say ni kweli hela zote ni za IPTL,swali la msingi la kujiuliza ni, je hakuwa na kazi nazo hadi agawe kama njugu kama kweli zote ni halali yake kweli?????,inawezekana hela yako halali ukaigawa kama njugu kwa kiasi hcho kweli,hakuna mazingira ya rushwa kweli?????
 
Kumbe kina yerico na saanane walikua sawa asee,zito hafai
yani rukeni juu, tueni chini, laleni, simameni,jikunjeni kama chura ila ukweli uko wazi kuwa Kikwete anatetea wizi wa ESCROW kwasababu yeye ndio mnufaika mkuu wa sakata hili.
mpaka sasa wahisani hawana hamu na sisi kwa uwizi huu wa uliofanywa na wateule wa raisi na raisi mwenyewe.
 
Mkuu, Invisible hebu tusaidie kumtafuta Zitto aje atoe ufafanuzi kwani akikaa kimya maana yake ni kuwa, watu waamini hii kitu.
 
Last edited by a moderator:
Delivering Global Dispute Resolution Services

Overview|Experience|Professionals|News|Alerts|Publications|Events
Related Experience

Investor-State Arbitration Experience

The following is a list of representative cases Hunton & Williams’ International Arbitration and Transnational Litigation team has handled before the International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID):

Standard Chartered Bank (Hong Kong) Limited (SCB HK), as Assignee from Independent Power Tanzania Limited (IPTL) v. Tanzania Electric Supply Company (TANESCO), ICSID ARB/10/20 (filed September 2010, pending) (Arbitrators: Donald McRae (President), Zachary Douglas, Brigitte Stern). Hunton represented TANESCO in a claim filed by SCB HK as the alleged security assignee of IPTL under a Power Purchase Agreement (“PPA”) to collect disputed capacity payments from TANESCO on the IPTL power plant located in Dar es Salaam, Tanzania. In a Decision on Jurisdiction and Liability issued 12 February 2014 and published on the ICSID website, the Tribunal found TANESCO had been overcharged and ordered that the parties confer on recalculating and reducing the tariff. The Tribunal further held it did not have jurisdiction to enter a money judgment in favor of SCB HK.
Standard Chartered Bank (SCB) v. The United Republic of Tanzania, ICSID ARB/10/12 (filed May 2010, Final Award rendered 2 November 2012) (Arbitrators: William Park (President), Michael Pryles, Bart Legum). Hunton successfully represented the Government of Tanzania in an investment arbitration filed by Standard Chartered Bank (SCB). SCB claimed Tanzania expropriated a 100 MW power plant, the senior debt of which was owned by SCB’s subsidiary, Standard Chartered Bank Hong Kong (SCB HK). SCB asserted jurisdiction against Tanzania under the UK-Tanzania bilateral investment treaty (BIT). Tanzania filed an objection to jurisdiction, and on 2 November 2012, the Tribunal unanimously sustained Tanzania’s objection under the UK-Tanzania BIT and dismissed the arbitration. The Final Award is published on the ICSID website, and is currently the subject of an annulment proceeding.
Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) v. Independent Power Tanzania Limited(IPTL), ICSID ARB/98/8 (Interpretation Proceeding) (filed June 2008, discontinued August 2010) (Arbitrators: Kenneth Rokison (President), Andrew Rogers, Charles Brower, Makhdoom Ali Khan (replacing Mr. Brower following his resignation)). This was only the second Interpretation Proceeding filed in the history of ICSID, and is unique in that it was filed 7 years after the Final Award in ICSID ARB/98/8. After the original Tribunal from ICSID ARB/98/8 was re-constituted, TANESCO filed a jurisdiction challenge to IPTL’s authority to maintain the proceeding. Before the authority issue was resolved, the case was stayed by consent of the parties following the appointment in Tanzania of a provisional liquidator for IPTL. The arbitration was subsequently discontinued by IPTL pursuant to ICSID Arbitration Rule 44. The procedural history of the case is published on the ICSID website.
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) v. The United Republic of Tanzania, filed July 2008. IPTL filed a Request for Arbitration seeking to enforce the payment guaranty of the Government of the United Republic of Tanzania for the obligations of its wholly-owned electric utility, TANESCO. Hunton represented Tanzania in objecting to registration of the Request for Arbitration. The Request was not registered while TANESCO’s similar objection to IPTL’s authority was being considered by the Tribunal in the Interpretation Proceeding, ICSID ARB/98/8, described above. The Request for Arbitration was withdrawn by IPTL in August 2010
 
hapa mpaka tulete mkalimani,lakini hoja za mleta mada zinajibikaje hizi?
 
Hiviiiiiiii,let say ni kweli hela zote ni za IPTL,swali la msingi la kujiuliza ni, je hakuwa na kazi nazo hadi agawe kama njugu kama kweli zote ni halali yake kweli?????,inawezekana hela yako halali ukaigawa kama njugu kwa kiasi hcho kweli,hakuna mazingira ya rushwa kweli?????

Kugawa au kula peke yake ni uamuzi binafsi, nadhani yule anayefanya wema tofauti na tuliouzoea hapa wa kila mtu kula kwa urefu wa kamba yake ! Anaonekana anatoa rushwa ni mwizi. Mi niwashauri "wazawa" wenye pesa wakome kuwekeza nchini maana wakina nanii matv yao hayata waacha wakastawi
 
Hiviiiiiiii,let say ni kweli hela zote ni za IPTL,swali la msingi la kujiuliza ni, je hakuwa na kazi nazo hadi agawe kama njugu kama kweli zote ni halali yake kweli?????,inawezekana hela yako halali ukaigawa kama njugu kwa kiasi hcho kweli,hakuna mazingira ya rushwa kweli?????

bwana jR sio mjinga kiasi hicho na huwa apigi madili Ya kijinga
Sawa pesa ni za IPTL na kubali
escrow ilikuwa na 306bl
Hisa za JR. 30% Ya hizo hela ni kama 92.bl hapo ni nje Ya hisa na Machmar anachokuwa zinazobaki . Sasa SINGASINGA yeye alichukua hayo mauzo Ya escrow ndo kununulia hisa za IPTL hiyo umuiona kwenye dunia ipi kama sio ufisadi?
 
Hiviiiiiiii,let say ni kweli hela zote ni za IPTL,swali la msingi la kujiuliza ni, je hakuwa na kazi nazo hadi agawe kama njugu kama kweli zote ni halali yake kweli?????,inawezekana hela yako halali ukaigawa kama njugu kwa kiasi hcho kweli,hakuna mazingira ya rushwa kweli?????

mkuu usihangaike nao hawa,tutawanyoosha 2015.bado miezi tu.
 
Hiviiiiiiii,let say ni kweli hela zote ni za IPTL,swali la msingi la kujiuliza ni, je hakuwa na kazi nazo hadi agawe kama njugu kama kweli zote ni halali yake kweli?????,inawezekana hela yako halali ukaigawa kama njugu kwa kiasi hcho kweli,hakuna mazingira ya rushwa kweli?????

Hiyo ni mosi.

Pili: Hivi iweje huo mgao ufanyike kwa formula ambayo hata hauhitaji kuumiza kichwa kugundua kuwa kuna kamchezo hapo...1.6b, 800m, 80m, 40m,3.2b.

Tatu: Mgao huo umefanyika kwa viongozi flan flan wa serikali kutoka wizara na idara zinazo husika na hilo sakata kwa njia moja au nyingine...kwanini??

Nne: Iweje shirika la umma likae kimya kwa miaka saba kuchukua hatua ambazo zingekua na manufaa kwa taifa na serikali ikae kimya tu inaangalia kama vile inataka tanesco waharibikiwe?? Nashangaa eti leo Kiongozi Mkuu anatumia muda mrefu kutueleza sakata zima lilivyokua kama vile tanesco wenyewe hawana midomo.

Kuna Mdau amepost uzi anasema hao viongozi walikua na hisa iptl. naanza kuamini kwa kiasi flani kuwa kuna kaukweli maana ukiangalia mgao huo ulivyokaa...sio bure.
 
hapa mpaka tulete mkalimani,lakini hoja za mleta mada zinajibikaje hizi?

Sitaki kuamini kuwa ripoti nzima itakosa uhalali kutokana na kasoro hii ila nachoamini ni kuwa kunahitajika ufafanuzi kidogo tu au kufanya marekebisho ya kiuandishi tu.
 
The bottom line is,The public money was stolen in the name of ESCROW account at Tegeta,full stop. The rest you can keep to yourself.
 
Back
Top Bottom