UONGO WA RIPOTI YA PAC KUHUSIANA NA SAKATA LA ESCROW - PART 1.
Ripoti ya PAC Ukurasa wa 6 (kwa nakala iliyokuwa kwenye tovuti ya Bunge) unanukuliwa hivi:
Mheshimiwa Spika, gharama hizi zilikoma kulipwa moja kwa moja kwa IPTL mwaka 2007 baada ya TANESCO kubaini kuwa IPTL inakokotoa gharama hizo kwa msingi wa USD 38.16 milioni (ambayo ni sehemu ya mkopo wa USD 105 milioni uliochukuliwa na wanahisa kutoka Umoja wa Mabenki ya Malaysia (Consortium of Malaysian Banks) ambao baadaye ulinunuliwa na Standard Chartered Bank ya Hong Kong) badala ya mtaji wa uwekezaji wa kiasi cha Sh. 50,000 uliosajiliwa BRELA na hivyo kufanya tozo ya capacity charges kuwa kubwa. Endapo ungetumika mtaji wa uwekezaji wa Sh. 50,000/= katika kukokotoa capacity charges TANESCO ingekuwa inalipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa Spika, kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha capacity charges kilichokuwa kinatozwa na IPTL mnamo mwaka 2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya capacity charges. Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo.
Mheshimiwa Spika, mpaka tunapowasilisha Taarifa hii Bungeni, Uamuzi wa ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa, hivyo TANESCO wanaendelea kulipa USD. 2.6 milioni (sawasawa na shilingi 4,511,000,000/= kwa mwezi) kila mwezi kama capacity charges kwa IPTL izalishe au isizalishe umeme. Hivyo, utekelezaji wa Mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya IPTL na TANESCO umetawaliwa na migogoro toka ulipoanza mpaka sasa.
NOTE:
Paragraph ya kwanza iliyonukuliwa hapo juu inadai mwaka 2007 TANESCO ilibaini tatizo halafu kwenye paragraph inayofuatia TANESCO ikaamua kufungua shauri ICSID mwaka 2004 kutokana na kutoridhishwa yale waliyoyabaini mwaka 2007. Tatizo linagunduliwa 2007 halafu unaenda kulifungulia shauri ICSID mwaka 2004?
FACTS:
Hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa ICSID mwaka 2004 na TANESCO.
Kesi pekee iliyopata kufunguliwa ICSID na TANESCO ni ile kesi/shauri namba ARB/98/8 iliyofunguliwa mwaka 1998 na kutolewa uamuzi mwaka 2001. Kesi/shauri hilo linarejewa (referred as) kama ICSID-1 kwenye Ripoti ya PAC.
USHAHIDI:
Ripoti ya PAC haijaweza kutuambia hiyo kesi iliyofunguliwa mwaka 2004 na kurejewa kama ICSID-2 ilikuwa kesi/shauri namba ngapi. Kwenye Ripoti yaPAC, ICSID-1 ilitajwa kama kesi iliyofunguliwa mwaka 1998 na namba yake kutajwa kama ARB/98/8 lakini Ripoti hiyo hiyo imeshindwa kutuambia namba ya kesi ya ICSID-2.
Hivyo hivyo, hukumu ya kesi/shauri la ICSID-1 iliambatanishwa kwenye Ripoti ya PAC kama Kiambatanisho Na. 2 lakini Ripoti hiyo ya PAC haikuambatanisha hukumu ya hiyo kesi ICSID-2.
Hata kwenye tovuti ya ICSID, hakuna kesi/shauri lolote lililofunguliwa na TANESCO 2004 ama kutolewa hukumu/maamuzi February 2004. Isitoshe hakuna kesi/shauri lolote lilifunguliwa na TANESCO zaidi ya ile kesi/shauri la ICSID-1.
HUKUMU YA ICSID-2 INACHANGANYWACHANGANYWA:
Kwanza kwa sababu kulikuwa hakuna na kesi/shauri lililofunguliwa na TANESCO mwaka 2004 ICSID, ina maana pia kulikuwa hakuna hukumu ya hiyo kesi/shauri. Japo hiyo hukumu haipo lakini hukumu ya hiyo kesi/shauri imekuwa ikitajwa mara kadhaa. Kwenye paragraph ya pili hapo juu hiyo hukumu ya kesi isiyokuwepo inaelezwa kama Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo na kwenye paragraph inayofuatia kama Uamuzi wa ICSID-2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa.... Kuna tofauti ya kukubaliana kanuni ya ukokotoaji na kukutoa upya. Kwa kiengereza ni agree on formula to calculate na recalculate.
TAREHE YA HUKUMU YA ICSID-2
Ukurasa wa 6 wa Ripoti ya PAC ulidai kuwa mnamo mwaka 2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga na kwenye Ukurasa wa 34 wa Ripoti ya PAC inadai inadai .. (a) Kutekelezwa kwa uamuzi uliotolewa na Kituo cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Kimataifa (ICSID) mwezi Februari 2004 (ICSID 2). Aidha ICSID 2 ilielekeza TANESCO na IPTL kukokotoa upya kiwango cha capacity charges. Ni vigumu kuamini kuwa shauri linafunguliwa ICSID mwaka 2004 (hata kama lilifunguliwa tarehe 1 January 2004) likaja kupata ufumbuzi February 2004. Kama ilivyoelezwa hapo juu kulikuwa hakuna shauri lililofunguliwa na TANESCO kule ICSID mwaka 2004.
UZITO WA ICSIDI-2 KWENYE RIPOTI:
Hoja kuu ya Ripoti ya PAC ni kuwa fedha za Escrow zilikuwa zimechotwa kwa sababu makubaliano kati ya TANESCO na IPTL hayakuzangatia madai ya TANESCO yaliyopelekea kufungua ICSID-2 na uamuzi uliotolewa kwenye hukumu ya hiyo kes/shauri la ICSID-2. Tumeona hakuna ICSID-2 lakini uamuzi wa hukumu ya ICSID-2 imetumiwa kujenga hoja kuu mara kadhaa kwenye ripoti. Hiyo hukumu imetajwa kwenye ukurasa wa 6 (mara mbili), 23, 26, 34, 40 (mara mbili).
HITIMISHO:
Tuhuma kubwa zinatolewa kuwa fedha za Escrow zilitolewa kuilipa IPTL bila ya kuzingatia maamuzi ya kesi/shauri ICSID-2 kwenye kurasa hizo zote juu. ICSID-2 haiko, na hukumu ya ICSID-2 na tuhuma zote zinazohusisha ICSID-2 nazo ni TUHUMA ZA UONGO. Ripoti ya PAC imelidangaya Bunge na Taifa zima kwa ujumla.
Documents zote hapa:
http://www.orcis.com/escrow
*Imeletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Salim Khatri.