Escrow account ni uhujumu uchumi kwa Sethi, Rugemalira lakini siyo kwa SIMBA TRUST?

Kwa nini tutegemee utashi wa mtu kwenye kupambana na Ufisadi. Kwa sheria zetu zinategemea mapenzi ya mtu kutekelezwa? Madhara yake ndiyo haya tunaambiwa kwamba wengine tusiwataje hata majina yao tuwaache wapumzike!
Sasa ulitaka tutegemee utashi wa nini?
Si walikuwepo hao mlikuwa mnanegua mauno BUNGENI kuwamiss na waliizima hii hoja?
 
JPM anajua kweli kucheza na akili za watanzania, sasa amehamisha mziki wa makinikia umesahaulika now tunaimba IPTL...wale kina Masamaki imekuwa zilipendwa watu wengi hawapendi mambo yaliyopita, atapigiwa makofi kwelikweli kwa kuminya majipu ila kuayatumbua hathubutu..
Ikifika 2020 atajikuta ana maswali mengi ya kuulizwa lakini majibu hana
 
9724cebdc604af4e6507c0247ebd4228.jpg
Ccm ilisema haiwezi kuwachukulia hatua hawa.
 
Hivi Benki ikikosea wakaiingiza hela kwenye account yangu,nikazitoa nitashitakiwa kwa Wizi?au nitaambiwe nizirudishe tuu.kwa kesi yetu vipi watakaosema walizikuta tuu hizo hela kwenye account zao na hakuna ushahidi wa u husika wao.
 
Kama upande mwingine wa umiliki haijashutumiwa basi hiyo kesi hakuna kitakachoendelea na hao watarudi tu uraiani

Ni mtaji wa kisiasa tu unatengenezwa kujiandaa na 2020
 
Kwa nini tutegemee utashi wa mtu kwenye kupambana na Ufisadi. Kwa sheria zetu zinategemea mapenzi ya mtu kutekelezwa? Madhara yake ndiyo haya tunaambiwa kwamba wengine tusiwataje hata majina yao tuwaache wapumzike!
Mwajiriwa wetu anapotupangia waajiri wake jinsi atakavyofanya kazi huo ni utovu wa nidhamu.

Tuendelee kunoa ala zetu 2020 siyo mbali
 
Acheni kiherehere. Mlijua kama Seth na Ruge wangefikishwa mahakamani jana?
Kinachowafanya muamini huko kwingine Ngosha hatafika ni nini?
kuna watu wa ajbu sana dunia hii. hata kufika hapa ni kwa sababu ya mayowe ya watu wengine (najua wewe sio mmoja wapo) hivyo hata kufika huko kwingine mayowe yanahitajika. Kama wewe huoni haja haja ya kuwachagiza/kuwahimiza wakubwa wasogee mbele zaidi, kaa pembeni
 
Back
Top Bottom