Escrow: Kumbe PAC walituingiza choo cha sokoni (Part I)

Escrow: Kumbe PAC walituingiza choo cha sokoni (Part I)

mtoa mada vipi ulipata mgao toka ESCROW, au wewe ni mtoto wa Tibaijuka, endeleeni kujidanganya eti PAC walidanganya lakini mama yako yako kashasepeshwa na bado baba yako mhongo, na ikulu isipokuwa macho lazima isepeshwe,,,,halafu wewe umetoa wapi ujasiri wa kusema PAC ilidanganya kwa uchunguzi gani umefanya, au umetoka kuvuta ugoro na kunywa gongo ukaingia humu ndani kuandika upuuzi wako? hivi wewe umefanya uchunguzi kumuzidi CAG, hebu tunaomba uchunguzi wako na isyo kwenda kusoma ripoti za wanaume unakuja kutapika humu ndani, hata professel aliisoma sana hiyo ripoti lakini povu lilimutoka
 
watanzania tulikua wajinga na wapumbavu kwa kiasi kikubwa. Sasa wajinga wameanza kupungua na ipo siku wataisha kabisa na tanzania ya waerevu na wazalendo itazaliwa. Hili ndilo mleta mada na ccm hawalioni. Hawaoni mabadiliko yalivyo na kasi katika nchi hii, washinda na kulala wakizania wataendelea kututawala kwa ujinga wetu. Na mungu atakua upande wetu kwani hatawaamsha hadi pale watakapoanguka.

kim kardash ngoja niamini kuwa haya uliyoyaandika ni mashiko kweli na hivyo fedha zote ni halali kwenda iptl kama unavyotaka tuamini. Lakini (hata raisi anakiri kuwa) kodi haikulipwa kwa makosa ya ag. Adhabu ya kuikosesha mapato serikali zaidi ya 30bn ni kujiuzulu tu? Eti sasa wameiomba iptl ilipe kodi, wanaiomba. Ni aibu gani hii.

Jambo jingine ndugu yangu hata kama fedha zote zile ni halali kwa iptl, je utakatishaji wa fedha ulifanywa ili kumficha nani? Uchukuaji fedha mkombozi bank na stanbic ulifuta sheria za nchi kweli? Kama utakubali utakasishaji ulifanywa, je hakuna wa kuwajibika? Lipite tu kama nchi haina watu? Tunaenda wapi?

Ndugu yangu mtoa mada, serikali na chama cha mapinduzi hata kikitakasika katika sakata hili la escrow lakini bado harufu ya madudu mengi yanayoendelea kufanywa haitaisha. Kubaliana na mimi tunahitaji mabadiliko makubwa kama tuna dhamira ya kweli ya maendeleo yanayowanufaisha watanzania wote.

umemuuliza maswali magumu ambayo kwa uelewa wa mleta uzi#mwenye roho na akili ya kifisadi#sina hakika kama ataelewa ulicho kifafanua!


***hii nchi imejaa wala rushwa wenye roho za kutamani hata kuupoteza uhai wa flani alimradi tu adhima yao ikamilike.
Hakika ni taifa lenye laanw chini ya utawala wa chama cha makharamia c.c.m!
 
Wawe walituingiza Chaka au vp...ishu ni kuwa kulikuwa na upigaji uliopita kiwango.. Yaani utadhani nchi haina hata chombo kimoja cha ulinzi na usalama ambacho kilitakiwa kishtukie mchezo

hebu jamani kuweni na facts katika hoja zaidi ya kudai tumepigwa tu tumepigwa tu! toeni facts sio kufabricate mambo.
 
Hata mjitetee vipi hapa kwenye TEGETA ESCROW kuna ufisadi na wizi uliopitiliza na kama ndy hivyo mbona utetezi wa serikali uliotelewa na Pro MUHONGO haukutaja haya unayo tuambia. TATIZO NINALOLIONA HAPA MPO WATZ WACHACHE SANA AMBAO MNACHEZA NA MAISHA/UHAI WAZALENDO WENGI WA NCHI HII YA HAYATI BABA WA TAIFA - Lala mahali pema peponi Baba, ila taifa lako kwa sasa amani haipo kabisa.

Acha kukomaa bila facts ww jenga hoja sio tu kudai umeibiwa bila kuthibitisha umeibiwaje!
 
Nchi iko mikononi mwa mafisadi hivyo wanafanya watakavyo wakati wowote ule huku usalama wa mafisadi ukiwahakikishia usalama wao. EPA, utoroshwaji wa wanyama, kagoda, Meremeta, Rada, ndege ya Rais, Richmond/Dowans, Mikataba ya madini, Escrow, uuzwaji wa nyumba, IPTL, Kiwira Coal Mining na madudu mengine chungu nzima. Eti tuna usalama wa Taifa!!! kwi kwi kwi kwi lol!!!

Wawe walituingiza Chaka au vp...ishu ni kuwa kulikuwa na upigaji uliopita kiwango.. Yaani utadhani nchi haina hata chombo kimoja cha ulinzi na usalama ambacho kilitakiwa kishtukie mchezo
 
Nchi iko mikononi mwa mafisadi hivyo wanafanya watakavyo wakati wowote ule huku usalama wa mafisadi ukiwahakikishia usalama wao. EPA, utoroshwaji wa wanyama, kagoda, Meremeta, Rada, ndege ya Rais, Richmond/Dowans, Mikataba ya madini, Escrow, uuzwaji wa nyumba, IPTL, Kiwira Coal Mining na madudu mengine chungu nzima. Eti tuna usalama wa Taifa!!! kwi kwi kwi kwi lol!!!
Watu kama mengi ni mafisadi yasiokoma nadhani tuanze utaratibu wa kuwauwa pengine watatia aibu.
 
.....gharama hizi zilikoma kulipwa moja kwa moja kwa IPTL mwaka 2007......Ni lini Tanesco walibaini tatizo hilo haikuoneshwa ,...baada ya Tanesco kubaini.....Je ni hio 2007 ?

.....
kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha capacity charges kilichokuwa kinatozwa na IPTL mnamo mwaka 2004....Ni lini Tanesco walifungua shauri la pili pia haikuonyeshwa.

NOTE yako yote ni uzandiki haina ukweli zaidi ya kuviringisha ufahamu. LAbda utuonyeshe ni wapi au lini hilo shauri lilifunguliwa ,unaposoma angalia alama zinazotumika zikiwemo koma na fullstop ,unajitia upofu kutaka kupotosha watu wengine,
Ikiwa NOTE yako ni summary basi ukubali kuwa madudu yaligundulika 2004 na kusomwa na kuchunguzwa kwa muda wa miaka mitatu na shauri kufunguliwa 2007 ambapo Tanesco walisimamisha malipo.
:A S-rap: Soma tena utaelewa kama umetumwa basi aliekutuma kakutuma sipo.
 
Sidhani kama uliyoainisha yanahoja yoyote ya msingi katika suala la ESCROW. Bila kujali taarifa ilikuwa na mapungufu kiasi gani ukweli upo pale pale njaa zetu zetu wachache ndiyo chanzo wa umaskini wa Watanzania waliowengi. Ni aibu mtu na akili yako timamu kuendelea kuongelea hivi as if unataka kusema hakuna wizi ulifanyika. Ili uchambuzi wako uwe na maana badala ya kuchambua tarehe na miaka ya matuki yalipotokea ungetueleza kama kodi ya billions ililipwa na je kwa nini fedha zilitolewa wakati bado suala hilo halijafikia muafaka. Porojoporojo hizi ulizoandika zinapunguza credibility ya hicho ulichotaka kusema. Labada kama ulitaka tu kuonekana umeandika kuhusu ESCROW au mtu mwingine aliandika wewe ukaja kuweka tu bila kuangalia kwa undani. PAC wamesaidia waliowengi kujua kuwa kulikuwa na Wizi na mamlaka zinazohusika zimekiri kuwa kuna ukikwaji mkubwa wa taratibu, maadili na sharia.
UONGO WA RIPOTI YA PAC KUHUSIANA NA SAKATA LA ESCROW - PART 1.

Ripoti ya PAC Ukurasa wa 6 (kwa nakala iliyokuwa kwenye tovuti ya Bunge) unanukuliwa hivi:

“Mheshimiwa Spika, gharama hizi zilikoma kulipwa moja kwa moja kwa IPTL mwaka 2007 baada ya TANESCO kubaini kuwa IPTL inakokotoa gharama hizo kwa msingi wa USD 38.16 milioni (ambayo ni sehemu ya mkopo wa USD 105 milioni uliochukuliwa na wanahisa kutoka Umoja wa Mabenki ya Malaysia (Consortium of Malaysian Banks) ambao baadaye ulinunuliwa na Standard Chartered Bank ya Hong Kong) badala ya mtaji wa uwekezaji wa kiasi cha Sh. 50,000 uliosajiliwa BRELA na hivyo kufanya tozo ya capacity charges kuwa kubwa. Endapo ungetumika mtaji wa uwekezaji wa Sh. 50,000/= katika kukokotoa capacity charges TANESCO ingekuwa inalipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa Spika, kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha capacity charges kilichokuwa kinatozwa na IPTL mnamo mwaka 2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya capacity charges. Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo.
Mheshimiwa Spika, mpaka tunapowasilisha Taarifa hii Bungeni, Uamuzi wa ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa, hivyo TANESCO wanaendelea kulipa USD. 2.6 milioni (sawasawa na shilingi 4,511,000,000/= kwa mwezi) kila mwezi kama capacity charges kwa IPTL izalishe au isizalishe umeme. Hivyo, utekelezaji wa Mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya IPTL na TANESCO umetawaliwa na migogoro toka ulipoanza mpaka sasa.”

NOTE:

Paragraph ya kwanza iliyonukuliwa hapo juu inadai mwaka 2007 TANESCO ilibaini tatizo halafu kwenye paragraph inayofuatia TANESCO ikaamua kufungua shauri ICSID mwaka 2004 kutokana na kutoridhishwa yale waliyoyabaini mwaka 2007. Tatizo linagunduliwa 2007 halafu unaenda kulifungulia shauri ICSID mwaka 2004?

FACTS:

• Hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa ICSID mwaka 2004 na TANESCO.
• Kesi pekee iliyopata kufunguliwa ICSID na TANESCO ni ile kesi/shauri namba ARB/98/8 iliyofunguliwa mwaka 1998 na kutolewa uamuzi mwaka 2001. Kesi/shauri hilo linarejewa (referred as) kama ICSID-1 kwenye Ripoti ya PAC.

USHAHIDI:

• Ripoti ya PAC haijaweza kutuambia hiyo kesi iliyofunguliwa mwaka 2004 na kurejewa kama ICSID-2 ilikuwa kesi/shauri namba ngapi. Kwenye Ripoti yaPAC, ICSID-1 ilitajwa kama kesi iliyofunguliwa mwaka 1998 na namba yake kutajwa kama ARB/98/8 lakini Ripoti hiyo hiyo imeshindwa kutuambia namba ya kesi ya ICSID-2.
• Hivyo hivyo, hukumu ya kesi/shauri la ICSID-1 iliambatanishwa kwenye Ripoti ya PAC kama Kiambatanisho Na. 2 lakini Ripoti hiyo ya PAC haikuambatanisha hukumu ya hiyo kesi ICSID-2.
• Hata kwenye tovuti ya ICSID, hakuna kesi/shauri lolote lililofunguliwa na TANESCO 2004 ama kutolewa hukumu/maamuzi February 2004. Isitoshe hakuna kesi/shauri lolote lilifunguliwa na TANESCO zaidi ya ile kesi/shauri la ICSID-1.

HUKUMU YA ICSID-2 INACHANGANYWACHANGANYWA:

• Kwanza kwa sababu kulikuwa hakuna na kesi/shauri lililofunguliwa na TANESCO mwaka 2004 ICSID, ina maana pia kulikuwa hakuna hukumu ya hiyo kesi/shauri. Japo hiyo hukumu haipo lakini hukumu ya hiyo kesi/shauri imekuwa ikitajwa mara kadhaa. Kwenye paragraph ya pili hapo juu hiyo hukumu ya kesi isiyokuwepo inaelezwa kama “Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo” na kwenye paragraph inayofuatia kama “Uamuzi wa ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa...”. Kuna tofauti ya kukubaliana “kanuni ya ukokotoaji” na “kukutoa upya”. Kwa kiengereza ni “agree on formula to calculate” na “recalculate”.

TAREHE YA HUKUMU YA ICSID-2


Ukurasa wa 6 wa Ripoti ya PAC ulidai kuwa “mnamo mwaka 2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga” na kwenye Ukurasa wa 34 wa Ripoti ya PAC inadai inadai “.. (a) Kutekelezwa kwa uamuzi uliotolewa na Kituo cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Kimataifa (ICSID) mwezi Februari 2004 (ICSID 2). Aidha ICSID 2 ilielekeza TANESCO na IPTL kukokotoa upya kiwango cha capacity charges”. Ni vigumu kuamini kuwa shauri linafunguliwa ICSID mwaka 2004 (hata kama lilifunguliwa tarehe 1 January 2004) likaja kupata ufumbuzi February 2004. Kama ilivyoelezwa hapo juu kulikuwa hakuna shauri lililofunguliwa na TANESCO kule ICSID mwaka 2004.


UZITO WA ICSIDI-2 KWENYE RIPOTI:


Hoja kuu ya Ripoti ya PAC ni kuwa fedha za Escrow zilikuwa “zimechotwa” kwa sababu makubaliano kati ya TANESCO na IPTL hayakuzangatia madai ya TANESCO yaliyopelekea kufungua ICSID-2 na uamuzi uliotolewa kwenye hukumu ya hiyo kes/shauri la ICSID-2. Tumeona hakuna ICSID-2 lakini uamuzi wa hukumu ya ICSID-2 imetumiwa kujenga hoja kuu mara kadhaa kwenye ripoti. Hiyo hukumu imetajwa kwenye ukurasa wa 6 (mara mbili), 23, 26, 34, 40 (mara mbili).


HITIMISHO:

Tuhuma kubwa zinatolewa kuwa fedha za Escrow zilitolewa kuilipa IPTL bila ya kuzingatia maamuzi ya kesi/shauri ICSID-2 kwenye kurasa hizo zote juu. ICSID-2 haiko, na hukumu ya ICSID-2 na tuhuma zote zinazohusisha ICSID-2 nazo ni TUHUMA ZA UONGO. Ripoti ya PAC imelidangaya Bunge na Taifa zima kwa ujumla.
Documents zote hapa: http://www.orcis.com/escrow

*Imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Salim Khatri.
 
Rais ndo amewapeleka chaka...na kama kamat ya zitto i mean PAC ndo unadai imewaingza choo cha sokon bas ccm ndo imekupeleka uko wapo weng kwny hyo kamati.

Cha msingi ujue saiv hii nchi haiongozwi na sheria bali watu uongoza sheria. Ucwe shabaki wakt huo mgao ata mia ujapata...pesa zmepgwa ata kama rais anavyodai hazkua za uma lakn ujue zltoka tanesco
 
Hata mjitetee vipi hapa kwenye TEGETA ESCROW kuna ufisadi na wizi uliopitiliza na kama ndy hivyo mbona utetezi wa serikali uliotelewa na Pro MUHONGO haukutaja haya unayo tuambia. TATIZO NINALOLIONA HAPA MPO WATZ WACHACHE SANA AMBAO MNACHEZA NA MAISHA/UHAI WAZALENDO WENGI WA NCHI HII YA HAYATI BABA WA TAIFA - Lala mahali pema peponi Baba, ila taifa lako kwa sasa amani haipo kabisa.

Tafuta Hansard za bunge kwenye tovuti yao ndio utaelewa alichokisema na ambacho hakukosema mhongo,tatizo jamaa zenu walikua hawataki mumsikie siku ile ndio mana walikua wanazomea na kupiga kelele mwanzo mwisho,hawakutaka muyajue haya ambayo muhongo aliyasema pia,kuzomea ilikua ni strategy ya ku cover-up uongo wa PAC .
 
Rais ndo amewapeleka chaka...na kama kamat ya zitto i mean PAC ndo unadai imewaingza choo cha sokon bas ccm ndo imekupeleka uko wapo weng kwny hyo kamati.

Cha msingi ujue saiv hii nchi haiongozwi na sheria bali watu uongoza sheria. Ucwe shabaki wakt huo mgao ata mia ujapata...pesa zmepgwa ata kama rais anavyodai hazkua za uma lakn ujue zltoka tanesco

Sichezi wala kuchezeshwa ngoma ya siasa kama wewe ndio mana nilikwepa kutaja jina Zitto nikataja PAC
 
Hiviiiiiiii,let say ni kweli hela zote ni za IPTL,swali la msingi la kujiuliza ni, je hakuwa na kazi nazo hadi agawe kama njugu kama kweli zote ni halali yake kweli?????,inawezekana hela yako halali ukaigawa kama njugu kwa kiasi hcho kweli,hakuna mazingira ya rushwa kweli?????

Hivi rushwa ya aina gani hii mpaka maaskofu waadilifu wa kikatoliki wakaichukua!sijawahi kuiona rushwa sampuli hii,anyway,tujikite kwenye hoja na facts zilizowasilisha na kuzikataa kwa facts pia,badala ya kufanya ujanja wa juzi-divert,its not gonna help at all.
 
Hiyo ni mosi.

Pili: Hivi iweje huo mgao ufanyike kwa formula ambayo hata hauhitaji kuumiza kichwa kugundua kuwa kuna kamchezo hapo...1.6b, 800m, 80m, 40m,3.2b.

Tatu: Mgao huo umefanyika kwa viongozi flan flan wa serikali kutoka wizara na idara zinazo husika na hilo sakata kwa njia moja au nyingine...kwanini??

Nne: Iweje shirika la umma likae kimya kwa miaka saba kuchukua hatua ambazo zingekua na manufaa kwa taifa na serikali ikae kimya tu inaangalia kama vile inataka tanesco waharibikiwe?? Nashangaa eti leo Kiongozi Mkuu anatumia muda mrefu kutueleza sakata zima lilivyokua kama vile tanesco wenyewe hawana midomo.

Kuna Mdau amepost uzi anasema hao viongozi walikua na hisa iptl. naanza kuamini kwa kiasi flani kuwa kuna kaukweli maana ukiangalia mgao huo ulivyokaa...sio bure.

Wizara ya ardhi na makazi ambayo waziri wake ametajwa kupokea hiyo 1.6b wizara yake inahusika Vipi kwa njia moja au nyingine?mi siioni connection hapo,nisingeshangaa "mgao" angetajwa kuupata waziri wa fedha(BOT),gavana wa BOT,Waziri wa nishati na watendaji wengine pale wenye dhamana ya maamuzi pale wizarani n.k. lakini wizara ya ardhi na waziri husika alikua na ushawishi gani uliopelekea hela zitoke BOT siipati picha sawasawa.au mawaziri wa fedha,madini Makatibu wao wakuu na gavana wa BOT Wao walijitolea tu burebure kuwasaidia jamaa walipwe halafu wao wasipewe mgao wowote! Kuna kitu kina Zitto wanakijua hapa lkn hawataki na sisi tujue.
 
Wewe ni mmoja wa wale waliopewa lap top na muhungo ili kila siku muwe huku kupotosha umma? pambaf! Nyoko mkubwa!
 
Watu kama mengi ni mafisadi yasiokoma nadhani tuanze utaratibu wa kuwauwa pengine watatia aibu.

Nadhani tungeanza na Lowassa,Singasinga ,Chenge,Muhongo halafu tukaja kwa Mengi au wasemaje?
 
Nchi iko mikononi mwa mafisadi hivyo wanafanya watakavyo wakati wowote ule huku usalama wa mafisadi ukiwahakikishia usalama wao. EPA, utoroshwaji wa wanyama, kagoda, Meremeta, Rada, ndege ya Rais, Richmond/Dowans, Mikataba ya madini, Escrow, uuzwaji wa nyumba, IPTL, Kiwira Coal Mining na madudu mengine chungu nzima. Eti tuna usalama wa Taifa!!! kwi kwi kwi kwi lol!!!

Kwa sasa ipo chini ya Singasinga,maana anauwezo hata wa kumuamuru Rais asitekeleze maazimiao ya bunge.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom